Amewaita wenzake waigizaji lakini yeye ni full comedian na kiukweli amekidhalilisha Mgamba sana. Hivi wale wabunge wa CCM wenye busara walikwenda wapi hivi hawa ndo waliobaki?
amesema ukichukua kima cha chini wanachopendekeza CDM 315,000 ukizidisha na namba sijui ipi (kwa sababu hakuitaja) unapata zaidi ya bilioni tisa.
akachukua namba ingine sijui gani na akazidisha na namba sijui gani akapata zaidi ya trilioni 15 ambayo ni zaidi ya trilioni 15 kwa hiyo aka-conclude hiyo budget mbadala ni absolutely rubbish
Note: hakutaja namba yeyote naona zote alikua anawaza tu kichwani sie anatupa majibu, kwa kifupi jamaa katoa povu sana
Nimesikiliza Bunge la budget kweli lugha zinazotumika mwisho wake naona nchi yetu inaelekea kubaya sana kwa mtu aliyesikiliza bunge na leo jioni utakubaliana na mimi kabisa kuwa maadili ndani ya waheshimiwa wa bunge imeisha na hawajui kama wananchi tunawasikiliza na sii hivyo tu hata nchi za nje wanasikiliza nini kinaendela ndani ya bunge letu. Swali kweli tutafika?
1. Anasema OC ni kwa ajili ya mambo kama katiba mpya, kulipia fidia watu wanaohamishwa. Sasa kwanini wasitaje ni kiasi gani kinaenda kwenye fidia au katiba badala ya kusema OC? Nini maana ya budget kama husemi how much is going kwenye kila area? Kila mtu anajua OC ndiko watu wanakula.
2. Mwigulu anasema ahadi ya serikali katika mpango wa maendeleo 2011/16 kutenga 35% inajumulisha human capital investiment yaani kusomesha wanafunzi! hivyo serikali kuweka 30% ni kwamba hiyo nyongeza ya 5% inakuwa kwenye human capital. Kama ndivyo kwa nini serikali ilisema 35% na sasa wanajitetea kuwa kuna human capital investment baada ya kubanwa kutenga hela hafifu?
3. Lakini kubwa, Mwigulu anaweza kusema kwa nini Tanzania ni maskini?
Huyu Mwigulu katibu wa Uchumi wa CCM ana matatizo ya akili jamani au nyie mmemuelewaje?
Badala ya kuchangia Bejeti ya mwaka 2012/2013 yeye anajibu hoja za Tundu Lissu tu, Why????
Aliamua kutoa matusi na kusahau kilichompeleka pale Bungeni. Nadhani itabidi apimwe akili huyu mtu na pia nashangaa kwanini CCM wamempa cheo kikubwa ndani ya chama!!!!
Napata wasi wasi na operating system (O/S) ndani kichwa chake. Sikuona sababu ya kutumia dakika 10 ya kuchangia bajeti hii kwa kujibu hoja ya LISSU. Inaeonekana wananchi wa Iramba Magharibi na wenyewe wana matatizo ya akili pia kwa kumchagua Mbunge wa namna hii.
kati ya kauli ya lisu, mwigulu, na komba, ni ipi ya kuuzi zaidi? Maana lukuvi kacmama mara 1.? Wanachi tumesahauliwa nimetamani 2015 iwe kesho, zimenipa hacra sn hizi kauli.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.