Bunge Lisirushe Matangazo yake 'LIVE' - Nape

Bunge Lisirushe Matangazo yake 'LIVE' - Nape

alafu baadae mje kutuambia kwamba chadema wameingia bungeni na mabomu ya alshababu. Huo ujinga hakuna mtu ataukubali isipokuwa baadhi tu, ya magamba

kweli kabisa ndugu......hawa watu ni kama wachawi!
 
hao wasioenda kazini au maofisini unafikiri huwa wanazubaa ndani kuangalia bunge?kwa taarifa asilimia 80 ya nyumba mda huu ziko empty,au wapo mahousgal au wamama wa nyumbani na wako busy wanafanya usafi,kupiga deki kuosha vyombo,kufua,kuenda sokoni,kuandaa mlo wa mchana etc.
Wanaongaliaga TV mida kama hii hawazidi 5000 nchi nzima.

Hoja hapa ni sababu za kutorusha bunge live,hoja sio wangapi wanaangalia bunge.sababu alizotoa katibu wa bunge ni kwamba kuna wabunge wanatafuta misifa kwa kuwa wanaonekana live.swala sio wangapi wanaangalia bunge kwa muda gani.
 
HII MANENO NDIO INAWAPONZA...........HAWAPENDI TUIONE

bingoland.jpg

Mkuu huyu akigutuka usingizini atajibu.....NDIYOOOOOOOOO. na kugonga meza
 
Nataka nimtaarifu nape kuwa, kuangalia bunge sio tu mpaka ukae kwenye runinga, kupitia kwenye mitanado tunaweza kupata habari nyingi nini kinachoendelea bungeni, online tv, nape haihitaji kuwepo nyumbani ndio uone bunge, hata maofisini tunafuatilia, isitoshe ni haki yetu kuona wawakilishi wetu, nafikiri katika kosa ambalo ccm itafanya ni kukatiza haki ya kwa wanachi.

Mi nadhani wakati mwingine CCM, inawapa bureeeeee umaarufu vyama vya upinzani bila gharama yoyote, kuvipandisha chati bila gharama yoyote.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

“Suala la Bunge kurushwa ‘live’ halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?” alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa

MIMI SI MWANA UBUNGO ILA,Mnyika atabaki kuwa mnyika tu.Ni tofauti kabisa na Vipaza sauti kama NAPE,MWIGULU,LUSINDE,SHIGELLA,SHONZA aka dada CHIPS KUKU n.k .

Mnyika ni hazina ya Taifa hili kwa siku zajazo bila kujali chama gani atakuwa anakiwakilisha.Huwezi kuona maendeleo kama huna macho na ndo maana huwezi kuwa huru kwa sababu bado wewe ni mtumwa.

NAPE Badilika,jifunze,tembea uone ndo useme.Kataa kuwa mtumwa..
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

"Suala la Bunge kurushwa ‘live' halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?" alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa

Hapa ndipo unapoweza jua kuwa Tanzania kwa sasa hatuna viongozi makini. Maana ukisikilza kauli za waheshimiwa hawa kila mtu anajaribu kutoa sababu zake ambazo hazina chembe yoyote ya ukweli. Kwanza Makinda aliwahi kuwasifia TBC kwa kuonyesha Bunge LIVE,na akaipongeza serikali kwa kuongeza Bajeti ya Wizara ya Habari.

Lakini juzi baada ya kiti cha Spika na Naibu wake kuanza kupoteza mwelekeo Watu walewale wameanza kutoa sababu za kipuuzi kabisa. Katibu wa Bunge Bwana Kashililla anasema kuanzia sasa hakuna kuonyesha Bunge LIVE kwasababu ili kuzuia VURUGU za Wabunge wa CHADEMA wanaotaka umaarufu kupitia runinga!!!Lakini akaongeza pia kuwa itakuwa ni marufuku kwa waandishi wa Habari ku-recor/ku-mpiga picha Mbunge/Waziri anayelala Bungeni!!!Kwa hiyo kuanzia sasa watakuwa wana-RECORD, wana-EDIT na baadaye ku-BROADCAST hewani vipindi hivyo vya Bunge kwa ajili kulinda Heshima ya Bunge!!!

Naibu wa Spika Bwana Job Ndugai yeye amedai kuwa sababu ya kuondoa matangazo ya Bunge LIVE ni kutaka KUIMALIZA CHADEMA kisiasa kwa kuiondolea Umaarufu wa bure inaopata kutokana na vipindi vya Bunge kurushwa LIVE!!!

Leo Nape yeye anasema anaunga mkono maana wakti vipindi vya Bunge vinarushwa Watanzania wanakuwa hawaangalii maana wako makazini!!!!Hiki ni kichekesho cha karne. Hivi huyu Bwana Nape anataka kutuambia kuwa Watanzania wote ni Wakulima na Wafanyakazi tu??? Hivi Nape hajui kuwa kuna Watu kama wafanyabiashara wanaangalia Runinga wakiwa kwenye Bisahara zao???Mtu yuko dukani anasubiri Wateja au anasimamia bisahara zake na kuna wafanyakazi chini yake kwanini asiangalie runinga na akiwa amechagua chaneli ya TBC Bungeni Dodoma????Mbona hata kwenye maofisi haya haya ya serikali tunakuta Runinga zimewekwa maofisini na zinaangaliwa. Nimepitia ofisi kama Mabenki,Halmashauri za Miji, Wilaya na majiji kuna TV, ingia ofisi zote za Wakurugenzi, RC na DC wote wana ving'amuzi na wametune TBC!!!!

Kwa hiyo hoja ya Nape ni dhaifu sana wala haina mashiko. Pengine aliyesema sababu hasa za kutaka kuwamaliza CHADEMA kwa kuzuia umaarufu wao wanaoupata siku kwa siku kutokana na HOJA zao nzito zinazoitia serikali ya CCM KIWEWE!!Huu ndiyo ukweli na sababu za serikali kutaka kuzuia progrmmmes za TBC Bunge live kutorushwa LIVE!

CCM wamegundua kuwa Upinzani Bungeni na hasa CHADEMA unaendelea ku-gain popularity kutoka na HOJA nzito zinazoibuliwa na Wabunge wake na kuibana Serikali kiasi cha kushindwa kujitetea.Watu wanaweza kuhoji na kujiuliza mambo kama haya hayakuwahi kujitokeza wakati Bunge likiwa chini ya Spika Sam Sitta(Spika wa Speed)! Miaka 5 ya Sitta hatukusikia vurugu za Upinzani, Wabunge kupigwa picha wamelala(Walikuwa wakilala) kwa sababu Sitta aliliendesha Bunge kama inavyostahili kwa Bunge la Vyama vingi bila ya Upendeleo wala kuionea serikali aibu!!!

Sababu zingine zote zilizotolewa na hazina mashiko. Lakini CCM wajue kwamba Bunge hili si mali ya mtu fulani,si la CCM wala Makinda,Ndugai, Kikwete au Fisadi yoyote anayefikiri hivo. Bnge hili ni mali ya Watanzania wakiwa ni waajiri wa Wabunge wote,Mawaziri,Spika na Naibu wake maana ndiyo waliowapa ridhaa ya kutuwakilisha Bungeni kwa kura zetu. Sasa hatuwaelewi wanapoanza kutaka kutunyima uhuru wetu wa kuangalia Bunge LIVE. Hatutaki wala hatuhitaji kuona vipindi RECORDED and EDITED kujaribu kuficha UDHAIFU wa Serikali ya CCM ili kutaka kujiandalia ushindi hewa wanaouita wa KISHINDO!

Nahitimisha kwa kusema kuwa aktika hoja hii DHAIFU ya Uongozi wa Bunge akiwemo Spika Anna Makinda,Naibu Job Ndugai,Katibu Thomas Kashilila na Serikali wa kutaka kuondoa matangazo LIVE ya BUNGE nikutaka kujidanganya wenyewe. Tayari Watanzania wameshagundua na kung'amua sababu kubwa hasa ya kuondoa LIVE Broadcast ni KUTAKA KUFICHA UDHAIFU WA SERIKALI YA CCM NA HASA UDHAIFU WA SPIKA ANNA MAKINDA NA NAIBU WAKE JOB NDUGAI AMBAO WAMEDHIHIRISHA KUWA HAWAWEZI KUSIMAMIA WALA KUONGOZA BUNGE LA VYAMA VINGI!
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

“Suala la Bunge kurushwa ‘live’ halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?” alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa

VILAZA wanashida.....! sasa hapa watu wakiwa kazini wakati wa bunge kuna weza kuliondolea SIFA bunge?,au wabunge kulala FO..FO...FOOO,Na hii ndo sifa ya WATUMWA WA MAGAMBA kuuchapa.

USHAURI:Hapo sioni kama ni kweli nia yenu ni kuleta heshima ya bunge,heshima ya bunge imetoweka kwa spika kukosa uweledi na ukiukwaji mkubwa wa haki ,maadili na nidhamu.CCM hapo mme onesha UDHAIFU mkubwa kuwa kingia kifua wabunge walioshindwa kuwa tetea wananchi wao.
 
Wanaokuwepo Makazini ni wangapi TZ? Kwanza wengi wao ni waoga wa Siasa na mabadiliko.
 
Nape anaumwa! Pia hajui anachoongea. Watu wanakuwa kazini anaelewa kuwa kazini? ofisi ngapi zina tv, au anafikiri kazi ni kupayuka umbea majukwaani kila kukicha hivyo hupati nafasi ya kuangalia tv? Dukani, sokoni, kote ni ofisini hata shoe shine ni ofisi, baa pia ni ofisi, na pia wale wa maofisi ya serikali wanatoka kazini saa tisa na nusu na bunge linaanza saa kumi na moja hadi saa mbili, muda huo huyo mpayukaji na mropokaji anakuwa majukwaani akiongea umbea wake na maneno ya kishangingi
 
Huyu Nape nafikiri watanzania hata tusihangaike kupoteza muda kumjadili. Ndugu yangu Elungata kasema watanzania wanaoangalia bunge hawazidi 5,000 hivyo haoni sababu ya bunge kurushwa live! Ndugu yangu hakufanya research na akumbuke No research no right to speak! Simple research, ofisi nyingi za umma na zile zinazohudumia jamii km mabenki, hospitali, polisi, halmashauri za wilaya na jiji,supermarkets zina television na hizo nimekutajia tu chache na wala hatusemi watu wanaokuwa majumbani. Sio kweli kwamba watanzania wote wanakuwa kazini kwa wakati mmoja! Wengine wanafanya kazi za shift, wengine wanakuwa likizo! Hivi hawa watu wanataka kutudanganya nini hapa? Labda tu nirudi kwa Kashilira, huyu anataka kukimbilia kuzima moto wakati aliacha moshi ukifuka1 Bunge kukosa ustaarabu nini chanzo? Nani alimwambia chanzo ni kurusha live? Hawa watu wanataka kutufanya watanzania wote kama watoto wao,wanachoamua tu sie tuseme ndio! Watanzania tusikubari kupelekwa pelekwa tena! Enough is enough.
 
Kweli CCM imechoka haki ya mungu,ina maana wote wana akili moja
 
CHADEMA andaeni maandamano kupinga bunge kutooneshwa live,
 
nape sababu za kashilika na zako haziendani hapo ndipo nafahumu kuwa ww ni wa propaganda tu
Nape na CCM yako tunajua kitu gani mnataka kuficha. Si kingine ni udhaifu wenu.
Wengi tunao angalia bunge hata kwa wakati mdogo tu .tuao uwezo wa kuchambua pumba ni zipi na mchele ni upi.
Wabunge wote wa ccm hawajui kujenga hoja na hilo likop dhahili. Kama kua kitu wananchi wanakiangalia ni msisimko mpya wa kizazi kipya cha wana CDM vijana wazuri wanaweza kujenga hoja na kujieleza vizuri.Wengi wetu kama hakuna wachangiaji wa cdm ni afdhari nikangalie chanel yaa kwasakwasa. CCM mnatuboa hata mfanye kitu gani watu wamewachoka sana. Hata kama mnaweza kuyafanya zaidi ya vyama vingine inafika wakati watu wanawachoa tu.Mmechokwa hata mkivuana magamba , watu wamewachoka , tena ni afadhali mkasepe kidogo labda mkirudi tena tutawkubali lakini kwa sasa hakuna mtu ana taiumu na nyie
 
hao wasioenda kazini au maofisini unafikiri huwa wanazubaa ndani kuangalia bunge?kwa taarifa asilimia 80 ya nyumba mda huu ziko empty,au wapo mahousgal au wamama wa nyumbani na wako busy wanafanya usafi,kupiga deki kuosha vyombo,kufua,kuenda sokoni,kuandaa mlo wa mchana etc.
Wanaongaliaga TV mida kama hii hawazidi 5000 nchi nzima.

Bado hiyo sio sababu ya kutokuonesha Bunge live,mbona mnaturudisha nyuma?
 
bank kuna TV, hospital kuna Tv na maofisi kibao yana TV na asilimia kubwa ya wanafunzi wa vyuo wana TV sasa. Hii hoja ya nape inataka tuamin TV zipo sebuleni tu, umbo la kiutuzima lakin akil ya kitoto..
 
Nape Nnauye ameunga mkono mpango wa bunge kutoonesha moja kwa moja mijadala ya kwakuwa muda wa matangazo watu wanakuwa kazini. kwa maana hiyo, Nape anataka kusema matangazo yote ya Televisheni na hata Redio yasiende hewani wakati wa kazi? sikujua kama huyu jamaa mweupe kiasi kichwani kwake, hata propaganda sivyo hivyo
 
Back
Top Bottom