Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Kwa mwenendo wa utawala na uonogozi wa nchi hii usiokuwa na chembe ya ufanisi hata kidogo viongozi wa mihili ya Bunge na Serikali ndio maaduai wakubwa wa wananchi.Awali tuliamini kuwa maadui wakubwa ni umaskini,maradhi na ujinga laikini wakati huu tumeongeza na viongozi ni tatizo kubwa la maendeleo yetu.Kwa matukio mengi yasiyo na idadi hasa katika muhimili wa Serikali ambayo msimamizi wake ni Raisi na Bunge ambalo ni Spika na Katibu wake ni jambo la kusikitisha sana.Bunge limekuwa chpi ya ndani ya Serikali inayovaliwa kwa ajili ya kusitiri utupu na uchi wa Serikaali na wakati huo Serikali kuendelea kufurahia udhaifu wa Bunge lisilo wajibika.Pengine ni kuanza kuhoji kuna haja gani ya kuwa na bunge kwa kuendeshwa kwa gharama kubwa lisilo na tija?.

Mkuu hilo liko wazi mpaka sasa Tanzania haina Serikali wala Bunge, Watanzania mpaka sasa tunajiongoza wenyewe kwa asili yetu tu
 
Mh.Raisi ni ushauri wangu kwako usikubali kila kitu kinachopendekezwa bali tumia madaraka na nafasi yako kupinga mambo mengine.Mh.kwa mtizamo wangu mimi kama mwananchi wa kawaida, nadiriki kusema awamu yako imegubikwa na matukio mengi ya kusikitisha na kufedhehesha ambayo yanafanya awamu yako kuonekana ni awamu yenye udhaifu mkubwa.Mambo na matukio ni mengi ambayo yote yameishia kuzimwa bila hata aibu.Kuna kashifa na tuhuma nyingi ambazo ama wahusika walitakiwa kuchukuliwa hatua au hata kufanyiwa uchunguzi lakini kwa masikitiko makubwa mambo yote hayo yamezimwa either na serikali yako au kupitia bunge lenye wabunge wengi wa ccm na serikali yako ikionekana kufaidika na maamuzi hayo "dhalimu" ya bunge.Sihitaji kuyaorodhesha hapa kwani yanafahamika.

Mh.Raisi, kauli iliyotolewa leo na katibu wa bunge,Dr.Thomasi Kashilila, kuwa wanakusudia kusitisha urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kupitia TV, ndio imenifanya niandike haya nayoyaandika hapa.Mh.hata kama jambo hili liko nje ya ofisi yako,bado naamini unaweza kutumia nafasi yako kama raisi kufutilia mbali jambo hili.Hakika hili likitokea, katika awamu yako hii, basi ujue unazidi kujiongezea rekodi ya mambo ya kusikitisha na kufedhehesha chini ya uongozi wako.Hii itakuwa ni aibu ya mwaka na isiyoweza kuwa na "justification" ya aina yoyote mbele ya umma wa watanzania.

Mwisho,mh.unataka watanzania wakukumbuke kwa namna gani kama utaruhusu mambo kama haya yatokee?

Mh.hamna kitu kibaya kwa kiongozi kuwa na historia isiyoridhisha.Histori hii itasomwa hata na vizazi vijavyo.

Chukua hatua sasa!
Salary Slip, mawazo yako uliyompa Rais ni yenye hekima kubwa,lakini si rahisi kupokelewa mpaka ungemalizia kwa kuwatukana chadema, kungekuwa na tusi kwa chadema si ajabu ungeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa fulani
 
Hapo inaonyesha ni jinsi gani bunge letu linavyoendeshwa kimabavu. Nia yao ni kuwa wabnafutata yale yanasomwa na wabunge wa upinzani ambayo yanakosoa serikali lakini si dawa watu wataendelea kupaza sauti zao. Yaliyotokea Mtwwara yatasambaa sehemu kubwa ya nchi hii:target:
 
waache mambo yao wanaocheza mpira laivu mbele ya mraisi wao wake zao watoto zao wakitafuta umaarufu wa kuchezea timu kubwa zaidi au kuonyesha wao ni zaidi ya timu pinzani lakini wanafungwa mbele ya watu wao ili kuondoa aibu na wao wakatae kuonyweshwa live
 
Mi nafikiri serikali inazidi kujichimbia kaburi. Hayo maamuzi hayawezi kuleta tija kwao. Huyo dr anaesema hayo, hana tofauti na mtoto wa form two!!! Huu ndio udhibitisho kuwa "akili ndogo inaongoza akili kubwa"
 
waache mambo yao wanaocheza mpira laivu mbele ya mraisi wao wake zao watoto zao wakitafuta umaarufu wa kuchezea timu kubwa zaidi au kuonyesha wao ni zaidi ya timu pinzani lakini wanafungwa mbele ya watu wao ili kuondoa aibu na wao wakatae kuonyweshwa live
 
siku hizi katibu wa bunge ana nguvu ya kuwaburuza wabunge .....yeye si kazi yake ni kuwalipa posho tu.......spika ndio alitakiwa kuwaongelea wabunge!!!
 
hawana lolote hawa,wanaogopa kuona jinc watu wanavyoyaelewa mambo yao ya kipuuzi tu,nyinyiem mbwisiiiii
 
Ni mfumo wa digital,
kwa kila msitaarabu hawezi kuwaza upuuzi huu,
hapa ndipo tunaweza kutofautisha akti ya kiongozi na mtawala
 
Serikali ya ccm inacheza na muda "huwezi kuzuia balehe muda ukifika" kipindi cha digitali mnataka tuangalie recorded???
 
Kulikuwa na madai kwamba wanaofanya fujo Bungeni ni wapinzani na kukawa na jaribio la kuwaadhibu. Sasa, kwa nini Serikali ya ccm inawasaidia hao wapinzani wanaofanya fujo? Si wawaache na fujo zao zionekane na wananchi ili wawanyime kura 2015? Au ccm na serikali yake wamezuia fujo za wapinzani (chadema) zisionekane ktk TV kwa sababu wangependa wapinzani washinde 2015? Very very interesting.

Pili, Hapo ndipo JF itakapopata umaarufu mara 10 (take it from me) kwa kuwa hayo yanayoondolewa Bungeni (edited ktk TV) yatakuwepo JF. Napendekeza Chadema waweke mtu Dodoma (Afisa habari) ili awajuze wanajf na watz wakati huo.

NB. Hapa sipendekezi kwamba juhudi za kupinga msimamo huo ziachwe - hapana. Lazima tupambane kupatikana kwa haki ya habari live kupitia Tv.
 
Hivi hawa watu wana akili timamu kweli?!Kutokurusha live itawasaidia nini?!Au wanaona aibu?
 
Kwenye Maboresho ya Serikali za Mitaa, wananchi wanasikiliza Mijadala yote ya Mabaraza ya Madiwani bila kificho na wengine wanawekewa vipaaza sauti nje ya kumbi za mikutano hiyo. Iweje utawala Bora usiwepo kwa Bunge ambalo linawakilisha watanzania wote kwa ujumla? Huu ni ukiukaji wa wazi wa Utawala Bora kwa chombo kinachojiita eti ni Mhimili!
 
Mkuu Kiranga kinachofanywa na serikali ya CCM ni sawa na kuziba ndoo inayovuja ilhali maji chanzo cha maji kingali wazi, matokeo yake maji yatajaa kwenye ndoo na yatavuja kutoka kinywani mwa ndoo.
Ni dhahiri CCM wameishiwa mbinu za kuongoza, bora tuanze kuipa buriani mapeeeeeeeeema

Umetaja sana CCM kama hili ni tatizo linalohusu jando la CCM pekee.

Kwa faid ya taifa.

Wewe CAHDEMA?

Asante sana kwa maneno yako yakinifu.
 
siku hizi katibu wa bunge ana nguvu ya kuwaburuza wabunge .....yeye si kazi yake ni kuwalipa posho tu.......spika ndio alitakiwa kuwaongelea wabunge!!!

Haikuwahi kutokea katika historia ya bunge la Tanzania, kwa katibu wake kuingilia kazi za Spika kiasi hiki. Kashilila amekuwa na kimbelembele cha ajabu na kwa kiasi kikubwa anaonesha ni jinsi gani Spika ni dhaifu.
 
ILI kukomesha vurugu na wabunge wanaotafuta umaarufu wa bei chee, Bunge limeanza mchakato wa kusitisha matangazo ya vikao vyake kurushwa moja kwa moja na televisheni, kama ilivyo sasa.

Badala yake linatarajia kuanzisha chaneli yake, itakayorusha yaliyojiri kwenye vikao hivyo, baada ya kuhaririwa. Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, alisema hayo jana alipokutana waandishi wa habari Dar es Salaam, kuzungumzia yaliyojiri katika mkutano wa 10 wa Bunge, uliomalizika hivi karibuni. Alisema uamuzi wa kutorusha matangazo hayo moja kwa moja, unatokana na hali halisi ya vurugu zinazotokea ndani ya Bunge.

“Bunge sasa limekuwa kama ukumbi wa siasa, kanuni hazifuatwi, kila mtu anasimama kivyake na kutaka kuzungumza ilimradi tu aonekane kwa wananchi kuwa naye yumo. “Hali hii haileti picha nzuri hata kidogo, sasa tumependekeza kutokurushwa moja kwa moja kwa vikao hivi vya Bunge,” alisema Dk Kashililah. Alitoa mfano:

“Sote tunaona yanayojiri kila siku bungeni…mbunge anasimama na kutamka kuhusu utaratibu, mwongozo wa Spika, hakuna kitu kama hicho huku kote ni kuvunja kanuni na kanuni hizi jamani ziko wazi kabisa, lazima Bunge liendeshwe kwa utaratibu, pale si klabuni wala sokoni.”

Alisema kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Bunge, tayari wameanza kuwasiliana na Tume ya Mawasiliano (TCRA) na Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC), ili kuweka utaratibu mzuri wa kurusha matangazo hayo, na kupatiwa chaneli yao.

“Tunachotaka hata kama hawa TBC wataendelea kurusha matangazo, basi kuwe na utaratibu mzuri wa udhibiti wa matukio ndani ya Bunge. Hili si jambo geni, hata nchi nyingi za wenzetu wanafanya hivi,” alisema.

Alisema katika hali halisi, mambo mengi yanayofanyika ndani ya Bunge hilo kwa upande wa habari, ni kosa, ikiwemo upigaji picha wa wabunge ambao hawazungumzi.

“Katika Sheria za Mabunge ya Jumuiya ya Madola, kumpiga picha mbunge asiyezungumza ni kosa, hata kama amelala kwani nani kawaambia kulala ni kosa?” Alihoji.

Makinda Dk Kashililah alisema Bunge linatarajia kupeleka kwa mamlaka husika, majina ya wale wote waliotuma ujumbe mfupi na kupiga simu za matusi kwa Spika Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai, kwa kuwa tayari majina ya wamiliki wa namba hizo yamepatikana.

“Nawahakikishieni wale wote waliotuma matusi yao kwenye simu ya mheshimiwa, majina yao tunayo, tutayawasilisha kwenye vyombo husika na lazima wataitwa kuhojiwa,” alisisitiza.

Alisema kuhusu hoja ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, kuhusu masuala ya elimu, uamuzi wa kuiondoa kwenye ratiba haukufanywa kiholela kama inavyodaiwa, bali ilikubaliwa ndani ya Kamati ya Bunge ya Uongozi, ambayo wajumbe wake pia wamo viongozi kutoka vyama vya upinzani.

Hata hivyo, alibainisha kuwa hoja hiyo itawasilishwa katika Mkutano ujao wa Bunge na hoja nyingine tisa ambazo hazijawasilishwa, wabunge wenye hoja hizo wametakiwa kutoa taarifa ya kuomba ziwasilishwe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen-Kijo Bisimba, akitoa tathimini ya mwenendo wa Mkutano uliopita wa Bunge jana, alisema ipo haja ya wabunge kujiangalia kwa karibu katika uwezo na utayari wao kujadili masuala ya maslahi ya taifa, bila kuingiza ushabiki na maslahi binafsi.

Pia walitaka Spika wa Bunge kutumia nafasi yake kuelekeza Bunge, ili lifanye kazi zake vizuri zaidi.

Imeandikwa na Halima Mlacha na Lucy Lyatuu.

Source: Habari leo
 
vyombo vya habari havijakatazwa kuripoti na Wala hajasema Bunge halitaonyeswa kabisa alichosema halitakuwa LIVE tena litakuwa recorded na baadaye kurushwa baada ya kufanyiwa editing kama kutukakuwa na vurugu zitaondolewa kwanza.

Kufanyia editing mkutano wa bunge na kurusha uyatakayo ni ubakaji mkubwa wa demokrasia, enzi za kumsifu mfalme kuwa amevaa nguo ilihali yu uchi zimepita, katibu wa bunge anaturudisha stone age period na enzi za ujima.
 
Natabiri vidosho wengi kwenda jela kuanzia mwezi march mpaka Julai


weee kuku kweli, weka namba yako nikutukane kama unanipata.... mfano line imeshajiliwa shinyanga, ameishi mbeya na sasa yupo dar es salaam. kinondoni, kijitonyama, kwa arimaua kisiwani utampata mtu huyu.....

Weka hapa no ya kashilila uone adabu, kwa spika na naibu nimetupia tano tano.
 
Hii ni habari njema kwetu wenye magazeti. Tehe tehe tehe!


Manyerere
Manyerere, angalieni tu msije kujikuta kila siku mnaambiwa mkanushe habari na kuomba radhi la sivyo mtapelekwa mahakamani. Kisa, wananchi hawakuwa LAIVU kwa hiyo hakuna ushahidi kwamba mbunge fulani alisinzia au aliongea pumba!
 
Back
Top Bottom