BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,117
Ukaguzi uliofanywa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) umebaini HESLB iliwapa Mikopo Wanafunzi ambao hawakuwa Vyuo Vikuu kwa maelekezo ya Serikali.
Pia, PAC imesema kati ya 2018/19 wanafunzi 2,852 walipangiwa mikopo chini ya kiwango kwa upungufu wa Tsh. Bilioni 1.14 huku Tsh. Bilioni 2.25 zikilipwa kwa wasiokuwa na uhitaji.
Aidha wanafunzi 6,182 walipangiwa mikopo zaidi ya kiwango kwa kiasi cha Tsh. Bilioni 5.66 wakati wanafunzi wapya wengi wakipangiwa chini ya 100%.
=======================
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (PAC) imebaini utoaji wa mikopo inayofikia Sh1.76 bilioni kwa wanafunzi wasiostahili katika kipindi cha kati ya mwaka 2016 hadi mwaka 2018.
Hayo yamesemwa leo Jumanne Novemba 2, 2022 na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Japhet Hasunga wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2021.
Amesema mikopo hiyo ilitolewa kati ya mwaka 2016 hadi 2018 kwa wanafunzi ambao hawakuwa kwenye vyuo vya elimu ya juu lakini walipewa mikopo kwa maelekezo ya Serikali
Amesema uchambuzi wa taarifa ufanisi kuhusu upangaji na ugawaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kumeonekana uwepo wa maboresho makubwa katika taratibu za utoaji wa mikopo na ongezeko la idadi ya wanufaika wa mikopo husika.
Amesema pia kumekuwa na ongezeko la wanufaika wa mikopo kutoka 116,706 (2016/2017) hadi 149,389 (2020/2021). Alisema upangaji wa mikopo usiotosheleza kwa wanafunzi wapya ambapo Bodi haikuweza kutoa mikopo kwa asilimia 100 kwa waombaji waliostahili.
Alisema walibaini pia waombaji kupangiwa ada chini ya kiwango na zaidi ya kiwango cha ada stahiki na kwamba mwaka 2018/2019 wanafunzi 6,182 walipangiwa mikopo zaidi ya kiwango kwa kiasi cha Sh5.66 bilioni.
Alisema wanafunzi 2,852 walipangiwa mikopo chini ya kiwango kwa upungufu wa Sh1.14 bilioni na upangaji wa mikopo inayofikia Sh 2.25bilioni kwa waombaji wasiokuwa na uhitaji.
“Kutowapangia mikopo wanafunzi wanaostahili kupata mikopo na usimamizi hafifu wa bakaa na fedha za wanafunzi wanaohama vyuo na uhamasishaji duni wa vyanzo vingine vya fedha kwa ajili ya mpango wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu,” amesema.
MWANANCHI