Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigullu Nchemba anaonekana kuwanyima usingizi Wapinzani na mashabiki wao.
Je inawezekana Mbunge huyu akawa tishio kwa wapinzani?
Kwa maoni yangu mimi naona kama NI kweli wapinzani wanamgwaya Mwigullu, kwani kama siyo tishio, basi wasingehangaika naye.
Si wabunge tu wa Upinzani wanaohaha kuhakikisha CCM haufuruki kupitia kwa Mwigullu, bali hata mashabiki wao, kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii na wengine wanaonekana kutumia muda mrefu kumponda Mbunge huyo machachari wa CCM.
Lakini swali la msingi ni , je Anayoyasema Mwigullu hayana msingi au sasa Wapinzani nao wanaona kama wanashikwa pabaya na wanajaribu kutapatapa? Na kama wanatapatapa, wanaogopa nini? kwani nao wana madhambi? Ni mabaya gani hayo?