Nape akipata wasaa, asome tena hiyo nukuu aliyotoa kwenye gazeti la Nipashe. Inamvunjia heshma - yeye Nape- na pengine ni vema , in the future, akavuta pumzi na kutulia kabla ya kuongea na waandishi wa habari.
Kuonesha ni jinsi gani Nape amelikoroga, anasema: 'anaunga mkono jambo lolote linalota heshma kwa bunge'. Lakini anaendelea kwa kusema kuwa bunge linarushwa 'live' wakati wa asubuhi, na wakati huo (kwa maoni ya Nape) watu wako makazini, hivyo hawana muda wa kufuatili'
Kwa maneno mepesi sana, Nape anataka watu waazima na akili zao waamini kuwa kuonesha vikao vya bunge live- asubuhi kunalivunjia heshma bunge! Hii ni hadithi ya ajabu kabisa toka kwa Nape, na ndio maana nashauri asome tena nukuu yake ili aepushe chama chake na taifa kwa jumla na haya masimulizi ya kuanga-unga.
Heshma ya bunge haina uhusiano wowote na kurushwa live asubuhi, mchan, jioni au usiku wa manane. Kama bunge linaendeshwa kihuni kihuni, bila kufutata kanuni na taratibu zilizowekwa, usitegemee heshma. Kwa bahati nzuri tunayo mifano halisi. Bunge la Tanzania lilipata hesham kubwa wakati wa Spika Sitta. Na hii ni kwa sababu ya uelewa wake na kuheshimu utawala wa sheria lakini pia kuelewa kuwa bunge ni mhimili huru na wa muhimu kwa uhai wa taifa. Sitta aliongoza bunge kwa HAKI.
Makinda, kwa sababu anazozijua yeye, licha ya kuwa Naibu Spika wakati wa Sitta, amerudisha nyuma hatua zote tulizofikia, kama taifa kwenye suala zima la utawala wa sheria. Bunge haliwezi kuwa na heshma kama anayeongoza haelewi 'equation' ya heshma ya bunge inajumuisha nini? Bunge haliwezi kuwa na heshma kama mkalia kiti cha Spika anavuruga kanuni, taratibu,tamaduni/desturi zilizowekwa kuongoza bunge? Ukisshavuruga kanuni maana yake unaruhusu 'chaos'. Na dawa yake si kutoonesha vikao vya bunge 'live'. Hivyo, hoja ya Nape ni ya kipuuzi na haiwezi kutatua tatizo la msingi linaloharibu bunge.