BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

BUNGENI: Mjadala wa mpango wa maendeleo wa taifa

Anaunga mkono mpango huo kwa kuwa ni wa manufaa kwa wananchi wake wa Vunjo

anayataja maeneo ya uboreshaji wa miundo mbinu hasa barabara na Kilimo ina maana kubwa kwa watu wa Vunjo, pia bei ya mazo ni muhimu kwa wakulima wake wa kahawa ambao ana hakika watapata 8000 kwa kilogram ya kahawa

anatoa wito wa kupewa miche bora ya kahawa itakayotoa mavuno ya kutosha kuwanufaisha wakulima wa Vunjo

....anapigiwa makofi flani hivi..sijui ya nini hasa...
 
Anamalizia

anaomba suala la amani na usalama liimarishwe ili kuwezesha mpango huo kutekelezeka kwa ufanisi
 
huyu mzee hana wa kiraracha kwisha kazi yake!
 
anaomba demokrasia isitumike vibaya kwa kumpiga ngwara rais aliyeko madarakani...Full kujipendekeza
 
Ameanza porojo zake za kuponda wenzie. Eti yeye alikuwa maarufu lakini alikubali kushindwa. Anasema tusitumie demokrasia kama kigezo cha kumpiga ngwara Rais aliyepo madarakani
 
VUVUZELA LA CCM,Mzee wa kiraracha anamtetea kikwete
 
Badala ya kuchangia hoja za mpango wa maendeleo anaanza kuzungumzia jinsi alivyoshindwa urais mwaka 1995.
 
Mrema anaharibu, anasema maandamano yanawafanya watu washinde kulima!
 
Msigwa kasimama na kuomba mwongozo kwamba Mrema katoka nje ya mada. Hili bunge angekuwapo Makinda lingekuwa limechafuka vibaya. Mwenyekiti naye kachemka eti hakuna mtu yeyote aliyetajwa wakati Mrema kamtaja Dr. Slaa
 
anasisitizia kuwa kaona alisemea hilo, anahamia kwenye maandamao na kaamua kumtaja PhD live inaonekana hakubaliani na maandamano ati anasema '' maandamano ya kila siku yanachosha na hayafai''

kapigwa muongozo

anaambiwa kama alipigwa stop mchangiaji mwingine kwa nini huyu aendelee, Mchungaji kamkaba koo

mwenyekiti kaibuka na kusema miongozo iombwe kwa kufuata taratibu na si kwa bila kunukuu kanuni

anapigiwa makofi na kumruhusu kibandiko aendelee kutema moto

na sasa MIC yake inasikika vizuri baada ya kuonyesha anaponda CDM, Aisee hizi Mic zitakuwa zinaminywa

Kapigwa muongozo tena this Tym kamanda Lissu
 
Katoa kanuni ya 61 anapinga taarifa kuwa maandamano kuwa hayapo kila siku

WABUNGE WANAONGEA HOVYO HOVYO KAMA KWENYE KIJIWE CHA KAHAWA MIC ZIPO ON KIBAO

WAKATI SHERIA Inaruhusu Mic ya Speaker na Mchangiaji kuwa ON wakati wa kutoa hoja...AISEEE HIII SIJAIPENDA
 
CCM wanamchekea Mrema (kupe lao) wanajiona km vile wameshinda! Alafu kuna mwanamke anaropoka ropoka! Janualy makamba kaliona hilo!
 
Back
Top Bottom