Kitu kingine nimegundua humu kwenye huu uzi kuna watu hawajui tofauti kati ya Bukoba na Kagera. Eti mtu unakuta anakwambia mimi nilifika Biharamulo nimeona Bukoba bado iko chini sana. Inabidi mjue Bukoba sio Kagera yote, ni wilaya kama hizo mnazotaja Biharamulo, Ngara, Muleba, n.k sasa unapoenda Muleba ukasema uliona Bukoba haijajengeka unakuwa very wrong. Bukoba zipo mbili tu; Bukoba mjini na Bukoba vijijini.
Kingine wengi mnaonekana mnajua Kagera yote ni wahaya kitu ambacho sio sahihi. Wilaya zinazoishi wahaya kiasili ni Bukoba vijijini, Missenyi, Muleba na Bukoba mjini yenyewe japo kuwa sasa imekuwa na mchanganyiko (japo kidogo) wa makabila mengine kwa kuwa ni mjini.
Hivyo ni kosa kubwa la kiwango cha lami mathalani mtu kwenda Ngara au Karagwe akase.a wahaya wanaishi maisha magumu hata vijijini hawajajenga nyumba za maana. Hizo wilaya hazikaliwi na wahaya ni wasukuma na wasubi kwa Biaharamulo, Waanagaza kwa Ngara na wanyambo kwa Karagee na Kyerwa.
Ukitaka ujue mhaya vijijini kwake kumejengeka kiasi gani nenda wilaya za Misenyi, Muleba na Bukoba vijijini alafu uone ukirudi kama utakuwa na hata confidence ya kukaa nyima ya keyboard kuilinganisha Bukoba na Moshi.
My take: Maneno kila mtu anaweza kuongea kulingana na kipaji chake cha kubisha au kubeza, ila nadhani points na evidence ndio muhimu zaidi na ndio maana hapa wa Bukoba wanaleta picha ila wa Moshi naona mapambio mengi picha ni aibu. Kabla hujajivika ubishi hakikisha unafika maeneo husika.
Siku iwe njema kwenu