Escrowseal1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 4,430
- 4,222
Serikali ya awamu ya Sita hivi karibuni ilijitutumua kuwa inao uwezo wa kulipia wanafunzi wote wanaoqualify kupata mikopo elimu ya juu ,ila pia ikaenda mbali na kupiga siasa kuwa itawakopesha wanafunzi wa elimu ya kati.
Ki ukweli hali ni tofauti wanafunzi wengi wenye vigezo hawajapewa mikopo na wana maisha magumu Sana vyuoni. Wengi inawalazimu ukoo mzima kuchangishana na kuwalipia mahitaji huku serikali ikipiga chenga kama za mchezaji Pele kuwa inashughulikia appeal zao.
Wanafunzi kurundikwa vyuoni na hasa wa kike wanawekwa kwenye majaribu makubwa. Kipindi hiki cha mitihani vijana wanahaha maana wasipolipa hawawezi kuendelea na mwaka wa masomo . Inabidi watoto kutapatapa kutafuta pesa kwa ndugu na jamaa wasio na majukumu juu yao.
Serikali ya CCM aliyewaroga aliishia wapi. Acheni kufanya siasa na future za watu. Kwa ufaulu niliouona mwaka huu nilijua kabisa kuna usanii utatokea . Kuna baadhi wameambiwa baada ya kufanya appeal kuwa watapewa mikopo mwakani , at the same time bado watoto wanahangaika chakula na na Karo na hawezi kuruhusiwa kufanya mitihani.
Hebu wahusika acheni kufanya udalali na future za wanetu wekeni mipango inayopimika na kama hamna uwezo basi hizo passes mnazotoa pungizeni wapate wenye ufaulu wa may be point kadhaa na kama serikali haina uwezo semeni kuliko Kufa na tai shingoni .CCM mmogwa na nani?