KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!
Jamani eti Bungeni kuna wasomi!*
Nimemuangalia kiumbe aitwaye Mwigulu akibwabwaja. Pia nimemsikia Tundu akitumia neno 'silly.' Neno hili silly hutumika sana nchi za magharibi wakati wa uchaguzi kwamba ni silly moment. yeye kaamua kusema wakati wa bajeti ni silly time.
Ubaya mkubwa wa Lisu ilikuwa kuanza kushambulia moja kwa moja CCM badala ya kuishambulia bajeti ya hovyo iliyo bungeni ili angalau apate kuungwa mkono na baadhi ya wana CCM. Wapo wengi tu wasiyopenda ujinga kama huo ulioletwa bungeni.
Tatizo la Mwigulu naona hajapata exposure ya kutosha dunia hii. Hana mifano ya kweli, alichonacho ni theories za mambo aliyoyasoma darasani. Anadhani yanamsaidia kujadili bajeti bila fahamu kwamba shida ya mwanakijiji siyo supply-demand curve.
Hili ni tatizo linaloongezeka kwa watu wengi wenye viji-digrii vyao pale bungeni. wanajisahau na kuanza swaggers za taaluma zao wakidhani ndo umaarufu. Kwa mtu kama Mwigulu naona hakuzoea kushangiliwa maana aliposhangiliwa ndo kabisaaa! akaongeza manjonjo kama mcheza mdundiko. Nikimuangalia hana jipya zaidi ya theories za vitabuni na internet. Amejiita senior economist wa bank kuu. Mimi mara moja nika google jina lake kama limewahi kuchangia uelewa wowote wa uchumi dunia hii. Wapi! nimejisemea mwenyewe, rubbish Mwigulu
Ndo maana sasa wakaingia na akina Komba kwa kudhani kushangiliwa ndo kufanya vizuri.*
Mwigulu,*Komba, et al., nawaomba waache kusubiri kushangiliwa. Hakuwapi lolote katika jamii. Kuna watu bungeni wana taaluma ambazo wakizitumia hakuna hata atakayewaelewa.