ndugu wana bodi kwa masikio yangu nilimsikia mheshimiwa spika wakati anaongelea vurugu za bungeni kuwa anaiomba serikali iiongezee fedha TBC1 ili irushe vizuri vituko vya wabunge waonwe na wapigakura wao wanayofanya huko mjengoni mara tena kaibuka katibu wa bunge ndugu T. kashilila huyu anasema vipindi vya bunge havitarushwa live funga kazi kuonesha ushabiki wa siasa hasa kwa CCM akadai wabunge wakapige kelele kama vile mwembeyanga nk. hapa ni dhahiri ujumbe umefika kwa walengwa ukija kwa AG. anakwambia yanayotokea bungeni ndo kawaida ya mfumo wa vyama vingi wananchi wazoee hivi kwa hali hii bunge kuwa kama jamhuri ya kambali madhali kila mtu ana ndevu basi mfalme tutafika????? eee chama changu tukufu CCM tuhurumieni watanzania bunge ni sehemu pekee tunayoamini inatutetea wanyonge.. nawasilisha:A S cry: