BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

sourse plz

MBUNGE wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila jana jioni alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kuwataja wabunge wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuomba rushwa katika halmashauri ambayo hakuitaja.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano, Kafulila aliwataja Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel wote wa CCM akidai kwamba aliwakamata wakiomba rushwa kwa viongozi wa halmashauri.

Wakati akitaja majina hayo, Kafulila nusra aingie katika mgogoro na Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene ambaye alikuwa akimwamuru kukaa chini kutokana na muda wake wa kuchangia kumalizika. Kafulila alikuwa akiendelea kuzungumza bila kujali kengele ya pili iliyopigwa kuashiria kwamba muda wake wa kuzungumza ulikuwa umekwisha.

"Mheshimiwa Mwenyekiti kwa wakati wa sasa ni vigumu kusimamia matumizi kwani mfumo wetu wa uongozi unaruhusu ufisadi, wapo viongozi, mawaziri, wabunge wanaomba rushwa...." alisema Kafulila na kuamsha zogo ambalo liliambatana na sauti zisizo rasmi katika ukumbi wa Bunge zikiuliza ".....wapo humu humu?" Kafulila alijibu "Ndiyo..."

Sauti moja ilisema wataje, hapo ndipo aliposema "....Wapo kina Zambi, Badwel, nimewakamata na nimechukua hatua, hatuwezi kuendelea namna hii," kisha akaketi.

Baada ya dakika chache tangu alipoketi, Kafulila alionekana akiteta jambo na Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali na Augustine Mrema wa Vunjo na baadaye Mkosamali aliomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge, akitaka waliotuhumiwa watajwe ili wafahamike vizuri.

Zambi na Badwel ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa pamoja na Kafulila chini ya Mwenyekiti wao, Mrema.

"... Mwenyekiti, tumesikia tuhuma zilizotolewa hapa kuhusu rushwa, naomba mwongozo wako maana hapa tumesikia juu juu tu...,"alisema Mkosamali. Mwenyekiti wa Bunge, Simbachawene akijibu hoja hiyo alisema atatoa mwongozo wake baadaye, katika muda ambao ataona unafaa.

Kauli ya Naibu Spika

Naibu Spika, Job Ndugai alisema taarifa ya tuhuma za rushwa kwa wabunge ziliwahi kutolewa katika kikao cha Kamati ya Uongozi na Mrema, ijapokuwa majina ya watuhumiwa na mlalamikaji hayakutajwa.

"Kama Mheshimiwa Spika aliandikiwa barua mimi sifahamu, lakini nakumbuka katika moja ya vikao vya kamati ya uongozi suala hili liliwahi kuelezwa na nadhani tukio hili linadaiwa kwamba lilitokea huko mkoani Tanga, kama sikosei na ilikuwa ni kama taarifa tu,"alisema Ndugai na kuongeza:

"Lakini Mrema alisema mlalamikaji alikuwa na ushahidi na akasema alikuwa na mpango wa kuwasiliana na Takukuru (Taasisi na Kuzuia na Kupambana na Rushwa) na sisi kwa kuona limekaa hivyo hatukuwa na mjadala tukadhani huko ndiko mahala pake."

Ndugai alisema msingi wa suala hilo kuwasilishwa kama taarifa katika kikao hicho, ulikuwa kutoa tahadhari kwa Kamati za Bunge zinazoshughulikia Hesabu za Serikali, kujihadhari ili zisitumbukie katika kashfa za rushwa na kuharibu sifa nzima ya Bunge.

Awali, Kafulila alisema tayari taarifa za tuhuma hizo za rushwa zilikuwa zimefikishwa kwa Spika kwa maandishi pamoja na Mrema kwa ajili ya hatua zaidi.

Kadhalika, Mbunge huyo alisema taarifa hizo zilikuwa zimekwishawafikia viongozi wa juu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na kwamba aliwahi kukutana na Spika kuhusu suala hilo ijapokuwa hakukuwa na hatua zozote ambazo zilichukuliwa.

Zambi, Badwel wazungumza

Akizungumza katika moja ya Ofisi za Bunge kuhusu tuhuma hizo, Zambia alisema taarifa hizo zimemsikitisha na kwamba anasubiri hatua za kibunge kwa kuzingatia kanuni ya 63.

"Nimemsikia akizungumza, taarifa hizo zimenisikitisha sana kwani kama alivyosema kwamba alitukamata, alikuwa anasubiri nini kutotoa taarifa wakati wote, au alikuwa akisubiri kutuumbua? Mimi nasubiri hatua za kibunge na nadhani kabla ya kufikia mwisho wa kikao cha leo, Mwenyekiti atatoa mwongozo,"alisema Zambi.

Kwa upande wake, Badwel alisema hakumbuki kuwapo kwa tukio la namna hiyo na kwamba wakiwa mkoani Tanga walizichukulia hatua halmashauri zote nne ambazo walizikagua na kukuta udhaifu katika usimamizi wa fedha.

"Kwani yeye alitukamata ni polisi au Takukuru? Kwanza Tanga hivi vyote havipo? Sisi tumefanya kazi nzuri sana kama mnavyojua Kamati ya LAAC imefanya kazi nzuri tu, sasa huyo anatafuta umaarufu tu na kauli zake zinalenga kutuchafua,"alisema Badwel kwa simu.
 
Hili la wanasiasa wetu kuzitafuna taasisi za UMMA tumelisema sana humu. Kiboko ya wote ni Mawaziri na taasisi za umma zilizo chini ya wizara zao.
 
nakubaliana na wewe but we fed up abt faiza foxy still mods defend her. anafanya atakalo hapa jamvini kama kwel mods wanatenda hak why do not take action against her?.
kha...!!una maana anaegemea sana sisiem afu mamod wanamwangalia tu bila kumban ama?We jamaa ni very hopeless .unashitaki kama mtoto wa miaka tano BE YOUR AGE
 
Niwewe au mwingine Mr. Mak? Umekuja kivyengine mnoo! Big up...albeit for now only
Tuhuma inaonekana ni za kweli,kwani jinsi Zambi alivokuwa akiongea kwa woga na kujihami kwa kumshambulia, na yule wa Bahi ndio hakuongea kabisa. Halafu ukiangalia interval ya alipoongea Kafulila na Zambi unaweza ona ukweli kuwa Zambi ni mtuhumiwa. Nasikitika kuwa bongo vyombo vyetu vya usala bado vipo kisiasa, kwani ilikuwa inatakiwa leo akina Zambi wawe wamekamatwa kwa tuhuma, simuliona alivotuhumiwa yule wa IMF alichofanyiwa. hapa kuna haja ya kuwawajibisha
 
Mr Mak leo ni birthday yako nini? Kale kalaik sikaoni hapa nilitaka nikugongee aisee!
Na wengine hebu igeni mfano basi. Taifa kwanza!
Kuna msemo wa kiarabu nakuandikia kwa kiswahili unasema:
KULU HAKI WALAU KANA MURAA=ONGEA HAKI(UKWELI) HATA KAMA INAUMA(INAKERA).
kwanini nimesema hivi, Faiza umechemesha kusupport ududu huo wa tuhuma za rushwa. Ukiijifanya sana mlevi wa siasa utajikuta unaunga mkono hata vitu vya kipumbavu. Rushwa ni rushwa tu, acha chai hata kama huyo mbunge angekuja kwako akakuomba akunanihii wewe bado ni rushwa inatakiwa kwa pamoja tuipinge kwa nguvu zote.
Ivi wewe kwa uelewa wako Mtu anaweza simama kwenye halaiki na kumtuhumu mtu wazi wazi bila kuwa na data za ukweli? mbona mheshimiwa zambi hajasema atamshitaki mahakamani kwa kudhalilishwa? kwanza alichelewa sana kuomba hata kale ka mwongozo, pia alifanya kujihami tu na kwa tuhuma hizo hata yule mwenzake wa bahi hakunyanyua hata mdomo.Inatakiwa Ujinga kama huu tusiuunge mkono.
 
Mbona hajasema ni rushwa ipi iliyoombwa? pengine waliomba chai Kafulia akaona enheee ndio hapa hapa! Hana mpango huyo.

stoning-in-somalia.jpg
 
Zamani zikitolewa tuhuma utasikia *THIBITISHA* siku hizi yanadhibitishwa kwa kutajwa watu kwa majina utasikia *ANAJITAFUTIA UMAARUFU* ndivyo wanavyosema waliotajwa. iko kazi lakini iko siku tutafika tu
 
Duh.Hivi kuna haja gani kuchangia kitu kama haujajiandaa?Simple minded people critize even themselves
 
Hongera na ni ujasiri wa hali ya juu wa kizazi hiki,mengi bado yaja.
 
Source ni mjadala wa Bunge jana jioni wakati Kafulila alipodai kwamba aliwakamata wabunge wa Magamba (Zambi, Mkosamali) live wakitoa rushwa na akawachukulia hatua!

Hapo kwenye nyekundu Buchanan angalia utapelekwa mahakamani.Aliowataja ni hawa hapa;
Godfrey Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel wote wa CCM.
Na hajasema walikua wanatoa bali wanaomba.Please be carefully.
 
Source ni mjadala wa Bunge jana jioni wakati Kafulila alipodai kwamba aliwakamata wabunge wa Magamba (Zambi, Mkosamali) live wakitoa rushwa na akawachukulia hatua!
Sahihisho kidogo mkuu katika red, wakiomba(kulazimisha) rushwa.
 
Mr Mak leo ni birthday yako nini? Kale kalaik sikaoni hapa nilitaka nikugongee aisee!
Na wengine hebu igeni mfano basi. Taifa kwanza!

Duh! Hiyo avatar yako nimeipenda, nakumbuka ni kwenye kikao hicho ndipo James Whistler alidedishwa na Wyatt (avatar ya Balantanda). Natamani tungekuwa na snipers kama Balantanda/Wyatt wa kuwa anadungua mmoja mmoja:-
Anaanza na JK->Pinda->Spika->Nape->Mkama->Rachel->Ridh1 na wengine wote wajinga wajinga.

Vipi Chadema wakiamua Kafulila arudi kundini, naona vitu vyake si mchezo; kijana analimiss kundi na lenyewe linammiss kinoma. Mi natamani warudiane.
 
Duh.Hivi kuna haja gani kuchangia kitu kama haujajiandaa?Simple minded people critize even themselves

Huyu alikuwa anafanya timing, aruhusiwe kumwaga upupu sio kuripuka tu. Na jamaa wamempotezea, lakini najua jamaa wataumbuka tu plus na hao wanaowalinda kwa sababu kila mtu atataka kujua kunani humo.

Katumia ule mfumo wa watoto akitaka kusema kitu anaanza kama hataki vile, utasikie "Niseme? Niseme kwamba ulichukua rushwa nisiseme? Ntasema mimi?" Utasikia mama anaulizwa, "Mama nikwambie flani alivyochukua rushwa nisikwambie?". Hapo mama akisema niambie kila kitu kinamwagwa hapo. Kafulila anasubiri mama aseme sema (na kwa ninavyojua mama atamwambia njoo uniambilie huku ili asimuumbue mwenzake mbele yetu, lakini na si tutajua tu kwa sababu baadaye atakuja kutuambia hata sisi).

Big Up Kafulila.
 
Tumesikia habari za kusikitisha na za aibu sana kuwa kuna wabunge walikamatwa wakiomba rushwa!!

Bila kujali ni wa chama gani, namuomba spika Makinda ahakikishe kuwa pamoja na uwezekano wa suala hilo kushugulikiwa na vyombo vya serikali, but bunge kama bunge litoe adhabu kali (baada ya kuthibitisha) kwa wabunge hao, ili kurudisha imani ya watanzania kwa bunge hilo...

My friend,

This is NOT news. Everybody knows the goings in TZ. Check this:
1. Kila anayefungua mkutano, warsha, seminar, etc lazima awe na bahasha japo hii ni kazi yao. Kiasi cha pesa kinaongezeka cheo kinavyokuwa kikubwa.
2. Makatibu wakuu na wakurugenzi lazima wawe kwenye orodha ya wahudhuriaji wa seminar, warsha, vikao vyote wizarani mwao. Hivyo wanakusanya sitting allowances hata 6 kwa siku. Sasa wewe mtayarishaji ujifanye mjanja usiweke jina lake, utaipata.
3. Makatibu wakuu na wengineo wakubwa wakienda nje ya nchi huwa pia wanavuta mshiko wa kusafiri ndani ya nchi.
4. Kwenye mashirika ya umma hali sio kama wizarani lakini pia safari za nje ndio mtindo. Wengine wamepewa majina ya explorers kama Vasco da gama, Captain Cook etc.
5. ......Madudu mengine machafu mengi tu. Huyo CAG na watu wake wanayajua hayo lakini culture ya KULINDANA imetufikisha hapa.
 
na mwaka huu lazima tutaona yaliyotokea kule kwenye bunge la mzee jomo kenyatta, paa, paa, paa,
 
Tatizo takurukuru wamewekwa na maganga kikubwa kwenye katiba mpya tutengeze chombo ambacho cha kupambana na rushwa kipo huru kama walivyofanya Kenya lasivyo tutabaki na makapi ya magamba.
 
Back
Top Bottom