Nakubalina na mpango huu wa kuwasaidia wagonjwa kwa wakati huu wa dharura. Shida yangu kubwa ni ufanisi wa hao madaktari wanaoazimwa.
Nijuavyo mimi hao madaktari wanaoazimwa yaani waliostafu, walioko wizarani na pengine na akina mbunge Kigangwara na wengineo kama Dr. Husein Mwinyi kama hawa-practice kwa muda fulani labda zaidi ya miaka 3 na kuendelea mambo haya ya ujuzi yanaanza kupotea/kusahaulika kichwani. Yes unakuwa bado unazo ideas za skills na knowledge but to be effective unahitaji kujikumbusha tena (refreshed).
Sasa swali langu ni Je hao wanaoletwa wastaafu na wa kutoka wizarani (hasa hawa - maana waliachaga siku nyingi ku-practice; kazi wanayo fanya ni ya kisera zaidi - paper works kuliko profession yao - dawa, muscles, diagnosis, nerves, ligaments, tendons and their specific names, surgery, n.k) watapewa muda wa kuwa refresh? Najua ni wataalam kabisa but to my opinion wanahitaji kujikumbusha tena!!!