Bungeni Live: June 28, 2012

Wakuu, kama ikiwapendeza, unganisheni thread za Mh. Pinda kuhusu mgomo wa Drs na maswali ya bungeni. ziko nyingi mno hata kuchangia inakuwa kazi.

Baada ya hapo mnaweza hata mkaifuta na hii ya kwangu
Asanteni
 
Kutokana na kutekwa kwa watalii na kuuwawa, kukuta wahamiaji zaidi ya arobaini wakiwa wamekufa vilevile kutekwa kwa dr.Olimboka, kumemfanya Rais wa nchi kurudi nchini kujadili hili swala na usalama wa taifa. Hayo yamesemwa na mh. waziri Mkuu M.K.Pinda Bungeni wakati akijibu maswali ya papo kwa papo leo Bungeni. Wakati huo huo mh. Tundu Lissu amemtaka waziri mkuu ajihuzulu kotokana na kushindwa kushughulikia matatizo ya madaktari. pinda kamjibu anamheshimu sana. Mia
 
Leo kwenye kipindi cha maswali kwa waziri mkuu, Mhe Pinda amesema yeye sio Mcha Mungu.
Hivi huyu waziri mkuu anatumia akili kweli?? Hana HOFU ya MUNGU ndio maana anakuwa muongo, muoga wa kuchukua maamuzi na dhaifu katika kuendesha serikali.
Amekiri ameshindwa kutatua mgogoro wa madaktari halafu yupo yupo tu. Ahhhhh, shida tupu.
 
Ingekuwa vyema kama hao waliomshauri wangemshauri kabla ya kutoa tamko lake la "Liwalo na Liwe"...When will HE (They) learn?!!
 
Usalama uko kwenye kupiga watu wasio na hatia...wale wanaovusha wahamiaji haramu na kutorosha nyara za serikali hawaguswi kabisa
 
Hata akirudi ataishia kutoa tamko kupitia kwa wazee wa dar kama kawaida yake...
 
Mh Mbowe amemuuliza Pinda kuhusu kauli yake ya "liwalo ni liwe" na mahusiano ya tatizo la Dr Ulimboko, kakwepa na kauli ya serikali haitokuwepo leo na kukwepa kuhusika na mateso ya ulimboko

Mbowe ni jembe la ukweli.
 
Back
Top Bottom