Hivi ndivyo Marekani inavyojimaliza yenyewe,na haizuiliki kwani si mipango yake tena

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,736
12,059
Baada ya kuitawala dunia kiuchumi na kijeshi kwa miongo kadhaa,sasa Marekani inaelekea kudondokea pua yake na hakuna wa kuizuia.

Katika kipindi cha miaka kama 24 imeshiriki vita vingi vilivyokuwa na malengo mapana ya kuzipindua na kuzitawala nchi kadhaa na nyingi zao ni za waislamu. Hakuna hata sehemu moja ilipofanikiwa.

Hata alipoweza kupindua serikali na kuua viongozi wake lakini bado hakuweza kutawala.

Hatimae mwaka 2022 akaingia vitani kiaina na Urusi chini ya kivuli cha NATO katika kuisaidia Ukraine ili ishinde.

Hivyo vita vimeendelea kwa takriban miaka 2 mpaka Urusi imemega maeneo yote ya kiuchumi ya Ukraine ikiwemo bandari na viwanda vya chuma na madawa.

Raisi Zelensky wa Ukraine tangu alikuwa akiwapa matumaini raia wake na mataifa washirika mpaka sasa ameishiwa maneno na anasema wazi wazi bila misaada ya fedha na silaha kutoka Marekani basi itabidi arudishe jeshi nyuma. Hilo ni tangazo la kukaribia kushindwa vita.

Pamoja na maelezo hayo ya Zelenky bado kuna wabunge wa Marekani wanaohimiza kuidhinishwa kwa msaada wa dola bilioni 61 ambazo nyingi zitaelekezwa Ukraine na nyengine Israel.

Fedha viwango vikubwa kuliko hivyo na silaha vimeidhinishwa na kupelekwa Ukraine mara kadhaa tangu pale vita vianze na wala havikusaidia chochote kuiokoa na hali iliyonayo Ukraine sasa ya kukata tamaa.

Marekani kukubali kutoa tena fedha kuokoa jahazi linalozama si akili yake tena bali ni mipango kutoka juu ili nayo izame moja kwa moja na kiburi chake kimalizike.
 
Hakuna Dolla iliyowah kudumu karne na karne duniani.

Unapompiga mtu nae anajioanga na kuangalia madhaifu yako, kama si yeye basi uzao wake utakuwa na kumbukumbu za kuendeleza mapambano ili kujilonda na unyanyasaji, ni kweli MAREKANI imefika mahala ushirikiano wa Korea kasi, China, Iranj na Urusi vimemdhibiti sana.

Kila akitafuta engo ya kuingia anakutakana ukinzani ambao hapo awali alikuwa haupati ikiwemo kutumia garama kubwa na kupata output kiduchu.

Mimi nafurahishwa na hilo ukizingatia Marekani ni Nyonyaji kuu la Mataifa mengi hasa ya Africa
 
Back
Top Bottom