Bungeni: Mbowe aweka msimamo wa posho

Mbowe ni mzalendo halisi wa nchi yetu, nimemsikia akisema pia viongozi wa umma wanatumia nafasi zao vibaya, wanasafiri na Business class au special,tembelea land cruiser, kulipana posho za mamilioni, semina kila wakati kuhusu kuepuka ugonjwa wa ukimwi n.k...............
Wakati wafanyakazi wa chini ambao ndio wanafanya kazi kubwa serikalini hakuna cha posho, exta duty issue kupata labda mara moja baada ya miezi 5 au 6 tena hela ndogo tu! malimbikizo ya mishahara kibao, watu wanaishia kukopa tu, ikija salary slip unatamani mtu mwingine asiione maana salio ni sh. 5000 tu mikopo kibao, jamani!!!!!!!!Ahsante Mhe Zito Kabwe na Mhe Mbowe pengine Serikali itasikia kilio cha wengi kwa kupitia ninyi

Kwa kweli hata sisi ambao hatukusikiliza bunge hili imetukuna mpaka machozi hasa ukifikilia wananchi wengi wanavyoteseka huko vijijini . Miaka hamsini ya uhuru kuna watanzania wanabebwa kwenye machela . Kweli wabunge wetu hawana aibu wala chebe ya huruma. Ni juzi tu wametangaza shule ya msingi mjini Dodoma ambayo watoto   wanakaa chini. Lakini leo wabunge hawajafanya makusudi yoyote kuhakikisha kuwa swala hilo halipo hasa hapo Dodoma wanapotaka tupaheshimu sana. Mimi nasema hiyo ni sehemu ya walanguzi ni si watatezi wa wananchi waliowanyonge wa Tanzania.

AMANI HAIJI ILA KWA NCHA YA UPANGA>

naomba kamanda mbowe na jopo lako endeleeni na msimamo wenu wa kukata posho kwani watanzania tupo nyuma yenu na tunasubiri hatima ya jambo hilo. Haiewezekani wachache wakafaidi our national cake najua wao watashinda bungeni kwa wingi wao na makofi wanayopiga hata wakiwa usingizini hivyo naomba muheshimiwa mbowe, zitto. lema, mnyika, lissu, mdehe, vicent nyerere na majemedali wengine leteni hyo hoja kwa wananchi tuone nani zaidi kati ya walipa kodi na wapokeaji kodi

Hapa shujaa ni Zitto tu

Kweli mbowe kichwa nimeamini,hapo hata CCM hawana cha kuongea hapo kawaambia kweli.

Aliyekuwa waziri kwenye serikali ya Mkapa, Kilontsi Mpologomi, nimemkuta anakopa spare za kufunga kwenye gari lake pale mtaa wa Libya, baada ya kuondoka yule mwenye duka akawa analalamika sana kwamba huyu bwana anapenda kukopa halafu kulipa kwa mbinde, kumbe walishazoea vya dezo serikalini.Na hiyo ndio siri ya wastaafu wengi kufa mapema mara baada ya kustaafu. Haya maisha ya kitaa watuachie wenyewe wabishi wa mjini.
dah umenikumbusha aliyekua Mbunge wa zamani wa KIGOMA KASKAZINI (CCM) Bw KAHENA. Mara ya mwisho nilikutana nae Kigoma mjin anashangashangaa hakuna gari wala baiskeli.

kuhusu huyo mbunge ni kweli mimi mwenyewe nimesha mtengenezea computer zake kulipa shida ni kweli wanakuwa na hali mbaya sana hata ofisini kwake ukiingia jamani ukiambiwa alikuwa mbunge uwezi kuamini

... mura mura, sasa hii huoni ya nguoni kidogo tata!

kale kajamaa kanaitwa NAPE katapinga hili. MKAMA vipi jamani peoples power imemtuliza kwishneyyyyy. Mbowe heko saaana CCM mwisho wao umefika sasa!

kale kajamaa kanaitwa NAPE katapinga hili. MKAMA vipi jamani peoples power imemtuliza kwishneyyyyy. Mbowe heko saaana CCM mwisho wao umefika sasa!

Subiri tamko....

kweli ni shujaa wa kuwa kiherehere cha ubinafsi, bilashaka ndo kakuweka hapa JF umtetee, hongera kwa ajira uloipata.
Mkuu sikuelewi. Hivi ukitofautiana tu na mtu basi huyo mtu anakuwa ametumwa? Kwa hiyo na wewe kuna mtu amekutuma ili utofautiane na mimi? Acha kukimbilia kusema mtu ametumwa. Ina maana mimi siwezi kujituma mwenyewe? Ukiona hivyo ujue wewe ndio umetumwa kwa kuwa unawaza utumwa tuuuuu!

Dodoma jirani na Bunge chini kidogo kuna shule inaitwa MAKOLE PRIMARY hii shule pamoja kuwa mjini tena karibu na Bunge lakini wanafunzi wanakaa chini yaani hakuna madawati. Sipati picha huko vjjin pakoje?. Posho znaliwa hapahapa?!

Mkuu sikuelewi. Hivi ukitofautiana tu na mtu basi huyo mtu anakuwa ametumwa? Kwa hiyo na wewe kuna mtu amekutuma ili utofautiane na mimi? Acha kukimbilia kusema mtu ametumwa. Ina maana mimi siwezi kujituma mwenyewe? Ukiona hivyo ujue wewe ndio umetumwa kwa kuwa unawaza utumwa tuuuuu!

mkuu na mimi huwa sikuelewi unaposema shujaa ni ZITTO tu, kwani hoja kaianzisha yeye au chama? sina mawazo ya utumwa mkuu, post yako imenichefua, cdm km chama kina mashujaa.

mkuu na mimi huwa sikuelewi unaposema shujaa ni ZITTO tu, kwani hoja kaianzisha yeye au chama?

Ushujaa wake unakuja kwa kuwa hiyo ni hoja ya Chama na ni msimamo wa chama na Chama kimesema kinaziondoa kwenye budget yake kivuli lakini wabunge wengine wanaendelea kuzipokea yeye kazikataa na kakataa kusaini hata baada ya kutishiwa kuwa atafukuzwa. Mimi naona huyu ni shujaa kuliko wengine ambao wanasema tu kwenye majukwaa huku wanazinyakua hizo posho.

Hao nawaona ni wanafiki walikubaliana waseme kuwa msimamo wao ni kuziondoa kwenye budget kivuli wakijua kuwa hakuna wa kuwahoji kwa kuwa budget kivuli haitaonekana wapi inatekelezwa. Kumbe Zitto alikuwa anamaanisha wanalolisema na akaamua kufanya kwa vitendo, na sasa tunamuona amebaki peke yake kama dege lisiloliwa!! Upo kaka?

Posho Zitatugawa,

mkuu na mimi huwa sikuelewi unaposema shujaa ni ZITTO tu, kwani hoja kaianzisha yeye au chama? sina mawazo ya utumwa mkuu, post yako imenichefua, cdm km chama kina mashujaa.

Usichefuke kwa hoja mkuu. Tupingane bila kupigana ama kuchefuana. Kwa hiyo Zitto si miongoni mwao?

Ushujaa wake unakuja kwa kuwa hiyo ni hoja ya Chama na ni msimamo wa chama na Chama kimesema kinaziondoa kwenye budget yake kivuli lakini wabunge wengine wanaendelea kuzipokea yeye kazikataa na kakataa kusaini hata baada ya kutishiwa kuwa atafukuzwa.

Mimi naona huyu ni shujaa kuliko wengine ambao wanasema tu kwenye majukwaa huku wanazinyakua hizo posho. Hao nawaona ni wanafiki walikubaliana waseme kuwa msimamo wao ni kuziondoa kwenye budget kivuli wakijua kuwa hakuna wa kuwahoji kwa kuwa budget kivuli haitaonekana wapi inatekelezwa.

Kumbe Zitto alikuwa anamaanisha wanalolisema na akaamua kufanya kwa vitendo, na sasa tunamuona amebaki peke yake kama dege lisiloliwa!! Upo kaka?

Posho Zitatugawa,

nimekuelewa kidogo, lakini mkuu huoni kuwa wameamua kutumia busara ili wasifukuzwe bungeni? endapo watafukuzwa wote magamba watapitisha hadi matapishi ya ikulu ndogo.

Halafu pia napata mashaka ni wapi wamesaini kuchukua hizo posho? mbona nimeona sehemu wamesaini mahudhurio tu. Anyway tuachane na hizo ishu, tushikamane pamoja tupambane na utawala huu wa kisanii.

Back
Top Bottom