Hii imefungua majadala mmoja mzuri saana, kuhusu mawaziri, kama kweli watu wana ushahidi wameenda/wanakwenda majimboni kutembelea wananchi wao na gari la uwaziri na huku anapewa kila mwezi pesa za lita 1000, nafikiri niwakati muafaka wafikishwe mahakamani kwa wizi wa mali ya umma. Hili watu walivalie njuka, hatuwezi kuacha mambo ya namna hiii.
Ila kwa wale wanaodai mbunge wa Dodoma kwa nini alipwe sitting allowance, hapa kuna utata je kwa nini umlipe mbunge za Zanzibar hela ya mafuta ya lita 1000, wakati jimbo lake ni dogo kuliko hata kata ya Kisutu? Na watu wake ni 200, yaani anaweza kuwatembelea kwa mguu na kuwamaliza wote siku moja. Jamani kuna mengi ya kurekebisha.