Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,785
- 46,503
Mwaka 1991 wakati USSR inavunjika mataifa kadhaa yaliyokuwa yanaunda umoja huo yalikuwa yanamiliki silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu. Ukraine lilikuwa ni taifa mojawapo lililokuwa likimiliki mzigo mkubwa wa silaha za nyuklia na nyinginezo nzito, ilikuwa taifa la tatu duniani kwa umiliki wa silaha za nyuklia baada ya Urusi na Marekani.
Kuvunjika kwa USSR ilikuwa ni furaha kubwa kwa Marekani na Uingereza na West yote kwa ujumla lakini pia kulikuja na hofu kubwa mno kwao kwamba kusambaratika huko kwa USSR kungeleta sintofahamu kubwa ya masuala ya kiusalama Ulaya kwa sababu mataifa mengi yaliyotoka USSR yalikuwa na silaha nyingi nzito zikiwemo nyuklia. Hapo ndipo Rais wa Marekani wa kipindi hicho George H.W Bush akabuni makubaliano ambayo aliwashirikisha Urusi, Uingereza na Ukraine kutatua sintofahamu hiyo. Baadaye makubaliano hayo yaliendelezwa kwa upana na ukubwa zaidi na Bill Clinton na yakaitwa Budapest Memorundum kwa sababu yalisainiwa rasmi katika mji wa Hungary wa Budapest mwaka 1994.
Makubaliano hayo ni marefu sana lakini katika kina chake hasa ilikuwa ni Ukraine kupeleka Urusi au kuharibu silaha zake zote za nyuklia pamoja na makombora yake masafa marefu kwa ahadi ya kwamba Urusi, Marekani na Uingereza hawataingilia uhuru nchi hiyo na wataheshimu mipaka ya Ukraine kama taifa huru. Pia Urusi kukazia ikaahidi msaada na mkopo wa gesi na mafuta wa zaidi ya $billion 2.5. Ukraine walitaka mkataba kamili kutoka kwa Marekani na Uingereza unao guarantee usalama wa mipaka yake lakini hadi mwisho wa makubaliano waliishia kupata ahadi tu kutoka kwa Wamarekani kwamba watapata ulinzi kamili kutoka kwao endapo taifa lolote litawaingilia au kuwavamia baada ya kukabidhi au kuharibu sila zao. Kulitokea mzozo, ubishani na upinzani mkali sana ndani ya Ukraine hadi kusababisha waziri wa ulinzi kujiuzulu lakini mwisho wa siku Ukraine ikaingia makubaliono hayo na kuyatekeleza yote mpaka kufikia mwaka 2008.
Matokeo yake baada ya muda mfupi baada ya Ukraine kutekeleza makubaliano yote Rais wa Urusi Putin akaanza kutoa kauli za ajabu ajabu kuhusu Ukraine kama "Urusi na Ukraine ni watu wamoja na mwisho wa siku lazima watarudi kuwa watu moja", "Ukraine kwanza ni taifa lisilio halisi la kutengenezwa tu lisilo na historia yake" n.k. Urusi ikaanza kuingilia siasa za ndani ya Ukraine kwa nguvu kubwa kipindi cha Rais Viktor Yanukovych wa Ukraine kuanzia 2010 baada ya kuona Ukraine ilikuwa inaelekea mueleko na kuzidisha ukaribu zaidi na West. Ikaanza kuzalisha vikundi vya uasi na kujitenga mipakani mwa Ukraine, ikavamia Ukraine mwaka 2014 na kuendelea kuivamia nchi nzima mwaka 2022. Urusi ikawa imevunja makubaliano yote ya Budapest memorandum na pia Ukraine ikiwa haina sila zake wala guarantee yoyote ya usalama kutoka Marekani au Uingereza. Wamarekani wengi hawataki kulikumbushia hili suala kwa sababu linaanika kiasi gani walivyo na deni kubwa kwa Ukraine.