hapo ndio unakosea kaka cuf haaihitaji chadema bali ccm! si kuna muafaka wa ccm na cuf?
cuf wangekua wanawahitaji chadema wasingekubali ule upuuzi waliofanya kule zanzibar
kilichofanyika zanzibar ni kuua demokrasia wakati chadema ni chama cha demokrasia
Naona sasa Chadema tunalewa umaarufu! na ipo hatari kubwa sana kwa chama tukiendekeza fikra kama hizi.....
sidhani kama cuf wanaweza kuunda upinzani na vyama vidogo sababu jumla ya wabunge wao wote ni 39(cuf 34) nccr 4, na tlp 1 wakati chadema wanawabunge 45!!
Kutofahamu maana ya kuunda kambi ya Upinzani!Example
(1)...........
(2).............
(3)..................
CUF wao si Zanzibar tu ndio wana wabunge wengi, mstakabali wa mapambano haya hautegemei kushirikiana na makafiri.
cuf=34,UDP=1,TLP=1,NCCR=4 total=40. sheria inaruhusu min ya wabunge 42, kuna uwezekano cuf wakaongeza viti viwili kati ya 7 ambavyo havina mshindi so far. kama hii ni njama ya ccm then cuf watawezeshwa washinde kwa kuwa mpaka sasa wao ndo wamiliki wa NEC. Malengo maovu mara nyingi huwa yanafeli hata yakifanikiwa huwa ni kwa malengo maalumu(i mean Mungu hawezi kuruhusu maovu mengi yatendeke kuliko tunavyoweza kuyakabili)sidhani kama cuf wanaweza kuunda upinzani na vyama vidogo sababu jumla ya wabunge wao wote ni 39(cuf 34) nccr 4, na tlp 1 wakati chadema wanawabunge 45!!
safi mkuuKutofahamu maana ya kuunda kambi ya Upinzani!
Sasa kama Chadema wakijiweka wao pekee wataweza, kuna muswada au hoja gani wanaweza kuusimamisha ikiwa idadi yao haifikia hata robo?..Je wanafanya haya kwa sababu gani ikiwa lengo ni kuwakilisha wananchi kisha mkashindwa hata kupitisha moja ktk Upinzani maana hamna kura za kutosha. Inakuwaje leo Bungeni bado is about Chadema na sio kulenga jukumu kubwa la kuwakilisha wananchi....
Sijui kama ni CUF haitaki kushirikiana na CHADEMA, au CHADEMA haitaki kushirikiana na CUF, lililowazi ni kuwa tangu 1995 upinzani hautaki kushirikiana na huu ni mwendelezo tu wa tabia ya upinzani TZ. mmoja kasema hapa kuwa hii inatokana na kutoaminiana, lakini pamoja na hilo, si CCM wala si upinzani, bado TZ tuna tatizo la ubinafsi, choyo, chuki, ujimbo, udini, ukabila na tamaa (za ukubwa) binafsi.
Kwa mwendendo huu, Watanzania tusahau kujinasua kutoka mikono ya umasikini na zaidi kutoka makucha ya udikteta wa CCM, kwani CCM kila upinzani unapogawanyika hiyo ndio furaha yao. Fikiria kama upinzani ungeliungana tangu 1995 tungelikuwa wapi sasa? Kumbukeni upinzani, "Umoja ni Nguvu".
CHADEMA kuungana na CUF ni sawa na kuuwa upinzani! Iko wazi CUF ni CCM B, kuna makubaliano ya siri kati yao. Time will tell
Nilukwa na matumaini ya Mabere Marando angekuwa spika lakini kwa mpasuko huo Marando asahau.