Mh.Raisi ni ushauri wangu kwako usikubali kila kitu kinachopendekezwa bali tumia madaraka na nafasi yako kupinga mambo mengine.Mh.kwa mtizamo wangu mimi kama mwananchi wa kawaida, nadiriki kusema awamu yako imegubikwa na matukio mengi ya kusikitisha na kufedhehesha ambayo yanafanya awamu yako kuonekana ni awamu yenye udhaifu mkubwa.Mambo na matukio ni mengi ambayo yote yameishia kuzimwa bila hata aibu.Kuna kashifa na tuhuma nyingi ambazo ama wahusika walitakiwa kuchukuliwa hatua au hata kufanyiwa uchunguzi lakini kwa masikitiko makubwa mambo yote hayo yamezimwa either na serikali yako au kupitia bunge lenye wabunge wengi wa ccm na serikali yako ikionekana kufaidika na maamuzi hayo "dhalimu" ya bunge.Sihitaji kuyaorodhesha hapa kwani yanafahamika.
Mh.Raisi, kauli iliyotolewa leo na katibu wa bunge,Dr.Thomasi Kashilila, kuwa wanakusudia kusitisha urushaji wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kupitia TV, ndio imenifanya niandike haya nayoyaandika hapa.Mh.hata kama jambo hili liko nje ya ofisi yako,bado naamini unaweza kutumia nafasi yako kama raisi kufutilia mbali jambo hili.Hakika hili likitokea, katika awamu yako hii, basi ujue unazidi kujiongezea rekodi ya mambo ya kusikitisha na kufedhehesha chini ya uongozi wako.Hii itakuwa ni aibu ya mwaka na isiyoweza kuwa na "justification" ya aina yoyote mbele ya umma wa watanzania.
Mwisho,mh.unataka watanzania wakukumbuke kwa namna gani kama utaruhusu mambo kama haya yatokee?
Mh.hamna kitu kibaya kwa kiongozi kuwa na historia isiyoridhisha.Histori hii itasomwa hata na vizazi vijavyo.
Chukua hatua sasa!