Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

BUNGE KUSITISHA KURUSHA VIKAO VYAKE.

BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.

Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.

Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile ya Mashirika ya umma POAC zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi juu ya hatua hiyo.
Mamba anamhurumia binadamu,hii ni kali!!!!!
Spika amewataja wenye fujo kwa majina na wanatoka upinzani.Kwa mantiki ya kawaida ya kutaka mpinzani wako ajimalize kisiasa ingekuwa ni kuacha matangazo yarushwe live ili wananchi wawaone wapuuzi wa UPINZANI.
Hiki kinachotaka kufanyika ni kujaribu kulinda aibu ya CCM na serikali yake.
NI aibu na naamini JK hatakubaliana na upuuzi huu!!
 
Who is Kaishilia in dis country,sorry kaishalia,ooh kashilila???Who is who in dis beautfuly country???HAYO MAMLAKA KAYATOA WAPI?MAWAZO ALICHANGISHA WAPI??Ama kweli ya mfa maji.
 
Wajaribu kufuta kama hatujaingia barabarani na hapo ndo ukombozi utakuwa umekuja, hela na garama za tbc kutujuza yanayojiri bungeni ni hela zetu. hawa jamaa wanaona watanzania ni wajinga kwelikweli, mtu anaamka tu anasema kile anachoona ni sawa utafikiri yuko nyumbani kwake na anaongea na mkewe na watoto wake.
 
Analog kwenda digital au digital kwenda analog. Du speed and standard!
 
Nikiwa kama mwanaharakati nitaitisha maandamano ya kupinga hoja ya kufuta kurusha live vikao vya bunge.
wananchi tuna haki ya kujua kinachojadiliwa na wawakilishi wetu huko bungeni. sisi ndio tutachambua nani anaongea anavunja kanuni za bunge. hilo halitawezekana kabisa vinginevyo bunge halitaendeshwa.
NADHANI HUU NI WAKATI WA KUITOA CCM SERIKALI YAKE HATA KABLA YA 2015

CCM NI JANGA TUIOGOPE ZAIDI YA UKIMWI NA UKOMA
 
Tutaandamana mpaka kieleweke Bunge linajadili mambo yanayohusu shida za watanzania na wnaoona ni watanzania na wabunge wenyewe wanawakilisha watanzania, hapa wanataka kuficha nini? nasema watanzania tutasimama wote kuhakikisha hii kitu haipiti.
Kabisa...!Tumechoka kuvumilia sasa!
 
Jamani vigogo msituone wananchi tumekuwa vilaza kihivyo mnaongea maranda tu bila kuwaza. Acheni tusikie wabunge wetu wakivunja sheria ili tuwahukumu vema wakati wa uchaguzi. Kaka mkiona hatujawahukumu mjue hoja hiyo ilibidi mbunge avunje kanune ili kuondoa madhara ya uchache bungeni. Tendeni haki na tuacheni tuone bunge letu live. Bunge si mali ya katibu wa bunge
 
Mimi naona kuwa aliyetoa wazo hili afunguliwe shitaka la jinai kwani anavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.
Katika Ibara ya 18.Kila Mtu
(d)anayo haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhimu kwa jamii
.

JE HUYU ANAYEAMUA KUMFURAHISHA MKE WAKE KWA KUTAKA ATUKOMOE ANA UELEWA WA KUTOSHA,AU NDO WALE WALE WENYE UDAKTARI WA ZAWADI?????
VYEO VYA ZAWADI NAVYO SI VIZURI KWANI UNATAKIWA KUMFURAHISHA BWANA WAKO KILA WAKATI HATA...............
 
huwez tatua tatizo kwa kulikimbia, kuacha kurusha bunge hakutabadili hali ya mbunge kusimamia kile anachoamini, kama kuna mbunge mpumbavu tena ndio atatumia mwaya huo hata kutukana matusi ya nguoni, cha msingi kama wanafikiri sheria za sasa hazina makali kwa hao "wabunge wanasababisha vurugu" basi watunge sheria kali zaid, mama kiti kimekushinda c ujiuzulu tu???
 
Weka namba za katibu wa bunge hapa ili nguvu ya umma itoe majibu sahihi... pls aliyenazo.

naona 2015 mbali sanaaaaaaa.....
 
Kutoonyesha live ni mbinu ya kuficha maovu yao. Wanataka kuonyesha yale wanayoyapenda tu na wasioyapenda watawala yasioonekane kwa wananchi, lakini mficha maradhi kilio kitamuumbua. Binafsi naona ni ujinga wa kanga kuficha kichwa kwenye mchanga huku kiwiliwili kikiwa nje akidhani moto ukija atapona. Msuguano wowote huleta maendeleo. Anachojaribu kufanya Kashilila kuacha kuonyesha lakini hazuii msuguano wenyewe. TV sio root cause of the problem. Tatizo ni namna gani kanuni za uendeshaji wa Bunge zinafuatwa. Namna gani haki inatendeka kwa wabunge wote bila kujali vyama. Katibu wa Bunge Tomas Kashilila naye anaangukia kwenye tatizo lilelile la Anna Makinda. Ni sawa na Nurse anayeosha kidonda juujuu huku akiacha usaha unapwita ndani. Nurse wa jinsi hafai kwa kuwa kidonda hakitapona.
Kwa nini Spika anayepindisha kanuni za Bunge asionekane kupotosha jamii bali Mbunge wa Upinzani anayepinga kuonewa aonekane ni mtomvu wa nidhamu na ni mfano mbaya kwa vizazi vyetu. Maadili hayana chama tawala wala cha upinzani.
Hivi madaraka ya kuwanyima habari sahihi wananchi wa Tanzania, Katibu wa Bunge kapewa na nani?

Nimegundua kuwa Kashilila na timu yake ni moja ya tatizo katika Bunge letu. Utakumbuka wakati wa sakata la hoja ya Mnyika, Mh Tundu Lisu alipojoji uhalali wa Waziri wa maji kupewa zaidi ya dakika 15, Naibu Spika akasema ni makosa ya watendaji wa Bunge - yaani Katibu na watu wake. Kitu cha msingi hapa ni kuwa ni Kashilila na watu wake wanaosaidia kutafasiri (au kupindisha) kanuni watakavyo. Nina hakika Kama wangekuwa na weledi spika na kundi lake wasingethubutu kucheea kanuni watakavyo na matokeo yake kushjindwa kuongoza kwa haki!
 
Ujue siku zote chizi akigundua watu wanamuangalia ndio anazidisha vibweka,sasa tuone off camera kama kuna chizi atachafua hali ya hewa ya bunge letu.
 
Weka namba za katibu wa bunge hapa ili nguvu ya umma itoe majibu sahihi... pls aliyenazo.

naona 2015 mbali sanaaaaaaa.....
Natabiri vidosho wengi kwenda jela kuanzia mwezi march mpaka Julai

 
yaani dunia ya sasa bado hao tuliowapigia kura hawataki tuwaone wakifanya kila ambacho tumewatuma.. huu .ni ubinafsi mkubwa ...
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wanasema Utawala wa Democrasia una maneno mawil muhim na yanayotegemeana sana,
Nayo ni UWAZ na UKWELI..

Penye uwaz pana ukweli na penye ukwel pana uwazi. Kutizama/kusikiliza Bunge Live panachukua neno moja kwanza yan UWAZ, na badae hilo la pili.

Kwahiyo Bunge kutokuonyeshwa Live ni kuundoa UWAZ then UKWEL hautakuwepo automatical. Serikal itapata tabu sana kuleta mrejesho kwa Jamii, mana watu wanasema KUONA ni KUAMIN, kwahyo kama hukuona utaamin kwa shda ama hutoamin kabisa.

Ingawa Makinda na Ndugai ni tatizo, Mi nadhan hil litakuwa ni kubwa zaid kwa wanakijan...
 
Back
Top Bottom