Bungeni: TLP, CUF, UDP na NCCR Mageuzi navyo vyaungana

Cuf inawauma sana kwa Chadema kuwa na nguvu kuliko wao.
Hivyo vyama mamluki Walichofanya ni utaahira mtupu.
 
jamani ivi kweli unategemea mtu kama Mrema atajiunga upinzani ni siri gani upinzani wataongea asijipendekeze kwa JK Na kumuambia, mimi nafikiri Bado kuna shida upinzani wenyewe wanatuhumiana na hawatuoneshi nia ya kukaa pamoja na kuweka mikakati isipokuwa baadhi yao wanakua vibaraka ndani ya bunge, chamsingi tutegemee mabadiliko makubwa kutoka CHADEMA kupitiwa wabunge wake na sio upinzania kwa ujumla wake,
for sure we need to pray for our country.

Mzee Gomezi
 
hapo ndio unakosea kaka cuf haaihitaji chadema bali ccm! si kuna muafaka wa ccm na cuf?
cuf wangekua wanawahitaji chadema wasingekubali ule upuuzi waliofanya kule zanzibar
kilichofanyika zanzibar ni kuua demokrasia wakati chadema ni chama cha demokrasia

wewe umesema kweli maana cuf walikubari vyeo vya kuajiliwa na ccm kuliko wapigania haki wa watu wao wanyonge
sasa wamekuwa daraja la ujinga la ccm kwenye kulizamisha taifa kwenye upuuzi mwingi
 
CHADEMA Haiwahitaji CUF hata kidogo hata kama wangekuwa na wabunge wachache. Kumbuka kinachoongoza chadema si idadi ya wabunge au kujipendekeza kwa CCM bali ni NGUVU YA HOJA WALIZONAZO BUNGENI. TAKE YOUR TIME AND MAKE A FOLLOW UP IN THE 10TH PARLIAMENTARY SESSIONS. THEY ARE MEN AND WOMEN OF PEOPLE

  1. ROSE KAMILI
  2. TUNDU LISU
  3. NDESAMBURI
 
sidhani kama cuf wanaweza kuunda upinzani na vyama vidogo sababu jumla ya wabunge wao wote ni 39(cuf 34) nccr 4, na tlp 1 wakati chadema wanawabunge 45!!

kwani kanuni za bunge zinasemaje kuhusu nani anaweza kuunda kambi ya upinzani?
 
Example
(1)...........
(2).............
(3)..................
Kutofahamu maana ya kuunda kambi ya Upinzani!

Sasa kama Chadema wakijiweka wao pekee wataweza, kuna muswada au hoja gani wanaweza kuusimamisha ikiwa idadi yao haifikia hata robo?..Je wanafanya haya kwa sababu gani ikiwa lengo ni kuwakilisha wananchi kisha mkashindwa hata kupitisha moja ktk Upinzani maana hamna kura za kutosha. Inakuwaje leo Bungeni bado is about Chadema na sio kulenga jukumu kubwa la kuwakilisha wananchi....
 
binafsi, napendekeza na kushauri CHADEMA, ishirikiane na wapinzani wenzao.. kwani umoja ni nguvu (na ni nguvu kama hakuna wasaliti).
Chonde chonde CHADEMA, tafadhali shirikianeni na wenzenu...
 
CUF wao si Zanzibar tu ndio wana wabunge wengi, mstakabali wa mapambano haya hautegemei kushirikiana na makafiri.

CUF nao hawaishi kuwashangaza watanzania. Huko nyuma Chadema waliuunga mkono mgombea wa CUF wa urais Lipumba, halafu bungeni walimuunga mkono kiongozi wao wa kambi ya upinzani Hamad Rashid. Kinyume chake CUF badala ya kuwaunga mkono Chadema kama walivyowaunga mkono wao, wakaweka mgombea wao wa urais Lipumba japo hakuwa na mvuto kwa wapiga kura wengi. Pia wanaamua kuacha kuungana na Chadema kwenye kambi ya upinzani bungeni tofauti na wao walivoungwa mkono na Chadema bunge lililopita, hapa CUF tuhesaba ni CCM B. Ukombozi wa watanzania utaletwa na Chadema na siyo CUF, labda wajirudi lakini CUF mtoto si riziki tayari.
 
mie nashangaa ile serikali ya upinzani Bungeni mbona hamna mtu wa CUF yaani ni Mbowe, Zitto na Lissu tu? wajameni compmromise inahitajika hata kuwalainisha wenzio ndo mambo yanaenda! Ila nina wasi na Zitto ni kama ametumwa maana yeye kuwa kwenye hiyo list ni kama alilazimisha na kusababisha wengineo toka vyama vya upinzani kusahaulika! Mara nyingi kiongozi wa chama ndie huwa kiongozi wa chama/upinzani katika Bunge pia haswa kama ni Mbunge! Tufahamu hilo!
 
Mh Mbowe alisikikika akisema CHADEMA kitashirikiana na vyama vingine vya upinzani ! Leo CUF wanakataa ushirikiano.....kosa lipo wapi kwa CHADEMA?
 
sidhani kama cuf wanaweza kuunda upinzani na vyama vidogo sababu jumla ya wabunge wao wote ni 39(cuf 34) nccr 4, na tlp 1 wakati chadema wanawabunge 45!!
cuf=34,UDP=1,TLP=1,NCCR=4 total=40. sheria inaruhusu min ya wabunge 42, kuna uwezekano cuf wakaongeza viti viwili kati ya 7 ambavyo havina mshindi so far. kama hii ni njama ya ccm then cuf watawezeshwa washinde kwa kuwa mpaka sasa wao ndo wamiliki wa NEC. Malengo maovu mara nyingi huwa yanafeli hata yakifanikiwa huwa ni kwa malengo maalumu(i mean Mungu hawezi kuruhusu maovu mengi yatendeke kuliko tunavyoweza kuyakabili)
 
Sijui kama ni CUF haitaki kushirikiana na CHADEMA, au CHADEMA haitaki kushirikiana na CUF, lililowazi ni kuwa tangu 1995 upinzani hautaki kushirikiana na huu ni mwendelezo tu wa tabia ya upinzani TZ. mmoja kasema hapa kuwa hii inatokana na kutoaminiana, lakini pamoja na hilo, si CCM wala si upinzani, bado TZ tuna tatizo la ubinafsi, choyo, chuki, ujimbo, udini, ukabila na tamaa (za ukubwa) binafsi.
Kwa mwendendo huu, Watanzania tusahau kujinasua kutoka mikono ya umasikini na zaidi kutoka makucha ya udikteta wa CCM, kwani CCM kila upinzani unapogawanyika hiyo ndio furaha yao. Fikiria kama upinzani ungeliungana tangu 1995 tungelikuwa wapi sasa? Kumbukeni upinzani, "Umoja ni Nguvu".
 
Kitu ambacho CHADEMA WANAJIFANYA WAMEKISAHAU, Hususan viongozi wake Mh. Mbowe, Mh. Dr. Slaa na Mh. Zitto, ni kuwa CUF ni chama madhubuti nchini ambacho katika uchaguzi uliopita kililemewa na hali ya siasa za Zanzibar katika uchaguzi uliopita na pia chaguzi zote zilizotangulia. Ningelikuwa MIMI ni WAO, nisingelithubutu kumeza mbegu mbaya ya kukiita chama chochote cha UPINZANI kuwa ni CCM B. Kosa hili liliwahi kufanywa na Profesa Lipumba na CUF lakini walijirekebisha na kuanza kutaka muungano wa vyama.
Hivyo basi Viongozi wa CHADEMA wanapaswa kufanya kazi ya ziada na ngumu ya kutambua kwamba baada ya maanguko ya NCCR-Mageuzi 1995, TLP 2000, CUF 2005 kusambaratishwa na CCM wanayo dhamana kubwa ya kuwakilisha maslahi ya kambi nzima ya upinzani ndani ya Bunge na nje kwa maslahi ya taifa.

Wacha tusubiri tuone, huenda wakafanikiwa, Ila kwa muono wangu CHADEMA + WAPINZANI WANAHITAJIANA, hayo ya kuitana CCM B, C mpaka Z hayatawasaidia. Ni upungufu kumeza propaganda ndogo kiasi hicho hata bunge halijatimiza mwezi, kuna tetemeko linakuja bado.:tape:
 
Nilukwa na matumaini ya Mabere Marando angekuwa spika lakini kwa mpasuko huo Marando asahau.
 
Kutofahamu maana ya kuunda kambi ya Upinzani!

Sasa kama Chadema wakijiweka wao pekee wataweza, kuna muswada au hoja gani wanaweza kuusimamisha ikiwa idadi yao haifikia hata robo?..Je wanafanya haya kwa sababu gani ikiwa lengo ni kuwakilisha wananchi kisha mkashindwa hata kupitisha moja ktk Upinzani maana hamna kura za kutosha. Inakuwaje leo Bungeni bado is about Chadema na sio kulenga jukumu kubwa la kuwakilisha wananchi....
safi mkuu
labda tatizo ni utayari wa kila mhusika je hapo ni vipi?
 
Sijui kama ni CUF haitaki kushirikiana na CHADEMA, au CHADEMA haitaki kushirikiana na CUF, lililowazi ni kuwa tangu 1995 upinzani hautaki kushirikiana na huu ni mwendelezo tu wa tabia ya upinzani TZ. mmoja kasema hapa kuwa hii inatokana na kutoaminiana, lakini pamoja na hilo, si CCM wala si upinzani, bado TZ tuna tatizo la ubinafsi, choyo, chuki, ujimbo, udini, ukabila na tamaa (za ukubwa) binafsi.
Kwa mwendendo huu, Watanzania tusahau kujinasua kutoka mikono ya umasikini na zaidi kutoka makucha ya udikteta wa CCM, kwani CCM kila upinzani unapogawanyika hiyo ndio furaha yao. Fikiria kama upinzani ungeliungana tangu 1995 tungelikuwa wapi sasa? Kumbukeni upinzani, "Umoja ni Nguvu".

CUF NDIO WAMEKATAA KUSHIRIKIANA NA CHADEMA, amesema John Mrema licha ya jitihada za Mwenyekiti wa Chama Mh. Mbowe.

SOURCE: TBC and STAR TV
 
CHADEMA kuungana na CUF ni sawa na kuuwa upinzani! Iko wazi CUF ni CCM B, kuna makubaliano ya siri kati yao. Time will tell

kikwete+lipumba+seif+1.jpg

Shekh! siye twala ubwabwa sahani mojaa ati yanini tugombane? we wala bara siye twala zenji!
 
Nilukwa na matumaini ya Mabere Marando angekuwa spika lakini kwa mpasuko huo Marando asahau.

siyo mpasuko mkuu ni lazima tujue kuwa Chadema siyo wajinga hata wao wanaona umuhimu kuwa pamoja
lakini believe or note Chadema wako alone on the move cose i thenk you may know that the other side are the same as
ccm small house
 
Nikisoma kanuni ya bunge na 14 na 15, sioni kama kuna room ya CUF na washirika wake kuwa na kambi ya tatu bungeni. Nahisi watakuwa upande wa chama tawala, ila wanaogopa kukiri haya kwa sasa wasipigwe madongo na watanzania. Ni matendo yao yatadhihirisha hili
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom