Budapest Memorandum: Ulaghai wa kihistoria Warusi waliowafanyia Marekani, Uingereza na Ukraine

Romania na Bulgaria ziko Black Sea na pia ni wanachama wa NATO.
Hawana mpaka direct na Russia. Russia amekuwa ally mkubwa wa Bulgaria na Romani miaka nenda rudi na hawana uhasama wa kihivyo.

Hivyo hao jamaa hawana uhasama na Russia kama allies wengine wa NATO.

Na Russia ana presence kubwa sana black sea hata kwenye territories za hizo nchi. Kiujumla black sea ipo controlled na Russia.
 
Sababu kubwa ya Putin kufanya anachofanya ni Ukraine kutaka kujiunga NATO. Kama ujuavyo nchi za NATO ni adui wa Russia kuanzia nyanja ya kiuchumi mpaka kijeshi. Na policy yao hao jamaa ni kuweka kambi zao za kijeshi kila kona ya dunia hasa kwa nchi wanazokuwa nazo marafiki au walioko kwenye umoja huo.

Lengo likiwa ni kuendeleza ubabe na kuchuma rasilimali za nchi husika. Yani US na allies wake wanaamini kuweka bases kila pembe ya dunia hata ikitokea all out war wanaweza kumpiga mtu yeyote mahali popote kutokea mahali popote duniani.

Angalia issue ya China na Taiwan. US ndio anasababisha chokochoko.

Sasa kumuingiza Ukraine NATO maana yake US anakuwa na access rahisi na anaweza kuweka kambi za kijeshi karibu kabisa na Urusi ambae ni hasimu wake. Hapo ni sawa na kumshika mrusi kalio. Hakuna nchi inayojitambua inaweza kukubali huu ushenzi, ndio maana hata China huu ujinga wa Taiwan hataki kuusikia.

So kwa maslahi mapana ya nchi yake Putin hakuwa na option zaidi ya kumstopisha Ukraine.
Vita nyingi duniani nyuma yake msababishi mkubwa ni US NA NATO.
 
Na wewe ni mmoja wa victims walioathirika na hizo propaganda za Putin za kudai kuwa Marekani inataka kuiangusha Urusi. Iwapo Marekani ingekuwa inataka kufanya hivyo, kwanza isingesimamia hiyo Budapest memorandum kuhakikisha silaha zote za Nyuklia zinakwenda Urusi na kuiacha Ukraine haine Kitu. Pili, Marekani ilikuwa na takriban miaka kumi za kuingusha kabisa Urusi yote baada ya kuvunjika kwa USSR. Badala yake katika kipindi cha kuanzia 1994 hadi 2004 Marekani iliisaidia sana Urusi kuimarisha uchumi wake bila vikwazo vyovyote; Mpaka sasa hivi Urusi inadaiwa fedha nyingi sana na Marekani ilizokopeshwa kwa ajili ya kujenga uchumi wake. Elewa hapa kuwa inadaiwa pesa ilizokopa (kama Tanzania inavyokopa), siyo pesa za kuuza hati fungante kama ambazo Marekani inadaiwa.

Tatizo la Putin ni nia ya kung'ang'ania madaraka tu, kwani kosa kubwa la Ukraine na Georgia limekuwa lile la kufanya uchaguzi na kubadilisha viongozi. Huo unakuwa ni mfano mbaya sana mlangoni mwake ambaye haamini utamaduni wa kubadili viongozi; hawezi kuishambulia Belarus mpaka pale watakapobadilisha rais
We jamaa acha uongo russia haijawahi kukopeshwa mkopo na marekani eti uchumi wa russia umejengwa na marekani yaani adui yako kabisa umsadie kuimarisha uchumi wake leta chanzo cha hiyo habari inayoonyesha kwamba marekani imetoa dollar million kadhaa kuisaidia russia.

Ki historia Ukraine imebadilisha viongozi wengi kuanzia 1991 tena walikuwa wanabadilisha kwa kupokezana term hii akishika Pro-west term inayokuja inashika Pro-Russia hiyo imeenda hivyo mpka mwaka 2014 sasa unavyosema wakifanya uchaguzi, ndo russia huzivamia huo nao ni uongo.

Uvamizi uliofanywa Georgia ilikuwa ni baada ya kutaka kujiunga na NATO, Kama sikosea ni 2008 rejea NATO summit ya mwaka huo waliotaka kujiunga ilikuwa yeye na Ukraine ila baadhi ya member wa NATO walikataa ikiwemo German na Ufaransa ambao nao waliona wakizikubalia itazua vita ila walichowaahidi ni kwamba kwa baadae inaweza kuwafikiria na mwaka huo huo baada ya hiyo summit ndo georgia ilivamiwa na russia.
 
Iweke hapa hiyo katiba ya Ukraine inayosema Ukraine itajiunga NATO
kumbe hili nalo hujui?
aiseee sasa mnapata wapi nguvu za kujibishana ikiwa hujui kama hili la ukraine kujiunga nato walishaweka kwenye katiba yao?


google basi usome na vingine..... inaonekana mnaandika mada ambazo hamjazielewa vizuri
 
soma hapa labda utaelewa kwanimi Urusi alivamia 2022,......
Sababu za uvamizi kutoka mdomoni kwa Putin
“Its goal is to protect people who have been subjected to bullying and genocide by the Kyiv regime for eight years. And for this we will strive for the demilitarisation and denazification of Ukraine, as well as bringing to justice those who committed numerous, bloody crimes against civilians, including citizens of the Russian Federation.”
 
1. kama huelewi kuhusu hili au hujui hili, basi hustahili kujibiwa!

2. hata cuba ilikua nchi huru, lakn unajua kilichotaka kutokea?

3. shida sio hayo makubaliano ya hungary, bali ni ukraine kuliweka suala la kujiunga nato kwenye katiba yao............ kwanini wataka kwenda Nato huku wakijua Nato na urusi hawakai chungu kimoja?
Kwa hiyo Ukraine ni mkoa ndani ya Russia.😲😲
 
Na wewe ni mmoja wa victims walioathirika na hizo propaganda za Putin za kudai kuwa Marekani inataka kuiangusha Urusi. Iwapo Marekani ingekuwa inataka kufanya hivyo, kwanza isingesimamia hiyo Budapest memorandum kuhakikisha silaha zote za Nyuklia zinakwenda Urusi na kuiacha Ukraine haine Kitu. Pili, Marekani ilikuwa na takriban miaka kumi za kuingusha kabisa Urusi yote baada ya kuvunjika kwa USSR. Badala yake katika kipindi cha kuanzia 1994 hadi 2004 Marekani iliisaidia sana Urusi kuimarisha uchumi wake bila vikwazo vyovyote; Mpaka sasa hivi Urusi inadaiwa fedha nyingi sana na Marekani ilizokopeshwa kwa ajili ya kujenga uchumi wake. Elewa hapa kuwa inadaiwa pesa ilizokopa (kama Tanzania inavyokopa), siyo pesa za kuuza hati fungante kama ambazo Marekani inadaiwa.

Tatizo la Putin ni nia ya kung'ang'ania madaraka tu, kwani kosa kubwa la Ukraine na Georgia limekuwa lile la kufanya uchaguzi na kubadilisha viongozi. Huo unakuwa ni mfano mbaya sana mlangoni mwake ambaye haamini utamaduni wa kubadili viongozi; hawezi kuishambulia Belarus mpaka pale watakapobadilisha rais
NATO na marekani siku zote wanataka kuiangusha urusi
 
Hujui kuwa Gorbachev alikuwa ni puppet wa WEst na sera zake za glasnost na perestroika ndio zilisababisha kuvunjika wa USSR jambo ambalo US na wenzie ndio walikuwa wanalitaka. Lakini kipindi hicho unachosema wewe kuwa NATO ingeweza kuisambaratisha Russia ndio kipindi ambacho kilikuwa na maraisi miamba sasa ambao waliinua nchi yao kichumi na kuweza ku compete na super powers nyingine (Yeltsin, Medvedev na Putin)

Ukweli ni kwamba NATO hawezi kuingia tena kijanja Ukraine so kama ni strategy basi Russia ame win. Kuhusu nguvu kazi kuwa vijana wanakimbia nchi hizo ni propaganda za West tu wala hakuna uhalisia.
Anapiga kelele tu huyo!

Muulize kwa nini Rwanda ya Paul Kagame ikifanya makeke yake wao ndiyo wa kwanza humu kupiga kelele kuwa anahatarisha amani ya ukanda wetu? Hali inafika mbali mpaka wengine wanasema Rwanda ni ya kuipiga tu!

Kama wabongo wenyewe kwa Rwanda wanaona hivyo sembuse Russia?! Watulie tu kwa usalama wa nchi yao?

Huyu Kichuguu aache unafiki.
 
Kuvamia nchi jirani siyo option. NATO ilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuitawanya Urusi katika kipindi cha kuanzia mwaka `1993 hadi 2004 kwani ilikuwa na control kubwa sana juu yake lakini haikufanya hivyo, badala yake ikajikita katika kuisaidia Urusi ili isimame imare tena, halafu baada ya hapo eti ndipo uadui uanza kama Putbi hakuwa na usongo wa ndani siku hizo zote?

Kitendo cha kuivamia Ukraine hakijasaidia lolote kwenye maslahi ya nchi yake bali ndipo ameikaribisha NATO zaidi mlangoni mwake huku vijana ambao niyo nguvu ya kesho ya taifa wakiwa wanakimbia nchi. Sasa hivi Putin anajivunia wale wazee wa zamani waliokulia ndani ya Soviet Union na watu wa vijijini wanasikiliza habari kwenye TV ya Taifa tu. siyo generation mpya inayoishi kwenye majiji kama Moscow na St Pettersberg.
Hapo kwenye Bold unatudanganya. Urusi na Warusi siyo kama Wasandawe wa Tanzania hadi waangalie taarifa ya habari ktk TV ya Taifa. Wale watu wapo mbali sana kiuchumi na kimaendeleo.
 
1. Utajiri wa Afrika unaporwaje wakati tunaona kila nchi ya Afrika ikiwa inatawaliwa na waafrika wenyewe. Unaweza ukatupa uthibitisho wowote wa madai yako..?

2. Mimi nafikiri Ukraine ni nchi huru tu kama vile Tanzania, Kenya, Zambia nk, sasa kuna nchi duniani yenye haki ya kuichagulia nchi yoyote maadui au marafiki.

3. Unafahamu chochote kuhusu Budapest Agreement iliyohusisha mataifa ya Ukraine, Marekani, Uingereza na Russia.
Kama hujui bado omba uelimishwe lakini Aftican resources are being plundered.

Mfano rahisi fuatilia saga ya Ufaransa na makoloni yake west Africa.
 
Mwaka 1991 wakati USSR inavunjika mataifa kadhaa yaliyokuwa yanaunda umoja huo yalikuwa yanamiliki silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu. Ukraine lilikuwa ni taifa mojawapo lililokuwa likimiliki mzigo mkubwa wa silaha za nyuklia na nyinginezo nzito, ilikuwa taifa la tatu duniani kwa umiliki wa silaha za nyuklia baada ya Urusi na Marekani.

Kuvunjika kwa USSR ilikuwa ni furaha kubwa kwa Marekani na Uingereza na West yote kwa ujumla lakini pia kulikuja na hofu kubwa mno kwao kwamba kusambaratika huko kwa USSR kungeleta sintofahamu kubwa ya masuala ya kiusalama Ulaya kwa sababu mataifa mengi yaliyotoka USSR yalikuwa na silaha nyingi nzito zikiwemo nyuklia. Hapo ndipo Rais wa Marekani wa kipindi hicho George H.W Bush akabuni makubaliano ambayo aliwashirikisha Urusi, Uingereza na Ukraine kutatua sintofahamu hiyo. Baadaye makubaliano hayo yaliendelezwa kwa upana na ukubwa zaidi na Bill Clinton na yakaitwa Budapest Memorundum kwa sababu yalisainiwa rasmi katika mji wa Hungary wa Budapest mwaka 1994.

Makubaliano hayo ni marefu sana lakini katika kina chake hasa ilikuwa ni Ukraine kupeleka Urusi au kuharibu silaha zake zote za nyuklia pamoja na makombora yake masafa marefu kwa ahadi ya kwamba Urusi, Marekani na Uingereza hawataingilia uhuru nchi hiyo na wataheshimu mipaka ya Ukraine kama taifa huru. Pia Urusi kukazia ikaahidi msaada na mkopo wa gesi na mafuta wa zaidi ya $billion 2.5. Ukraine walitaka mkataba kamili kutoka kwa Marekani na Uingereza unao guarantee usalama wa mipaka yake lakini hadi mwisho wa makubaliano waliishia kupata ahadi tu kutoka kwa Wamarekani kwamba watapata ulinzi kamili kutoka kwao endapo taifa lolote litawaingilia au kuwavamia baada ya kukabidhi au kuharibu sila zao. Kulitokea mzozo, ubishani na upinzani mkali sana ndani ya Ukraine hadi kusababisha waziri wa ulinzi kujiuzulu lakini mwisho wa siku Ukraine ikaingia makubaliono hayo na kuyatekeleza yote mpaka kufikia mwaka 2008.

Matokeo yake baada ya muda mfupi baada ya Ukraine kutekeleza makubaliano yote Rais wa Urusi Putin akaanza kutoa kauli za ajabu ajabu kuhusu Ukraine kama "Urusi na Ukraine ni watu wamoja na mwisho wa siku lazima watarudi kuwa watu moja", "Ukraine kwanza ni taifa lisilio halisi la kutengenezwa tu lisilo na historia yake" n.k. Urusi ikaanza kuingilia siasa za ndani ya Ukraine kwa nguvu kubwa kipindi cha Rais Viktor Yanukovych wa Ukraine kuanzia 2010 baada ya kuona Ukraine ilikuwa inaelekea mueleko na kuzidisha ukaribu zaidi na West. Ikaanza kuzalisha vikundi vya uasi na kujitenga mipakani mwa Ukraine, ikavamia Ukraine mwaka 2014 na kuendelea kuivamia nchi nzima mwaka 2022. Urusi ikawa imevunja makubaliano yote ya Budapest memorandum na pia Ukraine ikiwa haina sila zake wala guarantee yoyote ya usalama kutoka Marekani au Uingereza. Wamarekani wengi hawataki kulikumbushia hili suala kwa sababu linaanika kiasi gani walivyo na deni kubwa kwa Ukraine.
Umenza vem article yako lakini umeingiza propaganda plae ulipoanza 2008 Putin aligeuka. Je ulifuatilia mahojioni ya Putin na Mwandishi Culson Tucker? Hebu fuatilia. Na putin aikua anasema kama kasema uongo wakanushe.

Lakini pia hukuweka kiini cha mgogoro huu wa sasa. Vita vya wenyewe 2014 to 2022 Urusi ilihusikaje? NATO je? Eu je na hao wote walikua Sehemu ya Budapest Memorandum?
 
Sababu za uvamizi kutoka mdomoni kwa Putin
“Its goal is to protect people who have been subjected to bullying and genocide by the Kyiv regime for eight years. And for this we will strive for the demilitarisation and denazification of Ukraine, as well as bringing to justice those who committed numerous, bloody crimes against civilians, including citizens of the Russian Federation.”
acha utoto,

umeomba kujua ikiwa katiba ya ukraine inatambua hilo la wao kujiunga nato, nimekupa!

so far inaonekana uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo,
 
Kama hujui bado omba uelimishwe lakini Aftican resources are being plundered.

Mfano rahisi fuatilia saga ya Ufaransa na makoloni yake west Africa.
hivi vijamaa havina uelewa wa mambo yanayoendelea hapa tanzania na afrika, alafu vinadhani vinaweza kuelewa yanayoendelea Ulaya na Geopolitics za dunia.......
 
Back
Top Bottom