Bodi ya Mikopo Kuwapa Mikopo Wanafunzi Waliotemwa Samia Scholarship

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Serikali imewahakikishia kupata mikopo wanafunzi 226 ambao wametemwa katika ufadhili wa masomo wa Samia ‘Samia Scholarship,’ baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya kuendelea kupata ufadhili huo.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Heslb), Omega Ngole amesema litafunguliwa dirisha maalumu la maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kwa ajili yao ili kuwapa nafasi ya kuomba mkopo.

Hata hivyo inaelezwa kuwa, wakati katika 'Samia Scholarship' wanafunzi hao walipata ufadhili bure na wa asilimia 100, kupitia Heslb; watapata mikopo kulingana na vigezo vilivyowekwa na mfuko huo, huku wakitarajiwa kurejesha kama sheria na kanuni za mfuko huo zinavyoelekeza.
 
Mikopo elimu ya juu inatolewa kwa upendeleo. kama huna refa awamu zote za utoaji mikopo itaisha kisha unaambiwa ukate rufaa kwa vigezo sharti uwe na ushahidi ya kwamba wewe na familia yako ni wanachama wa TASAF, Mlemavu, au Yatima vitu vya ajabu sana na vinavunja ndoto za vijana wakati mikopo hiyo mhitimu atawajibika kuja kurejesha sio unatolewa bure.

RAIA ya BUSARA kwa Serikali

Kupitia nodi ya mikopo @HESLB
Wanafunzi waliochagua fani ambazo sio mahitaji maalu na vipaumbele kama walipata daraja la kwanza kidato cha sita inashauriwa wapewe mikopo kwa asilimia angalau 65% au 70% maana sio bure watarejesha pindi wahitimupo na kuajiriwa. naamini kwa dhati watawashukuru sana na watajitahidi kuitendea haki taalumu wanazozichukua ili waje walitumikie taifa lao kwa moyo wote na faida ya kiuchumi na kijamii.
 
Back
Top Bottom