Bunge Lisirushe Matangazo yake 'LIVE' - Nape

Bunge Lisirushe Matangazo yake 'LIVE' - Nape

Hivi jamani hata hamuwezi kutumia akili ndogo yenu hata 1/25 tu na kubaini kuwa maamuzi yote ya ovyo bungeni 99.9% ni maamuzi na maazimio ya Secretariati ya CCM?.CCM imebaini imepwaya sana na hasa kwenye Bunge ccm imedorora sana na kwa akili finyu zao wanakurupuka na hoja dhaifu sana.Hoja hii ni sawa na ile ya Makamba Sr, ya kuzuia Mchakato majimboni ambapo ccm ilizuia wagombea wake wasishiriki kwenye mjadala na mdahalo wa wagombea.Pia CCM ina maazimio ya kuzuia magazeti ya binafsi yenye mtizamo chanya na wananchi kusomwa kwa ufupi na mapitio kwenye radio na TV ya serikali na washirika wao kama RFA,StarTV,au kusoma habari nyepesi sana zisizo front page.Kwa hakika ccm ina jichimbia kaburi na serikali yake.ALUTA CONTINUA
 
.."Suala la Bunge kurushwa ‘live' halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?" alihoji Nape...
Inashangaza sana! Halafu mtu kama huyo ndio anapewa wazifa mkubwa tu katika chama kinacho tawala! Wakati mwingine mpaka ukisikia kauli zao unapata hisia kama vile wanatudharau sana watanzania.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

"Suala la Bunge kurushwa ‘live' halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?" alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa
alafu baadae mje kutuambia kwamba chadema wameingia bungeni na mabomu ya alshababu. huo ujinga hakuna mtu ataukubali isipokuwa baadhi tu, ya magamba
 
Sababu za kijinga kabisa mara zote hutolewa na Katibu Mwenezi wa CCM! kwa taarifa yako wewe NEpi, Sehemu za mapokezi katika maofisi mengi wameweka TV, Mabenki karibu zote wameweka TV kwaajili ya Wateja wao, Mahospitali kibao wameweka TV...Dunia imebadilika ILA CCM bado iko karne nyingi nyuma...
Mnapo lala sisi tulisha amkia hapo long time...I wish mtekeleze mlichokipanga ili mshuhudia kimbunga cha NGUVU ya Umma...
 
hao wasioenda kazini au maofisini unafikiri huwa wanazubaa ndani kuangalia bunge?kwa taarifa asilimia 80 ya nyumba mda huu ziko empty,au wapo mahousgal au wamama wa nyumbani na wako busy wanafanya usafi,kupiga deki kuosha vyombo,kufua,kuenda sokoni,kuandaa mlo wa mchana etc.
Wanaongaliaga TV mida kama hii hawazidi 5000 nchi nzima.
Kama ishu ni kwamba muda hakuna watazamaji au wanaotazama hawazidi 5000 nchi nzima, kuna haja gani gani basi ya kuzuia matangazo!!!! kitu hakitazamwi , sasa unaedit nini???? tafuteni maneno ingine...
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

"Suala la Bunge kurushwa ‘live' halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?" alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa

Mkuu Nape, Sio watu wote wamafanya kazi machana wengine tunafanya kazi kwa Shift , na wengine tunafanya kazi mahotelini ambako Luninga upo masaa24, na wengine tupo kwenye Reserch kuangalia Jinsi gani nchi yetu upinzani unavyofanya kazi na kuangalia kazi za bunge zinavyoendesha ni wani ya kesi study, Pili wananchi wanataka kujua jinsi Mbunge wao anavyobehave Bungeni . So suala la Kutokuonyesha Bunge live ni kuwanyima wananchi haki yao ya msingi.
 
Nape,ccm sii mlisema hamuitaji kura 400,000 za wafanyakazi waalimu?sasa eti mnataka wawaone kwenye tv for what?
 
Hii ni kuthibitisha kwamba uamuzi wa kutaka bunge lisionyeshwe live umefanywa na ccm na katibu wa bunge ndugu Kashilila ameutangazia umma maamuzi ya ccm kwa mgongo wa ofisi ya bunge.
Nape Nnauye anachekesha sana tena huyu bwana mdogo ni wa kuhurumiwa. Yani hajui kwamba kuna watu wengi sana wanafuatilia bunge? ni ukweli kwamba wananchi wengi wanafuatilia bunge na ndio maana wamekuwa mstari wa mbele kukosoa mwenendo mbaya wa uendeshaji wa vikao vya bunge hasa kwa vitendo vya spika na naibu wake kusigina kanuni kukipendelea chama chao.

Sio Nape Nnauye ni Nape Mwandosya. wewe huoni sura alivyofanana na Mwandosya? Mzee Nnauye hawezi kuzaa kilaza kiasi hicho.
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

“Suala la Bunge kurushwa ‘live’ halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?” alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa

Kutokana na fikra finyu za huyu Nepi basi vipindi vyote vya redio na runinga/television visitishwe muda wa kazi (Kuanzia saa 8 asubuhi mpaka saa 11jioni) ndipo vifunguliwe kwa sababu watu wanakuwa maofisini. Kwa kweli kuwa mshabiki wa CCM tu peke yake ni u-taahira.
 
Hana ubongo ila silicone!! Kwa hoja hiyo ni sawa na kupendekeza Tv station na radio zifunge matangazo kwa muda huo ambao yeye anadhani watu watakuwa makazini au lunch! Anaishi kwenye dunia gani huyu? Ni mambo mangapi ya kitaifa hufanywa mchana tena siku ya kazi na hao hao magamba wenzake na kurushwa live kwenye media?au ni pale tu uozo wao unapodhihirika ndipo huitwa mchana au saa za kazi? Wasifunike matatizo!ni vyema wakaji tathmini na kujirekebisha,wabunge wa upinzani wanapata umaarufu kutokana na hoja zao zenye maslahi mapana kwa taifa,nao kina nape wameshindwa vipi kutafuta umaarufu kwa hoja? Huku ni kujimaliza kisiasa,mkuu wenu jk alipowataka mutoke maofisini na kwenda kuonana na wananchi hakuwa na lengo jingine bali kuwajengea umaarufu nyie na chama chenu kupitia hoja,sasa nyie mnataka mjifiche haitasaidia chochote,tunataka tumwone mbunge wa chadema (walengwa)akitafuta umaarufu bungeni kwa matusi,au kwa kushabikia hoja muflisi,au kwa kutoa hoja isiyo na maana kisha sisi wananchi tutamhukumu,ila Tumwone kwanz sisi wenyewe na sio kupitia gazeti la Uhuru&mzalendo, hakika ule mwisho u karibu.
 
Huyu jamaa sijui kajitoa akili anaeitwa nape kwa hiyo wakati huu wa digitali anahamasha turudi analojia kweli tcra mna kazi nchi hii.
 
Matembezi ya mshikamano yanaitwa saa ngapi?Na hao wanaohudhuria wanakuwa wapo kazini au usingizini?
Kesi ya panya huwezi kumpa paka akaihukumu,kwani ni rahisi kuwa mboga wakati wa kwenda kusikiliza kesi.Pole Nnape.
 
Mambo yote yanayofanywa kwa kificho ficho mara nyingi ni ya kishetani. Bunge kutoonyeshwa live ni jambo la kificho na kuna namna mbaya ambayo inafichwa wananchi walipa kodi wasiweze kuona. Bunge sio mali ya KAshillila, nape, makinda, ndugai na familia yao bali ni mali ya watanzania wote wanaolipa kodi na wasiolipa kodi. Tbc nayo ni mali ya watanzania.
 
hao wasioenda kazini au maofisini unafikiri huwa wanazubaa ndani kuangalia bunge?kwa taarifa asilimia 80 ya nyumba mda huu ziko empty,au wapo mahousgal au wamama wa nyumbani na wako busy wanafanya usafi,kupiga deki kuosha vyombo,kufua,kuenda sokoni,kuandaa mlo wa mchana etc. Wanaongaliaga TV mida kama hii hawazidi 5000 nchi nzima.
Angalia Mungu wangu..alafu mseme mnataka kuifikia Kenya? watu dizaini kama hii ndio wanawarudisha nyuma watanzania....aisee watz mna kazi sana.....
 
aache mawazo ya kizamani huyo nape, wazee wa ccm ndiyo wanao ogopa mabadiliko
 
watu wote wanaoshika madaraka wakati huu ni wale wenye mawazo ya kizamani kama ya nape, wazee jamani waachieni vijana ngazi tuone mabadiliko
 
Kama ishu ni kwamba muda hakuna watazamaji au wanaotazama hawazidi 5000 nchi nzima, kuna haja gani gani basi ya kuzuia matangazo!!!! kitu hakitazamwi , sasa unaedit nini???? tafuteni maneno ingine...
Yaani Mkuu hiilo ni swali ambalo hawataliweza kulijibu.. Ila moto wameuona.. Maana watanzania wengi wamekuja juu na wameonyesha kabisa hawatakubaliana na ujinga wa kipumbavu kama huo..
 
Wangapi wameajiriwa na wanakuwa maofisini? Ofisi nyingi sanasana kwenye mabenki na sehemu za kusubiria huduma kuna TV zimewekwa ili watu wapate habari..hoja ya Nape haina mashiko
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, amesema kuwa jambo lolote ambalo linaleta heshima kwa Bunge analiunga mkono.

“Suala la Bunge kurushwa ‘live’ halirushwi kwa wakati ambao watu wanafuatilia kwani wakati wa asubuhi watu wanakuwa maofisini, wakati wa mchana wao wanakuwa wako mapumziko wanakula na Bunge nalo linakuwa mapumziko, sasa wanaangalia saa ngapi?” alihoji Nape.
Alisema hawezi kupinga suala ambalo linaonekana lina faida na kuleta heshima kwa Bunge hivyo anaafiki uamuzi huo.

Source:Nipashe Ijumaa
angalia msiwe mnawalisha watu maneno hapa jf!!!

Kama kweli Katibu Mwenezi wa chama tawala ndiye kayasema haya basi:
Nape = Juliana Shonza

Back
Top Bottom