Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Huu utakuwa ni kuKenge Ukiwa First Degree... Sisi wananchi tunaweza kuchambua pumba na mchele, only wenye kuongea pumba ndio wanao/watakao athirika kwa matangazo ya moja kwa moja (live). Watajitahidi sana kuficha mapungufu ya kiti cha spika na naibu wake Ila mwisho wa siku wata realise kuwa LAKUVUNDA siku zote HALINA MANUKATO/UBANI! CCM imeoza, CCM inaugua mkanda wa JESHI! hata wakivaa mavazi ya hariri uvundo utawaumbua tu...Sad! mapendekezo kama haya huwa yanaongeza hasira kwa Wananchi...
 
Hi CHADEMA, ama mdau yeyote mwenye namba za simu (Airtel, Tigo, Voda, Zantel, TTcl) za katibu wa Bunge Ndg Thomas Kashilila atumwagie hapa kwenye jamvi tumpatie ujumbe kuwa ajenda yake hiyo haifai. Mpango huo ni kuwanyima haki watanzania kujua kile wanancho jadili wabunge wao kwa niaba yao. Kama kazi mnayofanya mmetumwa, kwa nini mfiche aliye watuma???

Mkifanya hivyo nasi tutaandamana na kualani tusiwalipe mishahara na marupurupu kibao. Tunaweza kufikia mahali tukafuta hilo Bunge tuanze upya. More plans to come! Katibu usichezee uhuru wetu!

Mwenye namba zake tafadhali atuwekee hapa, ndo dawa yao.
 
Nakubaliana na meya wa jiji la Dar kuwa kuna baadhi ya viongozi wetu wanafikiri kwa kutumia makalio. Anawezaje kutunyima sisi wapiga kura haki ya kujua kama wabunge wanasema kile tulichowatuma. Huyu mpumbavu anataka kuficha madudu yanayofanywa na baadhi ya wabunge kwa ajili ya maslahi ya vyama vyao.

Huu ni usengerema wa hali ya juu kwa kiongozi asiye na aibu kama huyu. All the worst to him!
 
Can only be done by empty headed person! Mbali na kanuni kupwaya utashi wa kutekeleza kanuni ni muhimu!.jaman mbona demokrasia inarudi nyuma kwa kasi?
 
wanaoamua mwelekeo wa nchi yoyote hapa duniani ni Wananchi wenyewe.
Wanafanya hivyo kwa kiwango chao cha werevu, maarifa, mwamko au hata ujinga walionao. hata hili litaamuliwa hivyo hivyo.
 
Aibu kwa demokrasia, aibu kwa utawala bora....aibu kwa CCM.
Ukisha ona serekali inaanza kuzuiya vyombo vya habari na kuvinyima uhuru ujue kuna udhaifu wanavunja kamati za bunge bila sababu hivi unategemea nini? Au sababu wanaona wakubwa wanaofanya ufisadi wanaumbuliwa? Tendeni tuu yanamwisho.na hapa cdm mkikubali hili nitadhiriki kusema hakuna
Upinzani makini
 
Kuna haja ya wananchi kufikiri njia ya kuwaadabisha. wanaweza wakafunga kweli hawa au mitambo ikawa inakatika anaposimama Lissu.
 
Mwenye namba ya Thomas Kashilila atuwekee hapa.
 
Kwa akili ya Ma CCM baada ya kulazimisha Vingamuzi huku wakijua wenye uwezo ni wachache sasa wanakuja na kufuta Live Coverage ya bunge na watakuwa wana edit na kutuonyesha wayatakayo wao.
Baada ya hapo watafunga forum na blog zote.
Wakishindwa internet itakuwa marufuku.
 
Hivi kuna uhusiano gani kati ya kuvunjwa kwa kanuni za BUNGE na kusitishwa kwa vipindi vya BUNGE kurushwa live kwenye Televisheni? Hivi mbunge aliyevunja kanuni kwa makusudi na bila sababu ya msingi anapata umaarufu au anajifedhehesha?
 
that's stupidity ..Ila na nyinyi humu ndani acheni hizo mambo kila kitu hadi mukihusishe na UCHADEMA na uCCM
 
that's stupidity ..Ila na nyinyi humu ndani acheni hizo mambo kila kitu hadi mukihusishe na UCHADEMA na uCCM

Mimi sipendi polarization ya vyama.

Lakini kama bunge lina majority ya wabunge wa CCM, spika na naibu wake ni wa CCM, halafu linaleta Draconian moves za kumfanya Hammurabi aonekane chamtoto, kama CHADEMA wakisema haya ni matokeo ya uongozi mbaya wa CCM utakataa vipi hilo?
 
Hawezi kupingana na teknolojia. Hivi kwa kusitisha kuonyesha vipindi vya bunge tutakuwa tunarudi nyuma au tunaenda mbele? Yaleyale ya kupandisha bei ya mafuta ya taa ili kupunguza uchakachuaji?
 
Alaaniwe yeyote yule anayechangia kuifanya nchi ishindwe kupiga hatua ili kuondokana na umaskini tulio nao!!!!!!!
 
mweeee mpaka ikifika december 2015 tayari mengi yataonekana. kama kweli havitarushwa moja kwa moja kwa sababu walizotoa basi CCM itaanguka anguko kuu.
 
Huko ni kutapa tapa tu, mwisho watatuambia kuwa kuona au kuonyesha bunge inahitaji malipo. Hii ni sawa na kuwazuia wananchi kusafiri kwa magari na kuwataka watembee kwa miguu eti kwasababu wanataka kupunguza ajali. HUU NI UPUUZI Usio na mfano
 
Back
Top Bottom