Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Tatizo haya watu wamelewa madaraka. Wamesahau kuwa ajira wenye kuwapa hiyo ajira ni sisi wananchi na lazima tuone nini wanafanya. Hata huyo anaevunja sheria tunataka kumwona pale anapovunja sheria. Hoja mbovu kabisa haya m..kenge ni kuyatoa tu 2015.
 
​Katibu wa bunge si karani tu! Sasa hata karani amepewa meno TZ, ajabu kweli kweli!?
 
[QUOTE=wikolo;5688615]Hili ni tatizo la akili ndogo kuongoza akili kubwa. Huu ni ulevi wa madaraka uliopitiliza.[/QUOTE]

Mia! uko sawa.Hivi katika kizazi hiki cha maendeleo ya teknolojia na kijamii kuna ubongo unaoweza kuamua hili la kutokuonyesha vipindi vya bunge......nimekumbuka ndio maana walikatazwa kushiriki kipindi cha mchakato wa mahojiano ya wagombea ubunge majimboni kilichoonyeshwa live enzi za mzee wetu Tido ,huu ni mwendelezo tu!:majani7:
 
Yaani Tanzania ni nchi ya komedi mwanzo mwisho, halafu eti wanasema ni marufuku kupiga picha ya mbunge akiwa amelala bungeni??????????? ina maana bunge limekuwa sehemu ya kulala? wonders will never cease wawawekee vitanda kabisa ili wauchape ucngizi, shame on them!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Dr. Kashilila hajui kuwa hilo sio suluhisho, hajui kuwa anawanyima watanzania waliowachagua wananchi wao haki ya kuangalia wabunge wao wanafanya nini.
 
Happy Valentine wana JF wote! Kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na katibu wa bunge Ndugu Thomas Kashilila akidai bunge inabidi lisirushwe live ikiwa ni mkakati wa kudhibiti fujo bungeni limeibua sura mpya. Hii ni kutokana na wananchi wengi waliotoa maoni kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kupinga hoja hiyo. Naomba nirejee kumbukumbu za bunge za wizara ya habari,vijana na michezo.Mwaka jana wizara iliomba fedha karibia billion 18.3 tsh kwa ajili ya kuboresha TBC upande wa radio na television. Waziri alipohitimisha makadirio ya budget,Spika wa bunge Mhe.Anne Makinda alisema..."Hongera kwa mipango mizuri ya serikali,sasa wananchi watakuwa wanawaona vizuri wabunge wanaoleta vurugu badala ya kuwasemea wananchi" . Kutokana na kauli ya Dr.Kashilila bila shaka inapingana na imani ya Mhe.Makinda kwamba wananchi watawapima viongozi wao "live". Je,Mhe.Makinda amebadili msimamo wake?
 
huyo amekurupuka tu,hakushirikisha akili yake wakati anaongea
 
wasalaam wakuu.hapa nipo Magu mkoa wa mwanza.watu wamekasirika sana kusikia kwenye magazeti ya leo kuwa hawataona tena bunge live na wengi wanajiuliza hili bunge limekuwepo kwa ridhaa ya nani?na pia mtu mmoja kama sipika au katibu wa bunge wanaweza kuamua tusione bunge live au kuzuia miswada kujadiliwa bungeni kwa kuamua tu wenyewe?kumbuka pia ajali mbaya ya meli zanzibar ilivyokataliwa na sipika.wakuu nawauliza hili bunge ni mali ya nani?
 
nini sisi wananchi tunaojudge, kama wanafanya vurugu wacha tuone ili tutoe hukum, nafikili dr. kashilila hajielewi, wanataka wakandamize upinzani bungen ipasavyo then kesho yake watutangaze kama wanavyotaka. mfano bunge hili lisingekua linaonekana live. uhuru na mzalendo kesho yake kwenye front page yangesomeka hivi, "LISU AMTUKANA SPIKA, ADHABU KALI KUTOLEWA," "HOJA BINAFSI ZA UPINZANI UOZO MTUPU, BUNGE LAZITUPILIA MBALI,"
 
BUNGE KUSITISHA KURUSHA VIKAO VYAKE.

BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.

Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.

Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile ya Mashirika ya umma POAC zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi juu ya hatua hiyo.

Ni udhaifu mkubwa kuliko wowote ule duniani! akli fupi haiwezi kuwa na ufumbuzi wa kudumu wa tatizo husika.
 
Kwa mwenendo wa utawala na uonogozi wa nchi hii usiokuwa na chembe ya ufanisi hata kidogo viongozi wa mihili ya Bunge na Serikali ndio maaduai wakubwa wa wananchi.Awali tuliamini kuwa maadui wakubwa ni umaskini,maradhi na ujinga laikini wakati huu tumeongeza na viongozi ni tatizo kubwa la maendeleo yetu.Kwa matukio mengi yasiyo na idadi hasa katika muhimili wa Serikali ambayo msimamizi wake ni Raisi na Bunge ambalo ni Spika na Katibu wake ni jambo la kusikitisha sana.Bunge limekuwa chpi ya ndani ya Serikali inayovaliwa kwa ajili ya kusitiri utupu na uchi wa Serikaali na wakati huo Serikali kuendelea kufurahia udhaifu wa Bunge lisilo wajibika.Pengine ni kuanza kuhoji kuna haja gani ya kuwa na bunge kwa kuendeshwa kwa gharama kubwa lisilo na tija?.
 
Tatizo lipo kwetu watawaliwa (wananchi) unadhani tungekuwa tuna tammbua haki zetu na kuzidai kwanguvu kuna mshenzi yoyote ambaye angeweza kuja na hoja ya kipuuzi namna hii? umefika wakati sasa tuwaambie imetosha.
 
Bunge ni chombo cha si serikali.Ila ni mojawapo ya mihimili mitatu ikiwa ni pamoja na baraza la mawaziri na mahakama.
Majukumu yake yameainishwa kuwa ni kutunga sheria,kusimamia serilkali,kusimamia bajeti,n.k,
Ila sasa hapa kwetu theoretically,bunge linaonekana kuwa chombo cha Chama Tawala,ambao wanaweza kujiamulia mambo kwa jinsi wanavyowaza.
 
Back
Top Bottom