Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Bunge kusitisha kurusha 'LIVE' vikao vyake!

Kwa sababu ya serikali dhaifu ndiyo maana tunayaona haya.
 
Makinda hawezi mambo ya standard and speed! Halafu wanampaisha mzee SAIMONI SIGISI huku wakidhani wanammaliza. Mimi ningekuwa Sita ningeshahama ccm kitambo. Nitafurahi sana wakiacha kurusha kwa sababu ni sawa na kumpiga teke chura.
 
yaani hawa ni wapumbavu sana na li serikali lao..ngoja niondoke kwenye uzi huu maana ban itanihusu.
 
Makinda Mbona Kazi Unayo Mwaka Huu! Mwisho utazuia hata Bunge kuwepo...Mbona wakati wa Mwalimu Nyerere Bunge lilikuwa kali kupita hata sasa na lilikuwa la Chama kimoja..Tulikuwa tunasikia katika radio...So kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya sio issue...Issue ni kuzisimamia ipasvyo Kanuni coz msipozisimamia mkazipindisha, basi jiandaeni kuzia na magazeti kurepotu habari za bunge. Lakini pia mzuie rasio na TV zisitoe hata katika taarifa zao za harai jambo lolote linalohusu Bunge..

Source: Taarifa ya habari ya saa mbili Star TV
 
Bunge lina kanuni dhaifu kiasi cha kushindwa kudhibiti wafanya vurugu? Wakiendelea kufanya vurugu huko mafichoni watafanya nini?...litafutwa au..
 
Huu ndiyo wakati wa kuiangusha serikali dharimu na iliyojaa ushetani ya JK na waovu wenzake.
 
Dr Kashilila amenisikitisha mpaka nashangaa huu ni udokta gani usioweza kulinganisha vitu, anadai amekaa bungeni toka zamani kukiwa kuna redio tz tu iliyokua ikirusha bunge na hakukuwa na vurugu, mtu akiambiwa akae anakaa. Anaringanisha bunge la chama kimoja na bunge la vyama vingi ? Huu si uchizi jaman,hoja ya eti wabunge wanataka umaarufu ndo maana wanaleta fujo ni hoja ya kitoto kwa mtu mwenye madaraka makubwa kama katibu wa bunge. Leo ameongea pumba tupu, mara eti kuna kamati zingine zinaingilia kazi ndo maana zimefutwa kwa kua zinapoteza maana. Aseme ni kamati zipi na ziliingilia kazi zipi? Mbona mnatufanya wananchi ni wajinga jaman? Hembu oneni aibu, wewe ni dokta unajihaibisha mkuu!
 
katibu wa bunge dr kashilila atangaza kurejea mfumo wa kizamani wa kurekodi na kuedit kudhibiti mmomonyoko wa maadili.
analogy to digital na huu ujinga tutafika kweli

Asitufanye wajinga sie, Kasha tumwa na CCM kumaliza upinzani inaonekana Wassira kashindwa eti?
 
Bunge linajadili kusimamisha matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya bunge kurushwa katika televisheni kwa kile linachosema kupunguza wananchi kuona fujo zinazotokea bungeni. MAANA YAKE TUTAKUWA TUNAONA BUNGE LILILOFANYIWA EDITING.
 
bunge kusitisha kurusha vikao vyake.

Bunge linatarajia kufuta utaratibu wa kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta picha mbaya katika jamii.

Hayo yamesemwa na katibu wa bunge dk.thomas kashilila jijini dar es salaam wakati akitoa taarifa ya mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya kamati za bunge.

Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.

Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano yasiyokuwa na hoja za msingi.

Dk kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana ya kamati hizo.

Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo ile ya mashirika ya umma poac zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa baadhi ya wananchi juu ya hatua hiyo.

nilidhani ni kwa wananchi tu kumbe hadi kwenye vyombo vya utawala,kikiuka kanuni kunahusiana nini na kuonyesha bunge ilil lionekane na wananchi wote? Wamegundua kwamba upuuzi wote wanaoufanya bungeni unaonekana na wananchi,acheni wananchi waone ili waje wawahukumu kwa vitendo vyenu mnavyofanya huko bungeni,mmehajulikana kwamba hamko huko kwa maslahi ya wananchi bali kwa maslahi yenu na ya chama chenu,je chama bila wananchi kipo au mnajidanganya?
 
Tunaomba Msimamo wa CHADEMA hapa, kama vipi Bunge lisiwepo kabisa, ni Bora livunjwe, na hapa CHADEMA hawatakiwi kufanya makosa
 
Katibu wa Bunge Dr.Kashilila amesema wanaandaa utaratibu ili lisiwe likionyeshwa live badala yake litakuwa likirekodiwa na kuhaririwa,ndipo wananchi waweze kufahamu kilichoendelewa bungeni siku hiyo.source taarifa TBC1 saa 2 usiku
 
Tupaze sauti za hapana tuwaambie hawa manyamg'au hapana. Nchi inabakwa tunacheza na nyani tujiandae kuvuna Mabua.
 
Sera iliyokosa mashiko, Watanzania mnawaletea adited bunge... Karne ya kuchagua kivuli na picha imepita na nadhani bora wangeleta sera ya kukataa TV zisionyeshe mikutano ya vyama vta siasa.
Mipango yao mara nyingi inawageuka wenyewe.
 
Tweeter,Jamiiforum,Facebook kwa jumla Internet technology hawawezi izuia
Kina Zitto,JJ Mnyika watafanya kazi za updates,sound recording watatuma kama kawaida
Hii nchi sasa inaelekea kushindikana
 
Aisee. This is beyond any acceptable irrational...if at all there's...what a poor thinking. Hii hatua inapaswa kupingwa kwa nguvu za hoja zote zilizopo, ama itazidi kuugharimu sana huu mhimili, hasa viongozi wake.

Hii haiwezi kuwa namna sahihi ya kuficha udhaifu mkubwa wa serikali bungeni na uzembe wa bunge na wabunge, hasa wale wengi wa CCM!

Dkt. Thomas na wenzako, Watanzania si mabwege tena. Take it or live it, si wajinga tena. Wanajua mnachotaka kuficha. Wanajua mnaficha uchafh chini ya zulia. Nani hajui. Hata watoto wa chekechea wanajua hii move maana yake ni nini!

Naomba kumnukuu Lissu, mchague, ama bunge iwe sehemu ya mijadala ya afya au bunge lisiwepo kabisa, wananchi wajue moja.

Bunge ambalo haliwezi kufanya kazi yake kwa mujibu wa katiba, kisha linaanza kutafuta sababu kama hizi za kupuuzwa, linafunga ushahidi wa uzembe wake na ukibogoyo linaoung'ang'ania kwa faida ya CCM na serikali yake.

Dkt. Thomas, CCM imeshavunjika miguu. Kinachosubiriwa sasa hivi ni ama kuisukuma tu iangike kwa haraka, ama kuishikilia na kuisaidia ianguke polepole, huku wananchi wakiendelea kuumia. Wenye akili hawawezi kuthubutu kuitibu hiyo miguu.

Where do u stand! Ni ama unasimama pamoja na Watanzania wanaotaka kuona haki, matumaini na uwajibikaji kama moja ya misingi muhimu kwa amani na utulivu kisha maendeleo tunayoyatamani, ama unasimama kinyume nao, maana yake unasimama upande wa CCM.

Nani amewadanganya kuwa kutoonesha live vipindi vya bunge ndiyo njia itakayowapatia ushindi kwa kusimama katikati ya udhalimu na ukandamizaji. It is either u stand with the the oppressor (s) or the oppressed. Uamuzi huu unawatambulisha mko upande gani.

You are gone too...

una ccmophobia wewe. Huwezi kuandika maneno matatu bila kuitaja. Uhuni tunaoushuhudia wa watu wazima bungeni ni bora uchujwe kwanza
 
ipo siku watapiga marufuku TV stations kutorusha taarifa ya habari
 
Back
Top Bottom