BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

Tumesikia habari za kusikitisha na za aibu sana kuwa kuna wabunge walikamatwa wakiomba rushwa!!

Bila kujali ni wa chama gani, namuomba spika Makinda ahakikishe kuwa pamoja na uwezekano wa suala hilo kushugulikiwa na vyombo vya serikali, but bunge kama bunge litoe adhabu kali (baada ya kuthibitisha) kwa wabunge hao, ili kurudisha imani ya watanzania kwa bunge hilo...

hivi bado una imani na bunge lenye wabunge 80% wa ccm wanaoshabikia kila uozo?
 
Tuhuma inaonekana ni za kweli,kwani jinsi Zambi alivokuwa akiongea kwa woga na kujihami kwa kumshambulia, na yule wa Bahi ndio hakuongea kabisa. Halafu ukiangalia interval ya alipoongea Kafulila na Zambi unaweza ona ukweli kuwa Zambi ni mtuhumiwa. Nasikitika kuwa bongo vyombo vyetu vya usala bado vipo kisiasa, kwani ilikuwa inatakiwa leo akina Zambi wawe wamekamatwa kwa tuhuma, simuliona alivotuhumiwa yule wa IMF alichofanyiwa. hapa kuna haja ya kuwawajibisha


Ka-Zambi kanaonekana kweli kala rushwa kazuri tu,lakini Kafulila nae atakuwa na matatizo mbona kabana na hii issue muda mrefu wakati ni jinai.Hawa wote wanapaswa kuisaidia dola ili tupate ukweli,inawezekana Zambi alihama na fungu lote bila kutema kwa Kafulila,sasa deal imesanuka.
 
Walitaka kuyaficha majina ya wabunge wala rushwa bahati nzuri kafulila katufahamisha ni akina nani. Hapando naanza kuamini kwamba rushwa na CCM damu damu, kama wanaweza wajivue gamba la akina Zambi tuone
 
Imeandikwa na Halima Mlacha; Tarehe: 14th June 2011


MBUNGE wa Kigoma Kusini (NCCRMageuzi), David Kafulila ametoa tuhuma nzito za kuomba rushwa kwa baadhi ya wabunge na mawaziri.

Kafulila alirusha tuhuma hizo na kuwataja wabunge wawili wakati akichangia Mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2011/2016 ambapo alihimiza suala utawala bora na usimamizi wa matumizi ya bajeti.

“Kuna tatizo kubwa sana la mfumo wa kifisadi, kuna mawaziri na wabunge wanaomba rushwa na wako humu ndani nchi haiwezi kuendelea kwa mtindo huu. Kwa sasa bajeti inapangwa lakini utekelezaji wake unasuasua, mimi naomba mheshimiwa Mwenyekiti
iundwe Kamati ya Bunge itakayosimamia bajeti,” alisema Kafulila.

Hata hivyo kutokana na kupitiliza muda wake wakati akijieleza zaidi alitakiwa na George Simbachawene Mbunge wa Kibakwe (CCM) ambaye ni Mwenyekiti wa Bunge kukaa chini kwa kuwa muda wake umepita.

Kufuatia kauli hiyo baadhi ya wabunge walisikika kwa mbali wakimtaka awataje hao mawaziri na wabunge wanaoomba rushwa ambapo aliwataja ingawa hawakusikika
vizuri kutokana na kuchanganyika kwa kelele za kumtaka Mbunge huyo athibitishe huku wengine wakimtaka akae chini kwa kuwa muda wake umeisha wa kuzungumza.

Mwongozo wa Spika kutoka kwa mbunge wa Muhambwa, Felix Mkosamali (NCCR)wa kumtaka Kafulila awataje wanaokula rushwa ulikubaliwa na Simbachewene ambaye alimwambia utajibiwa katika vikao husika katika muda utakaofaa.

Awali wakati akichangia mpango huo alisisitiza juu ya kilimo kupewa kipaumbele kwa kuhakikisha kuwa kinakua kwa asilimia 10 na si sita zilizowekwa kwenye mpango huo.

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF), alisema kilio cha kuwa na Tume ya
Mipango ni cha Muda mrefu na sasa watu wamefarijika sasa tume hiyo imeundwa na mipango itaratibiwa vizuri.
 
Kamati ya Nishati na Madini yapokea rushwa
Wajumbe wengi wa kamati ya Nishati na Madini wamedaiwa kupewa rushwa ili kupitisha bajeti ya wizara wanayoisimamia.
Chanzo ndani ya kikao cha kamati hiyo kilichoketi leo bungeni Dodoma kimebainisha kuwa tuhuma hiyo imetolewa na Mbunge wa Korogwe ambaye hakuwepo wakati wa vikao vya kamati bajeti inapitishwa.
Mbunge huyo amesema kwamba baada ya kurejea amepata tuhuma toka wizarani kuwa baadhi ya wabunge walipokea rushwa.
Spika wa Bunge Anna Makinda ambaye alihudhuria kikao hicho alisema anafahamu jambo hilo na analifuatilia.
Mbunge huyo ameeleza kuwa chanzo cha taarifa za Wizarani kuvuja ni kikao kilichoitishwa baada ya Mbunge wa Muleba Kaskazini Charles Mwijage na Mbunge wa Ubungo John Mnyika kukataa kupokea bahasha zenye rushwa hiyo hali ambayo iliwashtua watendaji wa Wizara na kulazimika kuitisha kikao.
Katika kikao hicho kilichofanyika Dar es salaam wajumbe wengi walitaka kupitisha bajeti hiyo kufuatia rushwa iliyotolewa hata hivyo Mnyika ambaye ni msemaji wa kambi rasmi ya upinzani nishati na madini alikataa bajeti hiyo isipite mpaka kwanza serikali ikubali kufanya marekebisho ya kupunguza posho, kuongeza miradi mipya ya umeme, mfuko wa wachimbaji wadogo na ujenzi katika Chuo cha Madini.
Kufuatia hali hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati January Makamba aliwaomba wajumbe kupitisha bajeti hiyo pamoja na marekebisho ikiwemo kuhusu kubadili jina la jengo la makao makuu ya Wizara linalokusudiwa kujengwa Dar es salaam ili kuendana na dhamira ya CCM ya kuhamishia makao makuu Dodoma.











 
Rushwa ni sawa na TB Tanzania ama ugonjwa wa Kansa ya Damu tiba mpaka kifo cha mtu. Tutampata huyu wa kututoa hii damu na kuiingiza mpya isiyo na mdudu huyu. Shame kwa bunge kwani kamati zinafanya kazi kwa niaba ya bunge, kamati ikishindwa kufanya kazi inamaanisha bunge zima ni ovu.
 
Kamanda mbowe anamwaga vitu kuhusu mpango wa maendeleo, anashaur kusomeshwa kwa vijana nje ya nchi ili wapate jifunze tech za nchi zilizotuzidi kiuchumi akitumia falsafa ya kichina kwamba km huwezi vumbua basi iga (kucopy).
 
Kuwajibisha viongozi wa ngaz za chini kuweza kutengeneza ajira na si kutegemea serikal kuu, anasema tunapaswa kuacha consumption economy uchum unadepend katka kutumia zaidi ya kuzalisha.
 
Anaanza mnyika! Kwa kutaja kanuni za bunge km kujadil mipango ya muda mfup na mrefu ktk masuala ya maendeleo.
 
Anaongelea foleni za dar, na kushauri utengenezaj wa barabara zaGoba mpk mbezi mpk kinyerezi ili kuepuka foleni pindi ujenzi wa mabasi yaendao kwa kasi kuanza pembezon mwa morogoro road.
 
TBC wanakata kata, m nahisi ni janja ya kutoa wap attention ya kufuatilia vitu vya msingizi.
 
Ndiyo maana JK anadai kuwa demokrasia imekuwa; Hamad anatumia mdomo wake hivyo kwa sababu anao. Tungekuwa tunalipia kila tunachoongea basi Hamad angenyamaza na siasa zake za UNAFIKI.Hivi huyu mbunge wa CUF Hamad Rashid anajisikiaje kudanganya umma kuwa maandamano yanafanyika usiku!! Waandishi wa habari nao hata hawawezi kumbana ataje ni nchi gani maandamano yanafanyika usiku. Pale Tahirir Sq. maandamano yalianza asubuhi na wakakesha na wakendelea kukaa pale hadi Mubarak alipoachia ngazi. Sasa yeye Hamad hasije akajichanganya hapo.

Na kama Mizengo Pinda hasingempigia Prof. Lipumba simu kumuomba kusimamisha maandamano ya CUF wiki iliyopita, leo ingekuwa ni habari nyingine. Sasa ni wapi ambapo CUF wanadai wanachukia maandamano wakati hata Naibu Katibu Mkuu wao Mtatiro aliwahi kuongoza hayo maandamano hadi Wizara ya Sheria na Katiba? UNAFIKI TU.
 
Back
Top Bottom