Huu uzi ungekua na maana kama kungewekwa vigezo.
Mfano vya kijamii. Idadi ya wasomi, idadi ya matajiri, idadi ya watu, idadi ya NGOs, kambi za wakimbizi, jinsi jamii inavyojiratibu, ushahidi wa uwepo wa mila kandamizi au imani mbovu km mauaji ya albino na vikongwe, nk
Elimu. Idadi ya shule na vyuo level zote. Ufaulu kitaifa miaka walau mi5 nyuma.
Hadhi ya mji (jiji manispaa halmashauri etc. land area, vivutio vya utalii (moshi kili bukoba victoria), idadi ya watalii nk
Siasa. Nani mtawala, wana umoja, idadi ya wabunge, wametoa mawaziri rais (tunaangalia mji na sio kabila. Mfn Magu angekua wa Bk tyr gepu hilo), n.k.
Miundombinu. Kilometa za barabara za lami, huduma zinazofanya kazi za usafiri wa umma na viwango vyake (mabasi treni meli ndege na pia idadi zake kwa ratiba), idadi ya magorofa ya gorofa 4 5 6 7 8 9 10 n.k, usafi wa mji, urefu wa mitaro, urefu na ujazo wa mifumo ya majitaka, barabara zisizo za lami n.k.
Uchumi. Wote wana ndizi na kahawa na uvuvi kwahyo hapo ushindani ni kiwango cha uzalishaji mauzo na mapato kwa hizo shughuli na zinginezo pia walizozidiana. GDP, contribution ya kodi kwa taifa, idadi ya magari ya serikali na binafsi, trading na shopping centre,
Maadamu ni mijini inafaa kushindanisha maeneo ya sterehe na kujiliwaza (baa beach zilizoendelezwa cinema nyamachoma joints bustani za mijini hoteli na idadi ya vitanda4 swimming pools kumbi za disko pombe za kienyeji na ma maeneo rasmi ya kunywea ikiwamo ustaarabu wake na hapa picha zinahusika sn nk), idadi ya watumiaji wa simu na smartphones,
Uwezo pia uangalie huduma za kifedha mabenki na taasisi za fedha, mzunguko wa pesa,
Usalama na ulinzi. Idadi ya polisi na vituo vya polisi, kambi za jeshi, kiwango cha uhalifu, uelewa wa wenyeji kuhusu usalama kwa ujumla,
Kimataifa. Idadi ya mashirika na taasisi za kimataifa zenye makazi miji hiyo, ofisi ndogo za ubalozi, nk
Najua vingine vigumu kupata kwa ushabiki wa humuhumu ila with time inawezekana. Nadhani hapo tutaitendea haki JF as HoGT.
Kujaza mapicha ya majengo humu sio ishu sana maana ni sehemu tu ya ushidani tena kijipengele.
Kurahisisha teueni watu wenu wasimamie mtifuano. Maana kuna stori hii miji (sio kabila) ina wasomi na wastaarabu wengi. Make this a battle of minds.
Kila kipengele kitachokubaliwa kushindaniwa kuwe na takwimu.
Mwishoni itatupa mwanga as a people tukowapi na wapi pa kujiboresha.
Nawasilisha na poleni kwa gazeti lisilo na picha.