Waziri Mkuu Mwigulu: Wakandarasi warejee site

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
443
Reaction score
305
WAZIRI MKUU: WAKANDARASI WAREJEE SITE

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameelekeza wakandarasi waliokuwa wamesimamisha kazi katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara mkoani Mara kurejea maeneo ya kazi mara moja, huku Serikali ikiendelea kuwalipa ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Serengeti, Tarime Mjini, mkoani Mara, leo Alhamisi (Julai 2, 2026), Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka utaratibu mpya wa kuhakikisha fedha za Mfuko wa Barabara zinapelekwa moja kwa moja kwenye mifuko husika ili kuondoa changamoto ya kuchelewa kwa fedha za utekelezaji wa miradi.

"Serikali imepitisha uamuzi kwamba sasa fedha za Mfuko wa Barabara hazitapitia Mfuko Mkuu. Zitakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ili barabara hizi ziweze kujengwa."

Aidha, Waziri Mkuu alisema tayari amemuelekeza Waziri wa Ujenzi kuwaita wakandarasi wote waliosimamisha kazi warejee site na kuendelea na utekelezaji wa miradi ya barabara ikiwemo Tarime–Mogabiri, Tarime–Mugumu, Sanzate–Nata, Nyamongo–Mugumu na Mogabiri–Nyamongo.

"Nimemuelekeza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi waite wakandarasi ambao walishaondoka site, warudi site na endeleeni kuwalipa fedha waendelee kutekeleza hii miradi."

Alisema kuchelewa kwa baadhi ya miradi hakukutokana na kupuuzwa kwa maeneo husika, bali ni uamuzi wa Serikali wa kuelekeza rasilimali katika kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, ambao sasa umeongeza upatikanaji wa umeme nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka asilimia tano ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kujenga miundombinu ya biashara na kununua maeneo ya kimkakati kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo, vijana na wanawake.

"Kuanzia sasa sitarajii machinga, mamalishe na vijana wanaofanya shughuli mbalimbali za biashara kupelekwa maeneo yasiyofaa. Kama wanahitaji eneo la kimkakati, litumieni asilimia tano hiyo kulinunua."

Pia alisema Serikali itawasilisha bungeni marekebisho ya sheria ya kutaifisha mifugo kwa lengo la kuondoa adhabu zisizo na uwiano kwa wafugaji na kuendelea kulinda shughuli za uzalishaji.

Aidha, Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali imepiga marufuku kukamatwa kwa vitendea kazi vya wananchi kwa madai ya faini, akieleza kuwa hatua hiyo imekuwa ikikwamisha shughuli za uzalishaji na kujiongezea kipato.

"Kama jambo ni la faini, acheni kukamata vitendea kazi vya Watanzania. Waacheni wafanye kazi."

Sambamba na hayo, Waziri Mkuu alitoa wito kwa viongozi wa Serikali na Chama kujikita katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo badala ya kuanza makundi ya uchaguzi mapema, akisema wananchi wanahitaji huduma na maendeleo, si migogoro ya kisiasa.

Akihitimisha, Waziri Mkuu aliwataka wananchi kuendelea kulinda amani, umoja na mshikamano wa Taifa, akisisitiza kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Ilani ya Uchaguzi na mipango mingine ya maendeleo utafanikiwa endapo nchi itaendelea kuwa na amani, utulivu na usalama.
IMG-20260702-WA0101.jpg
IMG-20260702-WA0114.jpg
IMG-20260702-WA0108.jpg
IMG-20260702-WA0111.jpg
IMG-20260702-WA0118.jpg
IMG-20260702-WA0117.jpg
IMG-20260702-WA0110.jpg
IMG-20260702-WA0100.jpg
IMG-20260702-WA0109.jpg
 
WAZIRI MKUU: WAKANDARASI WAREJEE SITE

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameelekeza wakandarasi waliokuwa wamesimamisha kazi katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara mkoani Mara kurejea maeneo ya kazi mara moja, huku Serikali ikiendelea kuwalipa ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Serengeti, Tarime Mjini, mkoani Mara, leo Alhamisi (Julai 2, 2026), Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka utaratibu mpya wa kuhakikisha fedha za Mfuko wa Barabara zinapelekwa moja kwa moja kwenye mifuko husika ili kuondoa changamoto ya kuchelewa kwa fedha za utekelezaji wa miradi.

"Serikali imepitisha uamuzi kwamba sasa fedha za Mfuko wa Barabara hazitapitia Mfuko Mkuu. Zitakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ili barabara hizi ziweze kujengwa."

Aidha, Waziri Mkuu alisema tayari amemuelekeza Waziri wa Ujenzi kuwaita wakandarasi wote waliosimamisha kazi warejee site na kuendelea na utekelezaji wa miradi ya barabara ikiwemo Tarime–Mogabiri, Tarime–Mugumu, Sanzate–Nata, Nyamongo–Mugumu na Mogabiri–Nyamongo.

"Nimemuelekeza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi waite wakandarasi ambao walishaondoka site, warudi site na endeleeni kuwalipa fedha waendelee kutekeleza hii miradi."

Alisema kuchelewa kwa baadhi ya miradi hakukutokana na kupuuzwa kwa maeneo husika, bali ni uamuzi wa Serikali wa kuelekeza rasilimali katika kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, ambao sasa umeongeza upatikanaji wa umeme nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka asilimia tano ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kujenga miundombinu ya biashara na kununua maeneo ya kimkakati kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo, vijana na wanawake.

"Kuanzia sasa sitarajii machinga, mamalishe na vijana wanaofanya shughuli mbalimbali za biashara kupelekwa maeneo yasiyofaa. Kama wanahitaji eneo la kimkakati, litumieni asilimia tano hiyo kulinunua."

Pia alisema Serikali itawasilisha bungeni marekebisho ya sheria ya kutaifisha mifugo kwa lengo la kuondoa adhabu zisizo na uwiano kwa wafugaji na kuendelea kulinda shughuli za uzalishaji.

Aidha, Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali imepiga marufuku kukamatwa kwa vitendea kazi vya wananchi kwa madai ya faini, akieleza kuwa hatua hiyo imekuwa ikikwamisha shughuli za uzalishaji na kujiongezea kipato.

"Kama jambo ni la faini, acheni kukamata vitendea kazi vya Watanzania. Waacheni wafanye kazi."

Sambamba na hayo, Waziri Mkuu alitoa wito kwa viongozi wa Serikali na Chama kujikita katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo badala ya kuanza makundi ya uchaguzi mapema, akisema wananchi wanahitaji huduma na maendeleo, si migogoro ya kisiasa.

Akihitimisha, Waziri Mkuu aliwataka wananchi kuendelea kulinda amani, umoja na mshikamano wa Taifa, akisisitiza kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Ilani ya Uchaguzi na mipango mingine ya maendeleo utafanikiwa endapo nchi itaendelea kuwa na amani, utulivu na usalama.View attachment 3621003View attachment 3621004View attachment 3621005View attachment 3621006View attachment 3621007View attachment 3621008View attachment 3621009View attachment 3621012View attachment 3621013
Je ni wale wakufukia mahandaki barabarani au ni wakandarasi gani,ama wote kwenye miradi yote?
 
Nani aliyeruhusu uhamishaji wa mafungu ya mfuko wa barabara (Road Fund) wakati sheria hairuhusu hivyo walioko juu wanaweza kujiamulia mambo bila idhini ya bunge ? Pm atueleze maana yeye ndio alikuwa huko hazina wakati haya yanatendeka alimshauri rais akubali kuhamisha mafungu ya mfuko wa barabara pasipo idhini ya bunge hata kama nia ilikuwa njema kwanini alitoa ushauri ulioleta athari kubwa sio tu kwa kukiuka sheria lakini wengi wa wakandarasi wamefilisika mali zao kuuzwa na taasisi za fedha kutokana na kutolipwa madai yao licha ya kufanya kazi. Uharibifu mkubwa wa barabara zetu zote kuu (Regional & Trunk Roads) kutokana na kukosekana kwa fedha za marekebisho/matengenezo. Kwanini asiwajibike kwa kusababisha hayo hapo maana huwezi ukasema nia ilikuwa ukamilishe miradi ya kimkakati halafu kwingine watu wafilisike na mali zao kuuzwa kutokana na kutolipa marejesho kwa wakati baada ya wakala wa barabara kushindwa kuwalipa.
Mkandarasi gani leo atakuwa na imani ya kurejea site kwamba aendelee na kazi huku akisubiri malipo wakati mwanzo ashang'atwa na nyoka hivyo hata jani tu lazima limuogopesha (once bitten twice shy) hii inanikumbusha zama zile kabla ya kuanzishwa wa wakala wa barabara ilikuwa ikiitwa idara ya ujenzi, ndio tumerejea kwa kasi ya ajabu huko barabara zilikuwa mbovu kuliko na pesa kulikuwa hakuna za kuzitengeneza kwanini tumeanzisha mamlaka na tukaitungia sheria halafu tunavunja na kukuika sheria kisha tunakuja na utetezi kuwa tulikuwa tunakamilisha miradi ya kimkakati.
 
Nani aliyeruhusu uhamishaji wa mafungu ya mfuko wa barabara (Road Fund) wakati sheria hairuhusu hivyo walioko juu wanaweza kujiamulia mambo bila idhini ya bunge ? Pm atueleze maana yeye ndio alikuwa huko hazina wakati haya yanatendeka alimshauri rais akubali kuhamisha mafungu ya mfuko wa barabara pasipo idhini ya bunge hata kama nia ilikuwa njema kwanini alitoa ushauri ulioleta athari kubwa sio tu kwa kukiuka sheria lakini wengi wa wakandarasi wamefilisika mali zao kuuzwa na taasisi za fedha kutokana na kutolipwa madai yao licha ya kufanya kazi. Uharibifu mkubwa wa barabara zetu zote kuu (Regional & Trunk Roads) katokana na kukosekana kwa fedha za marekebisho/matengenezo. Kwanini asiwajibike kwa kusababisha hayo hapo maana huwezi ukasema nia ilikuwa ukamilishe miradi ya kimkakati halafu kwingine watu wafilisike na mali zao kuuzwa kutokana na kutolipa marejesho kwa wakati baada ya wakala wa barabara kushindwa kuwalipa.
Mkandarasi gani leo atakuwa na imani ya kurejea site kwamba aendelee na kazi huku akisubiri malipo wakati mwanzo ashang'atwa na nyoka hivyo hata jani tu lazima limuogopesha (once bitten twice shy) hii inanikumbusha zama zile kabla ya kuanzishwa wa wakala wa barabara ilikuwa ikiitwa idara ya ujenzi, ndio tumerejea kwa kasi ya ajabu huko barabara zilikuwa mbovu kuliko na pesa kulikuwa hakuna za kuzitengeneza kwanini tumeanzisha mamlaka na tukaitungia sheria halafu tunavunja na kukuika sheria kisha tunakuja na utetezi kuwa tulikuwa tunakamilisha miradi ya kimkakati.
do we have rule of law ?
 
Ni amani gani PM anataka wananchi waendelee kuilinda? Hiyo ya kuteka na kuwaua Watanganyika?

Kwa nini asitoe tangazo rasmi kuwa kuanzia sasa hawatawateka watu na kuwapoteza au kuwaua? Na kwamba hawatathubutu tena kukanyaga haki za wananchi?
Kulinda hali iliyopo, inamaanisha kulinda utekaji na mauaji ya wananchi, kuwabambikia watu kesi, kudhulumu haki za wananchi, kupora mamlaka ya wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka, kulinda ufisadi na uporwaji wa rasilimali za nchi.
 
Wengine tukisema kwasasa mikoa yote ya Tanzania ipo kwenye Ujenzi watu awaelewi

Badala kusisimka na Ujenzi wa Taifa lao👈
Baadhi yao wapo kuwapinga na kuwabeza Majembe yatu
Walioamua kuchapa kazi mwanzo mwisho✍️
 
Ni amani gani PM anataka wananchi waendelee kuilinda? Hiyo ya kuteka na kuwaua Watanganyika?

Kwa nini asitoe tangazo rasmi kuwa kuanzia sasa hawatawateka watu na kuwapoteza au kuwaua? Na kwamba hawatathubutu tena kukanyaga haki za wananchi?
Kulinda hali iliyopo, inamaanisha kulinda utekaji na mauaji ya wananchi, kuwabambikia watu kesi, kudhulumu haki za wananchi, kupora mamlaka ya wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka, kulinda ufisadi na uporwaji wa rasilimali za nchi.
Ndio ushangae utekaji, mauwaji na upotezaji ndio unashamiri sasa mtu amepotelewa na ndugu, jamaa, mzazi, rafiki, mjomba halafu asilalamike kisa eti kutunza sijui amani ambayo hao walioshika madaraka wanakula keki na familia zoo wakati walio wengi wanilia njaa na ukata na kupotezwa kwa wapendwa wao. Fikiria familia ya Mzee Kibao, Gwanda, Soka, Ben Saanane, Mdude, Chaula, Kapanya na wengi waliopetezwa
 
Huyu ndio alisemwa na Makonda kuwa anatumia matatizo ya wananchoio kuzunguka kujiandaa kutafuta uraisi 2030? Kama kweli mbona
 
Nani aliyeruhusu uhamishaji wa mafungu ya mfuko wa barabara (Road Fund) wakati sheria hairuhusu hivyo walioko juu wanaweza kujiamulia mambo bila idhini ya bunge ? Pm atueleze maana yeye ndio alikuwa huko hazina wakati haya yanatendeka alimshauri rais akubali kuhamisha mafungu ya mfuko wa barabara pasipo idhini ya bunge hata kama nia ilikuwa njema kwanini alitoa ushauri ulioleta athari kubwa sio tu kwa kukiuka sheria lakini wengi wa wakandarasi wamefilisika mali zao kuuzwa na taasisi za fedha kutokana na kutolipwa madai yao licha ya kufanya kazi. Uharibifu mkubwa wa barabara zetu zote kuu (Regional & Trunk Roads) kutokana na kukosekana kwa fedha za marekebisho/matengenezo. Kwanini asiwajibike kwa kusababisha hayo hapo maana huwezi ukasema nia ilikuwa ukamilishe miradi ya kimkakati halafu kwingine watu wafilisike na mali zao kuuzwa kutokana na kutolipa marejesho kwa wakati baada ya wakala wa barabara kushindwa kuwalipa.
Mkandarasi gani leo atakuwa na imani ya kurejea site kwamba aendelee na kazi huku akisubiri malipo wakati mwanzo ashang'atwa na nyoka hivyo hata jani tu lazima limuogopesha (once bitten twice shy) hii inanikumbusha zama zile kabla ya kuanzishwa wa wakala wa barabara ilikuwa ikiitwa idara ya ujenzi, ndio tumerejea kwa kasi ya ajabu huko barabara zilikuwa mbovu kuliko na pesa kulikuwa hakuna za kuzitengeneza kwanini tumeanzisha mamlaka na tukaitungia sheria halafu tunavunja na kukuika sheria kisha tunakuja na utetezi kuwa tulikuwa tunakamilisha miradi ya kimkakati.
Unaendaje site bila kupewa Pesa Mwigulu ndo alikua waziri wa fedha wakati mfuko road fund unakufa huyu Mwigulu hawezi kuaminika amejikita kwenye propaganda Kama katibu mwenezi wa chama Wakandarasi wamefilisika alafu yeye analeta porojo
 
Hakika ndio maana mpaka leo hii anaendekeza propaganda zake mara mabomu, milioni 5, vijana wamefundishwa badala ya kuja na majibu ya masuala magumu yanayoikabili nchi yetu kama hayo ya kutolipwa kwa wakandarasi mpaka kupelekea wengine kufilisika, mauwaji, utekaji, kupotea kwa watu na wengine kuokotwa wakiwa wamekufa nk. Ubovu wa miundombinu kama vile barabara nchi nzima, upatikanaji wa maji safi na salama mfano Mwanza tumeshuhudia licha ya kuwa pembezoni mwa ziwa lakini kuna adha kubwa sana ya maji safi na salama kwaajili ya matumizi ya binadamu maana hili nalo ni ajabu jingine halafu waziri husika yupo anapiga porojo bungeni. Badala yake tumeshuhudia jana na juzi akiwa Musoma (Mara) akiendeleza propaganda na porojo zake za mabomu, kuvuruga amani halafu anadai wakandarasi warudi site ilihali hawajalipwa madai yao wala haijulikani lini watalipwa na chanzo cha mtanziko ni yeye wakati akiwa hazina aliyetoa ushauri wa kuondoa mafungu ya mfuko wa barabara na kuhamishia mfuko mkuu bila kutambua mkwamo utakao tokea huko mbele sasa hivi ndio tunaona shida aliyotuletea barabara karibu 89% zimeharibika kotę nchini na pesa za kutengeneza hakuna halafu pm anakuja kutueleza kuwa zilienda kwenye miradi ya kimkakati na huko pia walikopa nido maana tunaona deni niani ya miaka 4 limeongezeka zaidi ya 50tilioni.​
 
Pesa za road fund wamechota wahuni na kutumia
 
WAZIRI MKUU: WAKANDARASI WAREJEE SITE

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ameelekeza wakandarasi waliokuwa wamesimamisha kazi katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara mkoani Mara kurejea maeneo ya kazi mara moja, huku Serikali ikiendelea kuwalipa ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Serengeti, Tarime Mjini, mkoani Mara, leo Alhamisi (Julai 2, 2026), Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka utaratibu mpya wa kuhakikisha fedha za Mfuko wa Barabara zinapelekwa moja kwa moja kwenye mifuko husika ili kuondoa changamoto ya kuchelewa kwa fedha za utekelezaji wa miradi.

"Serikali imepitisha uamuzi kwamba sasa fedha za Mfuko wa Barabara hazitapitia Mfuko Mkuu. Zitakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ili barabara hizi ziweze kujengwa."

Aidha, Waziri Mkuu alisema tayari amemuelekeza Waziri wa Ujenzi kuwaita wakandarasi wote waliosimamisha kazi warejee site na kuendelea na utekelezaji wa miradi ya barabara ikiwemo Tarime–Mogabiri, Tarime–Mugumu, Sanzate–Nata, Nyamongo–Mugumu na Mogabiri–Nyamongo.

"Nimemuelekeza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi waite wakandarasi ambao walishaondoka site, warudi site na endeleeni kuwalipa fedha waendelee kutekeleza hii miradi."

Alisema kuchelewa kwa baadhi ya miradi hakukutokana na kupuuzwa kwa maeneo husika, bali ni uamuzi wa Serikali wa kuelekeza rasilimali katika kukamilisha miradi ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere, ambao sasa umeongeza upatikanaji wa umeme nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema Serikali imeweka asilimia tano ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya kujenga miundombinu ya biashara na kununua maeneo ya kimkakati kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo, vijana na wanawake.

"Kuanzia sasa sitarajii machinga, mamalishe na vijana wanaofanya shughuli mbalimbali za biashara kupelekwa maeneo yasiyofaa. Kama wanahitaji eneo la kimkakati, litumieni asilimia tano hiyo kulinunua."

Pia alisema Serikali itawasilisha bungeni marekebisho ya sheria ya kutaifisha mifugo kwa lengo la kuondoa adhabu zisizo na uwiano kwa wafugaji na kuendelea kulinda shughuli za uzalishaji.

Aidha, Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali imepiga marufuku kukamatwa kwa vitendea kazi vya wananchi kwa madai ya faini, akieleza kuwa hatua hiyo imekuwa ikikwamisha shughuli za uzalishaji na kujiongezea kipato.

"Kama jambo ni la faini, acheni kukamata vitendea kazi vya Watanzania. Waacheni wafanye kazi."

Sambamba na hayo, Waziri Mkuu alitoa wito kwa viongozi wa Serikali na Chama kujikita katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo badala ya kuanza makundi ya uchaguzi mapema, akisema wananchi wanahitaji huduma na maendeleo, si migogoro ya kisiasa.

Akihitimisha, Waziri Mkuu aliwataka wananchi kuendelea kulinda amani, umoja na mshikamano wa Taifa, akisisitiza kuwa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Ilani ya Uchaguzi na mipango mingine ya maendeleo utafanikiwa endapo nchi itaendelea kuwa na amani, utulivu na usalama.View attachment 3621003View attachment 3621004View attachment 3621005View attachment 3621006View attachment 3621007View attachment 3621008View attachment 3621009View attachment 3621012View attachment 3621013
Ni kweli kabisa Pm

Waziri wa fedha wa wakati huo atueleze zile road fund jinsi zilivyojenga barabara nyingi
 
Back
Top Bottom