Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Wananchi tunauwezo wa kumfanya katibu wa bunge akashindwa kuratibu shughuli za bunge na hata spika akashindwa kuendesha bunge kama wanadhani wanauwezo wa kuamua kufanya watakacho wakumbuke bunge letu sio taasisi walizozianzisha kwa hiyo wachunge maamuzi yao
 
Kwa kuzuia live coverage serikali inataka kuficha nini, kama mbunge anavunja kanuni kwanini asichukuliwe hatua hadi waamue kuzima TV? Kashilila na spika wanataka kutuambia bunge lisipoonyeshwa live kanuni hazitavunjwa? kama ni utovu wa nidhamu ama aibu waache aibu hiyo ionekane kwa wapiga kura wao ili wamwadhibu kwa kumnyima kura next time.

Mimi nafikiri bunge likizuia kuonyesha live kwa wenyewe (wananchi) Chadema wasiishie kushitaki kwa wananchi tu, waende mahakamani kwa sababu kusikiliza na kuona mijadala ya bunge ni haki ya msingi ya mwananchi ambaye ndiye mpiga kura si haki ya Makinda, Ndugai na Kashililah pekee yao.
 
Duuh ama kweli hata madaktari siku hizi uwezo wa kufikiri umepungua. Ni kweli unaweza kutoa kauli ya namna hiyo ikawa ndo suluhisho? Naogopa sana
 
Hawezi kuyatatua ameyatengeneza makusudi wagawe halafu watawale kwake hiyo ndio raha ya uongozi wananchi wataendelea kuparurana yeye anapanda ndege anaenda zake kubembea
 
"BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii."

Magambas bwana eti watu wanatafuta umaarufu! Sasa hao wabunge wachache wanaojitokeza kutetea maslahi ya wananchi walio wengi waogope eti ukifanya hivyo utabatizwa na magamba kuwa unatafuta umaarufu? Hata hivyo ni mwanasiasa gani asiyetafuta umaarufu - alimradi umaarufu huo unawaletea tija wananchi. Huyu Kashihillah naye atakuwa amepata uDr wa online nini?
 
Tanzania ya sasa sio ya zaman tena watu wanatambua haki na wajibu wao. Wabunge wa CCM wakipitisha TUUU, CCM kwishnei wanatoa daraja la kutosha kwa wapinzan kuzid kufunua umbumbumbu wa viongoz na njama zao za kuficha ujinga wao. Au wale wenye vitambi vikubwa wanaosinzia wanataka waende na magodoro kabisa.
 
Huu utakuwa ni kuKenge Ukiwa First Degree... Sisi wananchi tunaweza kuchambua pumba na mchele, only wenye kuongea pumba ndio wanao/watakao athirika kwa matangazo ya moja kwa moja (live). Watajitahidi sana kuficha mapungufu ya kiti cha spika na naibu wake Ila mwisho wa siku wata realise kuwa LAKUVUNDA siku zote HALINA MANUKATO/UBANI! CCM imeoza, CCM inaugua mkanda wa JESHI! hata wakivaa mavazi ya hariri uvundo utawaumbua tu...Sad! mapendekezo kama haya huwa yanaongeza hasira kwa Wananchi...

Wasiache kurusha live tu, waache hata na kufanya vikao vyenyewe.
 
wanabodi JF,
Kwa mara nyingine jioni hii katika taarifa ya habari kwenye Luninga kadhaa,amejitokeza bwana kashilila ambaye ni katibu wa bunge,ametoa tamko kwamba wabunge wa ccm,wanakusudia kupitisha hoja ya kuzuia matangazo ya moja kwa moja kutoka kwenye vikao vya bunge kupitia luninga..
Hii ni kwa kile alichokiita kuwa ni kuzuia vioja vya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya wabunge wakati wa kuwakilisha hoja zao au kuomba miongozo ya spika jambo ambalo kwake yeye amesema linalifedhehesha bunge kwa wananchi.

MY TAKE:
hivi serikali yetu inashindwa kuiga mfano wa wenzetu KENYA ambao pamoja na kuhitilafiana kiitikadi na hata sometimes kikabila,lakini wamefanya kile ambacho hata serikali ya ccm ilikiogopa kupitia mgombea wake ambaye kwa wakati huo aliukacha mdahalo wa wagombea urais na hata ile midahalo majimboni ilipolazimishwa na uongozi wa TBC,ulimponza Bw Tido mhando,na hatimae kufuzkuzwa kazi kinyemela kabla ya mkataba wake kuisha.

Leo hii nchi imegubikwa na kashfa kila kona,ambazo wananchi tulitarajia kuona serikali kupitia mhimili wake ambao ni bunge lake,ikiacha demokrasia ikitumika ili kuisimamia serikali katika kuhakikisha hoja muhimu na zenye maslahi kwa wananchi na raslimali zetu zikijadiliwa ili kuliokoa taifa huko shimoni tunakopelekwa na mafisadi zikijadiliwa kwa kina na kwa usawa bila kusukumwa na itikadi za vyama,bali na uzalendo kwa maslahi ya taifa letu kwa sasa na vizazi vijavyo.

Hali imekuwa kinyume na matarajio ya wananchi.Bunge letu limegeuka kuwa kijiwe cha wana CCM kwa kutumia wingi wao ndani ya bunge na kupindisha kanuni kwa maslahi yao na chama chao na badala ya kuisimamia serikali,bunge limegeuka mbeleko ya serikali katika kuibeba kwa madhila yote tunayoyaona
Yakifanyika bila serikali kuchukua hatua madhubuti nitaorodhesha machache na yeyote humu anaweza kuongezea
.
*Tatizo la mgogoro wa Gesi asiiia kule mtwara

*Tatizo la ukandamizaji wa mhimili wa vyombo vya habari vinavyoikosoa serikali

*Tatizo la mitaala mibovu katika sekta ya elimu na maslahi duni kwa walimu.

*Tatizo la udini linalochipuka kwa kasi.

*mabilioni yanayosadikia kufichwa uswisi.

*spika kuvunja kamati muhimu za bunge kinyemela wakati ambao ndio zilihtajika kufanya kazi

*mauaji ya raia yanayofanywa na polisi bila hatua madhubuti kuchukuliwa na serikali,

*janga la ujambazi linaloongezeka kila kukicha nchini na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

*Ujangili wa maliasili zetu hasa meno ya tembo unaofanywa na waandamizi wa serkali.

*kero ya uhaba wa maji na ukame unaolikabili taifa

*Wananchi kuanza kutokuwa na imani na jeshi letu la polisi,

*ombaomba na watoto wa mitaani wanaoongezeka mijini kila kukicha. Nk.....

HALAFU BUNGE LINATAKA KUZUIA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA,jE?
Hii ni nini kama sio kutaka kuficha uozo mbalimbali utakaoibuliwa na wapinzani wachache ndani ya bunge usionekane kwa wananchi,ili kuilinda CCM kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,ambao uko mbioni kufanyika.na pia hata uchaguzi mkuu ujao.?

Je hii si aibu kwa wafadhili na mataifa tunayoita wahisani kwa kutaka wasijuwe jinsi misaada yao inavyotumika ndivyo sivyo?

Hivi kama hilo litafanyika,Rais wetu bado ataendelea kusafiri ughaibuni akiwa kifua mbele,au ndio mwanzo wa kutaka kuwekewa vikwazo kama kwa mu***e

Jamani narudia hii ni aibu kubwa kwa taifa linalojiita la kidemokrasia mbele ya jamii za kimataifa wakati,hapa ndani ya mjengo tukitaka hata raia wasijuwe kama mnafanya kile walichowachagua ili mkawawakilishe kwayo

Inauma sana sana-tena sana,ebu kama taifa tujiridi na viongozi wetu mumuungamie mungu mwenyezi.
 
Makinda na genge lake wanaturudisha miaka ileeeee ya zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM
 
He hili bunge ni la wana ccm tu wanapitisha si kwa sheria za nchi bali kwa matakwa yao. Ngoja tulete wabunge sawa mtaona chamoto
 
Duuh ama kweli hata madaktari siku hizi uwezo wa kufikiri umepungua. Ni kweli unaweza kutoa kauli ya namna hiyo ikawa ndo suluhisho? Naogopa sana
maajabu...haya huyakuti popote duniani....only tz...
 
Unataka wafanyaje kama maji yapo shingoni sio wamepeleka vilaza bungeni hawajui kitu zaidi ya kusifiana. Subiri watatunga misheria kibao ya kuwalinda. Shauri yao
 
He hili bunge ni la wana ccm tu wanapitisha si kwa sheria za nchi bali kwa matakwa yao. Ngoja tulete wabunge sawa mtaona chamoto
Ni kweli mkuu,kwani sasa ndio wakati muafaka wakuwapatia elimu na au sisi wenyewe kila mmoja wetu kuelewa nini maana ya kuwa na wabunge wa kutosha wa upinzani ndani ya bunge letu,na tusifanye makosa katika uchaguzi ujao maana tunakopelekwa na watawala wetu siko kabisaa kunakostahiili....
 
wanataka tuweke kambi nje ya jengo lie au! Kujua kinachoendelea bungen ni haki ya mtanzania na nadhan huyu kashilila amelewa madaraka!
 
Wameona kila wakienda bungeni wapinzani wanawatoa jasho na kujichukulia point muhimu, so ili kuficha aibu inabidi wasitishe kurusha vipindi live, kingine ni kuficha aibu ya waziri mkubwa, uwa akibanwa maswali vizuri anabakia kutoa chozi so wanamsitiri mkuru.
Pia madamu thenkyuu veri machi na mwenzie ndungai wameona hasira za wananchi kwa madudu wanayofanya bungeni so bora wayafiche ili wananchi wasione.
Rubish kabisa wanataka kuchagulia wananchi habari wanazo zipenda wao tu?
 
Bunge halioneshwi na hakuna mtakalo fanya,lalamikeni tu usiku mtalala maisha yataendelea.
 
Makinda hawezi mambo ya standard and speed! Halafu wanampaisha mzee SAIMONI SIGISI huku wakidhani wanammaliza. Mimi ningekuwa Sita ningeshahama ccm kitambo. Nitafurahi sana wakiacha kurusha kwa sababu ni sawa na kumpiga teke chura.
uame uache ulaji.thubutuuuuuu.....
 
Back
Top Bottom