BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

BRAIN DAMAGED POOR MREMA.
Alikatazwa na daktari kufikiri ili sukari isipande.
 
wabunge wa ccm wanakera mno!!!!wanachukuwa mda mrefu sna kuongea mambo ya chama badala ya kujadili hoja,but time ll tell...hawasomi alama za nyakati kabisaa!!!!!!!
 
Waliosema amezeeka hawakukosea.....nakumbuka akajibu kua bungeni hawabebi vyuma....nadhan wadau uwalimaanisha kua akili yake imestaki
 
Nadhani tatizo la magamba ni umri wao. Nadhani asilimia kubwa ya wabunge wa magamba ni wazee hawana jipya wanataaka kubaki na status quo ili wamalizie maisha yao.

Nadhini wanajua kabisa 2015 wengi harudi maana trend sasa haiwapi tena nafasi. Kama unataka kuona hili ni kweli utajua kwa ukali wao kwenye swala la posho kufyekwa. Wamekuwa wakali kama mbogo maana wako fainali bwana.

Nadhani tuwavumilie maana for sure hamna atakeye rejea tena 2015. Na nzuri zaidi hata watoto wao hawakubaliki tena hivyo nafasi ni kwa watanzania wenye uwezo kuchukua hizi nafasi.
Nimempenda Silinde ni kijana mzuri anatia matumaini sana kwa wana mbozi.

Nadhani ni wakati mzuri wa wabunge wa cdm kuanza kugroom vijana wengine kwa ajili ya 2015 ili kuong'oa hawa wazee wa magamba.
 
Wabunge wa ccm hawapambanui kati ya mzaha na mambo serious - wanasikitisha. Ombi wabadilike kuanzia kesho au la wafunge midomo hatutawalaumu - it is a real disappointment!!!
 
mrema bado anahisi thithiem wanawenza kum consider na kumpa ulaji. anajidhalilisha kwa kutoa pumba ili magamba wamwone wa maana sijui anafaidi nini.
 
Wasiwasi wangu sio Kafulila kuwa na vielelezo au la, bali ni kwamba wakijipanga kumkomoa, watamkomoa tu maana baada ya kutoa vielelezo kura itapigwa kujua kama kakosea ama la (au kama maelezo yanajitosheleza) na kwakuwa wabunge wa CCM ni wengi basi kijana atasulubiwa. Hili linaweza kutokea, hasa kwa kuzingatia ushabiki wa kichama uliojitokeza toka hili bunge lianze.
 
CCM wanamchekea Mrema (kupe lao) wanajiona km vile wameshinda! Alafu kuna mwanamke anaropoka ropoka! Janualy makamba kaliona hilo!
Ni mchungaji huyo mama,lakini ni mtu wa kujipendekeza sana mpaka anatia kinyaa.
 
Unamsingizia hamad, kila mtu ameangalia,.hamad alielezea namna watu wa kisiwa alichotembelea walivyo busy na wanavoconcentrate katika issues zao za kujenga taifa lao na hata wakiwa wanaandamana mchana hawana muda na hivyo maandamano yao hufanyika usiku.Umetosha.

Maandamano sio kutembea tu. Lengo lake ni kufikisha ujumbe kwa jamii, sasa ukifanya maandamano usiku, huo ujumbe utawafikia vip watu? Maandamano ni mabaya kwa sababu ni ya kuwabana watawala, yangekuwa ya kuwasifia, si ajabu kila wasiopenda changamoto wangeyasifia.
Suala la msingi ni kwanini watu wanaenda kwenye maandamano, tena kwa wingi? Wasipolitafutia majibu swali hili, kupinga kwao maandamano kutakuwa ni wivu tu wa kisiasa.
 
kauli iliyotolewa hivi karibuni kuwa wabunge wa ccm watetee budget kwa nguvu zao zote inataka kuturudisha nyuma na kutaka
kuligeuza bunge kuwa rubber stamp ya kupitisha madudu yake ya ajabu ajabu ambayo hayatusaidii sisi wananchi kwani baada
ya kusubiri kwa muda mrefu kwa mara ya kwanza tumeanza kusikia bungeni maneno matamu Bungeni kama:

1. FUTA POSHO HIZI NA ZILE ZITAWAOKOLEA WANANCHI KIASI FULANI CHA FEDHA.
2. KATA/PUNGUZA KODI BADALA KODI KUONGEZEKA KILA MWAKA ILI KUWAPA WANANCHI UNAFUU WA MAISHA.

3. DENI LA TAIFA NI TISHIO KWA USALAMA NA UHURU WETU.
4. WABUNGE WANAAZA KU CHALLENGE MATUMIZI YA PESA ZA KODI ZA WANANCHI BADALA YA KUPITISHA KILA KITU CHA GOVT.

HONGERENI SANA WABUNGE KWA KUANZA KUMFIKIRIA MWANANCHI BADALA YA KUENDELEA KUTUMIKA KAMA RUBBER STAMP
YA SERIKALI KWANI SERIKALI ILISHAZOEA KULITUMIA BUNGE KM DODOKI KUPITISHA MAMBO YAO NA KULITUPA PEMBENI NOT
ANYMORE.
 
kauli iliyotolewa hivi karibuni kuwa wabunge wa ccm watetee budget kwa nguvu zao zote inataka kuturudisha nyuma na kutaka
kuligeuza bunge kuwa rubber stamp ya kupitisha madudu yake ya ajabu ajabu ambayo hayatusaidii sisi wananchi kwani baada
ya kusubiri kwa muda mrefu kwa mara ya kwanza tumeanza kusikia bungeni maneno matamu bungeni kama:

1. Futa posho hizi na zile zitawaokolea wananchi kiasi fulani cha fedha.
2. Kata/punguza kodi badala kodi kuongezeka kila mwaka ili kuwapa wananchi unafuu wa maisha.

3. Deni la taifa ni tishio kwa usalama na uhuru wetu.
4. Wabunge wanaaza ku challenge matumizi ya pesa za kodi za wananchi badala ya kupitisha kila kitu cha govt.

Hongereni sana wabunge kwa kuanza kumfikiria mwananchi badala ya kuendelea kutumika kama rubber stamp
ya serikali kwani serikali ilishazoea kulitumia bunge km dodoki kupitisha mambo yao na kulitupa pembeni not
anymore.

nakubaliana nawe lakini hii namba 2 nafikiri ungezingatia kwani kila siku kelele hichi hakitoshi kile hakitoshi wanafunzi migomo pesa hazitoshi< barabara mbovu sijui dawa< sijuwi tuongezwe mishahar lakini ukiangalia uzalishaji wetu ni bomu> si serikali si wapinzani si wanaharakati kelele ukusanyaji wa kodi< huko ndiko kwenye uhai wa taifa>
 
Pamoja na ha hayo Ngekewa, kodi ya wastani pamoja na matumizi yanayotoa vipaumbele kwa mambo kulingana na umuhimu wake, pamoja na kuziba mianya ya wizi kwa kufanya pesa za watanzania zifike mahali zilipoelekezwa na kufanya kazi husika, vitasaidia kwa kiasi kikubwa kukidhi sehemu kubwa ya mahitaji yetu
 
MBUNGE wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila jana jioni alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kuwataja wabunge wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuomba rushwa katika halmashauri ambayo hakuitaja.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano, Kafulila aliwataja Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel wote wa CCM akidai kwamba aliwakamata wakiomba rushwa kwa viongozi wa halmashauri.

Wakati akitaja majina hayo, Kafulila nusra aingie katika mgogoro na Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene ambaye alikuwa akimwamuru kukaa chini kutokana na muda wake wa kuchangia kumalizika. Kafulila alikuwa akiendelea kuzungumza bila kujali kengele ya pili iliyopigwa kuashiria kwamba muda wake wa kuzungumza ulikuwa umekwisha.

"Mheshimiwa Mwenyekiti kwa wakati wa sasa ni vigumu kusimamia matumizi kwani mfumo wetu wa uongozi unaruhusu ufisadi, wapo viongozi, mawaziri, wabunge wanaomba rushwa...." alisema Kafulila na kuamsha zogo ambalo liliambatana na sauti zisizo rasmi katika ukumbi wa Bunge zikiuliza ".....wapo humu humu?" Kafulila alijibu "Ndiyo..."

Sauti moja ilisema wataje, hapo ndipo aliposema "....Wapo kina Zambi, Badwel, nimewakamata na nimechukua hatua, hatuwezi kuendelea namna hii," kisha akaketi.

Baada ya dakika chache tangu alipoketi, Kafulila alionekana akiteta jambo na Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali na Augustine Mrema wa Vunjo na baadaye Mkosamali aliomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, akitaka waliotuhumiwa watajwe ili wafahamike vizuri.

Zambi na Badwel ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa pamoja na Kafulila chini ya Mwenyekiti wao, Mrema.

"... Mwenyekiti, tumesikia tuhuma zilizotolewa hapa kuhusu rushwa, naomba mwongozo wako maana hapa tumesikia juu juu tu...,"alisema Mkosamali. Mwenyekiti wa Bunge, Simbachawene akijibu hoja hiyo alisema atatoa mwongozo wake baadaye, katika muda ambao ataona unafaa.

Kauli ya Naibu Spika

Naibu Spika, Job Ndugai alisema taarifa ya tuhuma za rushwa kwa wabunge ziliwahi kutolewa katika kikao cha Kamati ya Uongozi na Mrema, ijapokuwa majina ya watuhumiwa na mlalamikaji hayakutajwa.

"Kama Mheshimiwa Spika aliandikiwa barua mimi sifahamu, lakini nakumbuka katika moja ya vikao vya kamati ya uongozi suala hili liliwahi kuelezwa na nadhani tukio hili linadaiwa kwamba lilitokea huko mkoani Tanga, kama sikosei na ilikuwa ni kama taarifa tu,"alisema Ndugai na kuongeza:

"Lakini Mrema alisema mlalamikaji alikuwa na ushahidi na akasema alikuwa na mpango wa kuwasiliana na Takukuru (Taasisi na Kuzuia na Kupambana na Rushwa) na sisi kwa kuona limekaa hivyo hatukuwa na mjadala tukadhani huko ndiko mahala pake."

Ndugai alisema msingi wa suala hilo kuwasilishwa kama taarifa katika kikao hicho, ulikuwa kutoa tahadhari kwa Kamati za Bunge zinazoshughulikia Hesabu za Serikali, kujihadhari ili zisitumbukie katika kashfa za rushwa na kuharibu sifa nzima ya Bunge.

Awali, Kafulila alisema tayari taarifa za tuhuma hizo za rushwa zilikuwa zimefikishwa kwa Spika kwa maandishi pamoja na Mrema kwa ajili ya hatua zaidi.

Kadhalika, Mbunge huyo alisema taarifa hizo zilikuwa zimekwishawafikia viongozi wa juu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kwamba aliwahi kukutana na Spika kuhusu suala hilo ijapokuwa hakukuwa na hatua zozote ambazo zilichukuliwa.

Zambi, Badwel wazungumza

Akizungumza katika moja ya Ofisi za Bunge kuhusu tuhuma hizo, Zambia alisema taarifa hizo zimemsikitisha na kwamba anasubiri hatua za kibunge kwa kuzingatia kanuni ya 63.

"Nimemsikia akizungumza, taarifa hizo zimenisikitisha sana kwani kama alivyosema kwamba alitukamata, alikuwa anasubiri nini kutotoa taarifa wakati wote, au alikuwa akisubiri kutuumbua? Mimi nasubiri hatua za kibunge na nadhani kabla ya kufikia mwisho wa kikao cha leo, Mwenyekiti atatoa mwongozo,"alisema Zambi.

Kwa upande wake, Badwel alisema hakumbuki kuwapo kwa tukio la namna hiyo na kwamba wakiwa mkoani Tanga walizichukulia hatua halmashauri zote nne ambazo walizikagua na kukuta udhaifu katika usimamizi wa fedha.

"Kwani yeye alitukamata ni polisi au Takukuru? Kwanza Tanga hivi vyote havipo? Sisi tumefanya kazi nzuri sana kama mnavyojua Kamati ya LAAC imefanya kazi nzuri tu, sasa huyo anatafuta umaarufu tu na kauli zake zinalenga kutuchafua,"alisema Badwel kwa simu.

Malumbano bungeni

Wakati wa kuchangia hoja kuhusu Mpango wa Maendeleo, kulizuka mvutano juu ya nani mwenye haki nao na hatua hiyo ilikuja baada ya Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambari Nyangwine kuliekeza Bunge kuwa mpango ulikuwa umewasilishwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Kauli hiyo ilimlazimisha Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee kusimama na kutaka mbunge huyo kufuta kauli yake, lakini Nyangwine alisisitiza kuwa hatafuta kwa sababu ni kweli kwamba mpango ulikuwa umewasilishwa na Serikali ya CCM.

Msimamo huo ulimlazimisha Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohmed, kusimama na kulieleza Bunge kuwa kauli hizo zilikuwa hazina maana na kwamba zilikuwa za kupoteza muda wa Bunge kujadili mambo yenye msingi kwa taifa.

Hamad alisema Mbunge wa Tarime hakupaswa kusema kuwa mpango huo umewasilishwa na Serikali ya CCM kwa sababu ni wa taifa.Baadaye, Mwenyekiti Simbachamwene alisimama na kumtetea Nyangwine kuwa alikuwa sahihi kuwa mpango ulikuwa umewasilishwa na Serikali ya CCM.
 
Safi sana Vijana wapiganaji hao CCM wamezoea kulala lala tu. inasikitisha bado wa fikira za miaka arobaini na saba
sasa ndio wanafundishwa namna bunge linataka kuwa
 

Kafulila "Mheshimiwa Mwenyekiti kwa wakati wa sasa ni vigumu kusimamia matumizi kwani mfumo wetu wa uongozi unaruhusu ufisadi, wapo viongozi, mawaziri, wabunge wanaomba rushwa...." alisema Kafulila na kuamsha zogo ambalo liliambatana na sauti zisizo rasmi katika ukumbi wa Bunge zikiuliza ".....wapo humu humu?" Kafulila alijibu "Ndiyo..."

Sauti moja ilisema wataje, hapo ndipo aliposema "....Wapo kina Zambi, Badwel, nimewakamata na nimechukua hatua, hatuwezi kuendelea namna hii," kisha akaketi.

Baada ya dakika chache tangu alipoketi, Kafulila alionekana akiteta jambo na Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali na Augustine Mrema wa Vunjo na baadaye Mkosamali aliomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, akitaka waliotuhumiwa watajwe ili wafahamike vizuri.

Zambi na Badwel ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa pamoja na Kafulila chini ya Mwenyekiti wao, Mrema.

"... Mwenyekiti, tumesikia tuhuma zilizotolewa hapa kuhusu rushwa, naomba mwongozo wako maana hapa tumesikia juu juu tu...,"alisema Mkosamali. Mwenyekiti wa Bunge, Simbachawene akijibu hoja hiyo alisema atatoa mwongozo wake baadaye, katika muda ambao ataona unafaa.

Kauli ya Naibu Spika

Naibu Spika, Job Ndugai alisema taarifa ya tuhuma za rushwa kwa wabunge ziliwahi kutolewa katika kikao cha Kamati ya Uongozi na Mrema, ijapokuwa majina ya watuhumiwa na mlalamikaji hayakutajwa.

"Kama Mheshimiwa Spika aliandikiwa barua mimi sifahamu, lakini nakumbuka katika moja ya vikao vya kamati ya uongozi suala hili liliwahi kuelezwa na nadhani tukio hili linadaiwa kwamba lilitokea huko mkoani Tanga, kama sikosei na ilikuwa ni kama taarifa tu,"alisema Ndugai na kuongeza:

"Lakini Mrema alisema mlalamikaji alikuwa na ushahidi na akasema alikuwa na mpango wa kuwasiliana na Takukuru (Taasisi na Kuzuia na Kupambana na Rushwa) na sisi kwa kuona limekaa hivyo hatukuwa na mjadala tukadhani huko ndiko mahala pake."

Ndugai alisema msingi wa suala hilo kuwasilishwa kama taarifa katika kikao hicho, ulikuwa kutoa tahadhari kwa Kamati za Bunge zinazoshughulikia Hesabu za Serikali, kujihadhari ili zisitumbukie katika kashfa za rushwa na kuharibu sifa nzima ya Bunge.

Awali, Kafulila alisema tayari taarifa za tuhuma hizo za rushwa zilikuwa zimefikishwa kwa Spika kwa maandishi pamoja na Mrema kwa ajili ya hatua zaidi.

Kadhalika, Mbunge huyo alisema taarifa hizo zilikuwa zimekwishawafikia viongozi wa juu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kwamba aliwahi kukutana na Spika kuhusu suala hilo ijapokuwa hakukuwa na hatua zozote ambazo zilichukuliwa.

Zambi, Badwel wazungumza

Akizungumza katika moja ya Ofisi za Bunge kuhusu tuhuma hizo, Zambia alisema taarifa hizo zimemsikitisha na kwamba anasubiri hatua za kibunge kwa kuzingatia kanuni ya 63.

"Nimemsikia akizungumza, taarifa hizo zimenisikitisha sana kwani kama alivyosema kwamba alitukamata, alikuwa anasubiri nini kutotoa taarifa wakati wote, au alikuwa akisubiri kutuumbua? Mimi nasubiri hatua za kibunge na nadhani kabla ya kufikia mwisho wa kikao cha leo, Mwenyekiti atatoa mwongozo,"alisema Zambi.

Kwa upande wake, Badwel alisema hakumbuki kuwapo kwa tukio la namna hiyo na kwamba wakiwa mkoani Tanga walizichukulia hatua halmashauri zote nne ambazo walizikagua na kukuta udhaifu katika usimamizi wa fedha.

"Kwani yeye alitukamata ni polisi au Takukuru? Kwanza Tanga hivi vyote havipo? Sisi tumefanya kazi nzuri sana kama mnavyojua Kamati ya LAAC imefanya kazi nzuri tu, sasa huyo anatafuta umaarufu tu na kauli zake zinalenga kutuchafua,"alisema Badwel kwa simu.
 
Mbona hajasema ni rushwa ipi iliyoombwa? pengine waliomba chai Kafulia akaona enheee ndio hapa hapa! Hana mpango huyo.
 
Back
Top Bottom