KERO BRELA huduma zao mbovu hadi uwahonge pesa ndio wanakamilisha kazi yako

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

nokwenumuya

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
810
2,851
Ndugu zangu watanzania, sisi wajasiriamali tunaojaribu kufuata sheria na kuwa complied na sheria za Nchi tunapitia mengi sana.

Wakati wa JPM ulikuwa ukifanya returns BRELA au mabadiliko yoyote kwenye kampuni yako ulikuwa unapata huduma kwa haraka sana.

Nina miezi mitatu nimefile BRELA returns bila mafanikio, mwezi October mwanzoni Afisa mmoja wa BRELA akaniomba ili aweze kunikamilishia haraka nitoe 200,000. kwa kuwa kazi yangu ilikuwa imekaa muda mrefu nikawa sina msaada nikampatia.

Akaweza tu kunitengenezea Control Number nikalipa, baada ya hapo wananiambia kazi iko kwenye final stage, ili iweze kuwa approved inabidi nitoe 200,000 nyingine, just for a stupid and irresponsible person to press an approved button.

Nchi hii sijui tunaipeleka wapi, yaani mfumo wa Brela Online Registration System una urasimu mkubwa kuliko hata ule wa manual.

Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, na Maafisa wengine wote wanaohusika waingilie kati, wajaribu tu kuingia kwenye Online Portal ya Brela kujionea kazi ambazo zimewekwa pending bila sababu ya msingi.

Kwa kuwa wao wamekaa wanalipwa kwa kodi zetu hawajali kama wanatukwamisha katika shughuli za uzalishaji Mali au la.
 
Kuna ka business name kangu nilikuwa nasajiri naona week imekata bado sijapata majibu. Status iko waiting for final decision. Brela sikuhizi imekuwa ya kipumbavu sana.
hiyo final decision hadi utoe hongo. wakati wa JPM waki confirm hakuna mgongano wa majina baada ya kupewa control number na kulipiwa automatically ina generate cerfificate una print.

sasa hivi kusajiri business name ni 20,000 kisha ili wafanyakazi wa brela wai approve lazima walambe si chini ya 100,000.
 
hiyo final decision hadi utoe hongo. wakati wa JPM waki confirm hakuna mgongano wa majina baada ya kupewa control number na kulipiwa automatically ina generate cerfificate una print.

sasa hivi kusajiri business name ni 20,000 kisha ili wafanyakazi wa brela wai approve lazima walambe si chini ya 100,000.
ndio namimi nimeshangaa mkuu miaka ya zamani ilikuwa ukishapata control. number ulipe basi certificate unapata. inashangaza kudaiwa rushwa wakati wewe ni mlipa kodi tarajiwa kabisa. maana ukitoka hapo unaenda TRA maana yake hawa wanahujumu mapato ya nchi.
 
Back
Top Bottom