Bungeni Live: June 28, 2012

hivi hili tatizo la viongozi wetu kuto kauli za hovyo halafu baadae wanakuja kumeza matapishi yao itaisha lini?
ile liwalo na liwe la jana ya Pinda imeenda wapi leo?
 
Ni kawaida ya Serikali kuahidi bila kufikiri na baadaye wanakuja na taarifa ya kughairi au kimya tu.
 
Waziri Mkuu,ametuma Salamu za pole kwa Dr Ulimboka
Neno lake la liwalo na liwe alitamka kuepuka kuonekana Mtovu wa nidhamu kuzungumza huku akijua Jambo hili lipo Kwenye Muhimili mwingine.Akasema hata wakimlaumu viongozi wenzake basi litakalo kuwa na liwe.

Pinda ni mtu wa hivi hivi.
 
Nipo hapa MOI tangu juzi mgonjwa wetu aliandikiwa kufanyiwa upasuaji leo mchana, sasa hivi tunatoka kupewa taarifa kuwa haitowezekana kwa kuwa daktari mhusika hatokuwepo, na kuna tv hapa inayoonyesha bunge namsikiliza waziri mkuu, tumaini la mgonjwa wetu limepotea sijui tutafanyaje aaahh!!
 
Hawezi kutoa tamko jamaa ni dhaifu ameshaambiwa atulie kwanza
 
amesema ikibidi kauli yake isifutwe kwenue hansard ila spika anaweza amua kufuta au asifute....du
eti lugalo wanajitosheleza kutibu
 
Wanawataka wananchi waende hospital za jeshi!,lugalo na zingine zilizo chini ya jeshi.
 
Amepangua vibaya ( kidhaifu) mpaka imemuangukia! Pole Pinda kwa ugoigoi wako na serikali yako!
 
Swali la tundu lisu bungeni, kwa waziri mkuu.. Ili kulinda maslah pinda anajikanyaga kanyaga
 
Hiyo kauli alisema jana! Au ndio kusema hafahamu alichokuwa anasema?

Anafahamu vizuri sana...na kwasababu liwalo na liwe halijaweza kuwa, amefuta kauli yake pengine. I feel annoyed with these kind of leaders.
 
Pinda, kauli ya lolote na liwe alioitoa juu ya Mgomo wa Madaktari Alimaanisha kwa vile kesi
ipo Mahakamani na kwa kuheshimu muhimili wa dola. Yani Mahakama. Serikali haipaswi
kutoa kauli au kusemea shauri lililopo Mahakamani. Lakini kwa vile wanao athirika ni
wananchi na wanakufa. Hivyo lOLOTE NA LIWE serikali italisemea na kama itakua imeingilia
Mahakama, LOLOTE NA LIWE,
 
Tundu Lissu amtaka waziri mkuu ajiuzulu kwa kua mwezi wa pili mgomo ulishughulikiwa kwenye offisi yake na wakatangaza mgomo umeisha na sasa umerudi tena,

IF YOU TRIED YOUR BEST ANY YOU HAVE PROOF FAILURE WHY DONT YOU RESIGN?

Majibu ya waziri mkuu,
Mheshimiwa Tundu Lissu nakuheshimu sana lakini thats not the best approch hasa kwa mkubwa.
 
ni swali ambalo muheshimiwa tundu lisu amemuuliza pinda! Kwa nin asijiuzulu kwa sababu ameshindwa kutatua kwa mda mrefu.. Mgogoro wa madaktari.. Ili kulinda maslah ya serikali na taifa kwa ujumla..
 
Tundu Lissu huyo amwambia alitoa ahadi kuwa hakuta kuwa na mgomo tena na umetokea kwanini asijiuzulu kwa kushindwa kutatua tatizo la madaktari
 
Aachie kitumbua chake ngumu! Kasema kuna kitu kinachoweza kumfanya ajiuzulu ila siyo ishu ya madoctor!
 
Lilikuwa swali la nyongeza toka kwa Tundu Lisu wakati wa maswali ya papo hapo kwa Waziri mkuu.

Namuunga mkono Tundu Lisu, kwa hili japo Makinda kama kawaida yake ameendeleza ubabe.
 
Nimeshangazwa na maswali ya huyu mbunge kwa waziri mkuu! Eti anadai madaktari wanatumika na watu wanaowapatia fedha kuhamasisha mgomo ili nchi isitawalike.
Hivi huyu mbunge ni wa kuchaguliwa kihalali au ni wa viti maalum, na sasa anataka kubembeleza ukaribu kwa waliomchagua?
 
Back
Top Bottom