Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Haihitaji sayansi ya rocket kujua kuwa kinachopingwa na CHADEMA ni "mfumo" wa kulipa posho hizo. Kila mmoja anayepinga anaweza kuchukua hatua zake mwenyewe. Ndio Zitto akachukua hatua alizochukua. Hata huko CCM kuna watu waliwahi na wako na msimamo tofauti wa kichama. Walichukua hatua zao na kila mtu anajua walichokipata. Marehemu Kolimba ni mmoja wao.
Mfumo ni zaidi ya mtu mmoja mmoja!! Inatosha kabisa kupinga mfumo. Hata Mbowe akigomea hizi pesa, bila shaka utahoji kwanini Lissu na wengine hawajafanya hilo. Ili hao nao wasistahili, kubadilisha mfumo au sera hiyo ni muhimu zaidi kuliko Zitto na Makamba!
Mkuu naona kama unaenda kusiko. Kwanza ujue CDM ni CDM na inaipinga CCM hivyo basi si busara kujipima kwa CCM kwa makosa iliyofanya/waliyofanya na CDM iyafanye!
Hapo kwenye wekundu: Suala la posho siyo la mtu binafsi kwa CDM; hii ni sera ya CHAMA inatakiwa kuchukua hatua za kichama siyo kila mtu achukue hatua zake mwenyewe. Ingekuwa siyo sera ya Chama bali ni utashi wa mtu binafsi ingekuwa sawa kwa Zitto kufanya alichofanya. Lakini hapa tunaonelea sera na kiranja mkuu wa CDM ni Mbowe akiwa ndani ya Bunge na nje kama mwenyekiti hivyo basi alitakiwa kuonyesha mfano wa utekelezaji wa sera ya chama.