tubadilike-sasa
JF-Expert Member
- Jan 31, 2012
- 681
- 167
Kuna kitu CCM imemeza(epa-kagoda,radar,kuuza nyumba za viongozi,ubadhirifu wa rasilimali,impunity etc)hakishuki tumboni wala hakiwezi kutapikwa. Kukabwa huko ndiko kunakomfanya Mwigulu aropoke,nadhani hajaropoka kwa sababu ya hiyo bajeti ya upinzani tu,kuna sumu na makandokando mengi yamemjaa mwilini na akilini kama yalivyowajaa viongozi wengi wa CCM,ndio maana baada ya kusema alishangiliwa sana na kupongezwa na wenzake na hata mwenyekiti alipeta upande ule mwingine ulipotaka mwongozo. Hapo ndipo CCM inapokosea ikidhani kuwa hayo yanayoendelea bungeni sisi wananchi wa kawaida hatuyaoni. Kuna mambo CCM wamekosea,wayasahihishe na wala hawatahitaji kutokwa na misuli ya shingo na mapovu kama alivyofanya Mwigulu leo pale bungeni