Sijawahi kuandamana miaka ya hivi karibuni lakini yakiitishwa maandamano ya kupinga hii hoja mimi Kimbunga nitashika bango na kuwa mstari wa mbele. Hawa wabunge wetu wamepatwa na nini? Karne hii ya utandawazi, uwazi na uhuru wa kupata habari wao wanataka kutunyima kujua wanatuwakilishaje? Hivi wamesahau kwamba sisi ndio tumewatuma na tunatakiwa tujue wanatuwakulisha vipi? Wanataka kufanya siri?
Ama kweli madaraka kitu kibaya sana. Mtu akiitwa mheshimiwa basi anadhani anaweza kufanya analotaka? Mimi binafsi nataka tuendelee kupata habari za kibunge LIVE bila Chenga. Kama hawatimizi wajibu ipasavyo tuwaone wasitake kujificha.
.......