Yaani sielewi kabisa, maisha ya watz bado ni ya kufikirika zaidi kuliko uhalisia. Kila siku washabiki wa UJINGA na UPUMBAVU bado wanaongezeka na hali haieleweki. Sifikiri kama kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuunga mkono bajeti ya trilioni 15 huku fedha kwa ajili ya maendeleo zikiwa ni kiasi cha trilioni tano tu, zingine trilioni 10 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida (mishahara, posho na allowances). Halafu kibaya zaidi, bado watz na WABUNGE tuliowachagua kutuwakilisha, wanaushabiki wa vyama bila ya kuzingatia UHALISIA wa mambo.
Hivi unaweza kubeza maneno aliyosema TUNDU LISSU kwa sababu tu wewe ni mshabiki au mwanachama cha ccm? Unaweza ukabeza maneno aliyoongea mbunge wa MBALALI kwa sababu tu wewe ni chama pinzani? Haiingii akilini hata kidogo.
Kweli, bajeti ni mbovu, na LISSU ameongea ukweli halisi kuwa "SHAME ON THE GOVERNMENT, SHAME ON CCM AS A RULING PARTY AND SHAME ON THE PARLIAMENT, including him". Kuna lipi baya katika maneno hayo? Japo siyo wabunge wote wanaopitisha upuuzi huu bungeni, lakini kwa sababu wengi wao wanapitisha, ni kweli,"SHAME ON THEM ALL"
Mtu kama Mwigulu na Komba, wanaongea nini? mimi hata sijaelewa. Hivi kweli, hata chadema wakichukua nchi hii sikumoja watakuwa wanaongea UJINGA na UPUUZI kama huu wa Mwigulu na Komba kwa sababu tu wao ndio wenye serikali? Mbona Bulaya ameongea vizuri sana? Au na yeye anajiandaa kwenda CDM? Mi hata sijui kama yupo mtu katika uelewa wake wa kawaida anajivunia kuwa Mtz, mimi NAVUMILIA TU, nitafanyaje ilihali nimezaliwa Mtz? Lakini in real sense, hakuna cha kujivunia hapa Bongo. Hata baada ya miaka hamsini ya kutawala, chama cha mapinduzi bado kinatoa ahadi kwa wananchi kama vyama vya upinzani. Nashangaa kweli. Badala ya kusema ni kipi wametekeleza, bado wanatoa ahadi. AIBU SANA.
Hata baada ya miaka hamsini ya kutawala, bado, serikali imeshindwa kupunguza matumizi yake, na badala yake, matumizi ya serikali yanazidi gharama ya miradi ya maendeleo. Najiuliza, ahadi za rais kikwete za meli ktk ziwa victoria, Nyasa na Tanganyika zipo kweli bajeti gani?
Kuna kitu kimenishtua, bajeti ya wizara ya ardhi na maendeleo ya makazi ya mwaka wa fedha 2011/2012 ilikuwa bilioni ishirini na kidogo hivi, lakini fedha ambazo wizara ilipokea kutoka hazina kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni bilioni nne. Sijui kuna miradi gani ilitekelezwa kwa fedha kiduchu kiasi hicho.
Seriously speaking, THERE IS NO FUTURE AND PROSPEROUS LIFE UNDER CCM GOVERNMENT!!!! Kama tumeshindwa kwenye sanduku la kura, haimaanishi watu wanaipenda ccm, tutafute njia mbadala, napendekeza MAPINDUZI YA SERIKALI, kwani hili litasiadia hata kuondoa mikataba yote ya kinyonyaji ambayo ccm imeingia na wazungu wanaoliibia taifa hili maliasili kwa ushuru kiduchu.
STK ONE,