Mpesa MasterCard Tanzania: Kama unapenda uhakika wa malipo yako mtandaoni USIITUMIE

lwifunyomangula

New Member
Jul 30, 2020
1
75
Habari wana-bodi, kwa Majina naitwa Lwifunyo Mangula, ni mmoja wa watu wanaopenda technolojia ikiwamo IT ninaifurahia na nina kautaalamu kidogo kuhusu online business maana ninapenda hivyo vitu. So hapa nipo kutoa ushauri kwa wadau wengine kuhusu MPESA MASTERCARD TANZANIA kulingana na UZOEFU wangu wa niliopitia.

Mwanzo walipoleta MPESA MASTERCARD nikasema yes… kitu kizuri na nikajaribu kuitumia kwa mara kadhaa, lakini baada ya huduma mbovu nilizopata (HUDUMA YA MTEJA na KITEKNOLOJIA) kutoka kwao hivi karibuni basi nikaona niwashirikishe wadau nanyi msije ingia ktk changamoto za malipo mtandaoni na kiuchumi ktk shughuli zenu.

Tarehe 06/07/2020 niliingia ktk website moja ya ughaibuni kununua software Fulani na nikafuata taratibu za kufanya malipo na nikachagua 2checkout payment gateway, kisha Master Card kukamilisha malipo. Baada ya kubofya kitufe basi Tshs. 471,016.73 zikakatika katika akaunti yangu ya Mpesa Mastercard na nikapokea ujumbe wa meseji kuwa pesa imekatika. Ila nilipoangalia ktk website hiyo pesa ilikuwa haijawafikia na ukatokea ujumbe kuwa ‘failed’ na wakasema nilirudie.
screen shot message- hidden.jpg

Meseji ya Mpesa MasterCard kwamba pesa imekatwa kwa malipo

Kutokana na hilo nikajaribu kuwasiliana na pande zote tatu ikiwepo mmiliki wa website, 2checkout na Vodacom Tanzania. Ila baada ya kufuatilia nikaona Vodacom ndio watu wa kunisaidia maana kule wanasema malipo hayajawafikia. Huduma kwa mteja kwa hawa 2checkout na mmiliki wa website zilikuwa nzuri ila KASHESHE ILIKUWA KWA VODACOM TANZANIA.
2checkout first human respose - hidden.jpg

Majibu ya 2checkout.com ya awali kabisa, huyu ni mtu halisi

Mawasiliano na Vodacom Tanzania
Baada ya hayo nikapiga 100 kuongea na mtu wa Vodacom lkn sauti yao ikawa inanielekeza niende ktk mitandao yao ya kijamii kupata msaada na KWA KWELI HUDUMA YA KUONGEA NA MHUDUMU KWA SIMU 100 WAMEZIFICHA. Nikaenda Vodacom Facebook page, duu kuanza kuchat nao nikakuta nachat na BOT AMBALO HATA HALINIELEWI nini msaada ninao hitaji. Yaani swala la pesa kiasi hiki 471,016 wanakupa roboti uchati nalo sijui kuonesha kwamba kuwa hawathamini pesa zako?
Voda bot 2.JPG

Vodacom Tanzania Facebook Messenger Bot Wanayemwita TOBI

Voda bot cover.JPG

Huyu Bot amenisaidia nini hapa na Tshs. 471,016.73 yangu kama sio kunikosea UBINADAMU?

Nikaenda Vodacom website yao, huko nikaanza kuchat na alikuwa sijui mtu halisi na akasema kuwa swala langu haliwezi kutatuliwa online hivyo niende Vodashop; sababu kipindi hicho nilikuwepo Njombe mkoa basi nikajitahidi niende huko.

Nilivyofika Njombe Vodashop (MKOANI) nikawaeleza tatizo langu na wakasema swala la MPESA MASTER CARD WAO HAWAWEZI LISHUGHULIKIA bali niwasiliane na makao makuu. Duuu! Nikawaambia nimewapigia 100 lkn simpati mtu wa kuongea naye maana wanasema niende ktk social networks zao kutatuliwa tatizo langu (kule nilikotoka kuwasiliana na roboti). Nikamwomba na kumbembeleza kuwa anisaidie kuwapigia basi hao 100 kwa simu yangu, akakubali na kunisaidia na akawapata akanipa niongee nao. Nikawaelekeza tatizo langu na yule mhudumu akasema swala langu litatatuliwa na pesa yangu ITARUDISHWA NDANI YA SIKU 3. Daah, siku 3, nikalalamika kwamba mimi siku 3 ni nyingi maana hiyo Tshs. 471,016.73 ni kubwa kwangu; nikambembeleza yule mtu ifanyike haraka na akasisitiza siku 3. Wakanitumia meseji ya support desk number ili niwasiliane nao kwa WhatsApp. Nikaenda WhatsApp kuwasiliana nao na kuomba tena muda usiwe siku 3 lkn kwa kuchelewa wakanijibu wakisisitiza zitarudi ndani ya siku 3 na watanitaarifu.
Vodacom1.JPG

Vodacom WhatsApp Support

Vodacom  2.JPG

Vodacom 3.JPG


Vodacom Tanzania Wameanza Kunipiga Chenga Mteja
Okey, nikawa mpole na nikasubiri siku 3 zikapita na sikupokea pesa wala simu wala meseji. Nikawapigia 100 tena kwa kuifukua walipoficha huduma nikawapata na wakaniambia lile swala inabidi niende Vodacom Shop nikaandike barua ya kuomba pesa yangu kurudishwa nikiwa na kitambulisho. Duuu, sura mpya hapa! Ikabidi nifanye hivyo na kwenda Vodacom Shop Njombe. Nilipofika pale wale wahudumu wakashangaa kuhusu barua, baadaye wakajaribu kufuatilia wakasema inabidi nijaze fomu. Wakanipa fomu nikajaza na kuweka nakala ya kitambulisho. Nilipokuwa pale nakumbuka kuna kaka mmoja alikuwa na tatizo la post-paid kwa simu, aliwawashia moto pale na baadaye nikaona wanapunguza spidi kunihudumua mimi na kumshuhurikia yule kaka maana amewasha moto.
IMG_20200715_164056.jpg

Fomu ya kuomba pesa irudi from Vodacom , niliandika kwa Kiswahili na wao hawakunipa maelekezo ya Lugha
IMG_20200730_155335.jpgNikasubiri baada ya siku kadhaa kwamba pesa yangu itakuwa imerudi… wapi bado. Nikawapigia simu 100 na nakumbuka alipokea mkaka, huyu alikuwa mwelewa kidogo na akasema swala langu litatatuliwa ndani ya masaa 24. Nikamweleza nimeandika barua, nimepiga simu, nimeenda Vodacom Shop mkoa ila bado… akaangalia taarifa zake akasema anaomba washughulikie na ndani ya masaa 24 pesa nitakuwa nimerudishiwa pesa zangu. Okey nikaongeza uvumilivu.

Hapa Ni Kama Siku 21 Bado Vodacom Wananizungusha
Baada ya siku kama 2 nikaamua kuwapigia tena baada ya kuona masaa 24 yamepita na pesa sijapata. Alipokea mdada na akasema sawa ngoja basi walishughulikie (kama hawafahamu vile nilianza hii kitu tangu siku nyingi, hawana connection), nikamsisitiza kuwa nimewasiliana na Vodacom kwa muda mrefu na hii ni kama siku ya 21 tangu nifanye malipo. Nikamwomba na kumbembeleza nionge na Mpesa MasterCard Manager, baadaye akakubali na akanisubirisha na kisha nikaongea naye! Yule kaka manager, akaomba anipigie kwa simu private. Baadaye akanipigia na kumweleza mkasa mzima na kumwambia barua tayari niliandika na akasema anafuatilia na atanirudia baadaye. Baadaye alivyonipigia akasema barua ameiona na majibu yalikuwa inabidi nirudie kuandika barua kwa lugha ya Kiingereza ila walikuwa wamesahau kunitaarifu (kwahiyo bila mimi kuwapigia na kufuatilia huo mrejesho nisingepata na pesa ingekuwa imepotea). Nikamwambia vipi kama sijui kuandika Kiingereza? Akasema naweza omba mtu anisaidie kuandika hiyo barua ya kiingereza. Ikabidi nikubali kufanya hilo na nikamwambia kwa namna huduma mbovu ninavyoipata basi nitaenda ktk mitandao ya kijamii kuwaambia umma wasitumie huduma yao ya Mpesa MasterCard maana naona sisikilizwi na ni bora niwataarifu wengine wasiangukie tatizo kama hili; akanijibu kwa kuniambia kuwa kwa kwenda kuongea ktk mitandao ya kijamii ndio itatatua swala langu?

Tarehe 30 July 2020
Tarehe 30/07/2020 nikaenda Vodashop mkoa Njombe kuandika barua sasa iwe ya kiingereza. Nikafanya kama walivyotaka na kuiacha pale… bado nasubiri nione mrejesho wao utakuwaje; sijui watanipa pesa zangu au watazipotezea? Au sijui watanipigia simu au kutuma meseji kunipa hatua nyingine ya kufuata? Sijui ndio watakaa kimya bila mrejesho wowote mpaka nianze kufuatilia tena?
IMG_20200730_155239.jpg

30 July 2020 Fomu ya Kiingereza Niliyojaza

Nionavyo Mimi Na Ushauri Wangu Kuhusu Huduma Za Mpesa Mastercard Tanzania
  • Kulingana na huduma nilivyopata (Huduma ya Kiteknolojia na Huduma kwa Mteja) basi nina mashaka sana na uhakika wa HUDUMA ZOTE na MAONO mazima ya kampuni hili kama kweli limedhamilia KWELI KUWASAIDIA WATU ktk huduma mbalimbali maana HUDUMA KWA MTEJA inatupa picha juu ya FIKRA ZA KAMPUNI ktk kuhudumia WATU ambao ni wateja sisi. Mara nyingine ni bora teknolojia ifeli ila MAHUSIANO NA MTEJA YATUNZWE hii italeta maana ya kwamba huyu mtoa huduma ana NIA njema nawe, ila kwa mimi nilivyoona basi hawana hiyo NIA YA DHATI ya kumhudumia mteja labda wana malengo yao mengine.
  • Kama swala la pesa linatoka ktk simu yako ila mlengwa (muuzaji) aliye nje ya nchi haipati, basi kuna uwezekano labda mfumo wao haujakaa vyema ktk kumsaidia mteja kuweza kufanya biashara ya UHAKIKA na mtu mwingine wan je ya nchi. Hivyo inawezekana labda hakuna uhakika wa malipo ya MPESA MASTERCARD ktk biashar zetu. Okey sawa labda tatizo ni la muda, mbona zinakaribia siku 30 hakuna utatuzi wake pesa iende au irudi ktk simu yangu?
  • Swala la kuelekezwa niende ktk mitandao ya kijamii kupata msaada na nikaenda huko na kukuta Bot ndie anayenisikiliza kuhusu pesa yangu ya Tshs. 471,016.73 na mbaya zaidi ninamweleza huduma ninayohitaji wala hanielewi: Binafsi ninaona huku ni kukosa UTU na UBINADAMU kwa mteja maana sisi sio mashine bali ni watu wenye hisia na roho; kwa haraka haraka ninavyojua mimi Tshs. 471,016.73 ni pesa nyingi sana kwa mteja ambayo ni kama mshahara wa mtu ambaye ana majukumu ya kutunza familia. Pesa ina nguvu ya MOYO sasa hili wao sijui hawajali ktk wateja sisi? Kama pesa ya 471k unapuuzwa na kupewa roboti likusaidie, je ndugu yangu wewe mwenye kutuma Tshs. 5,000/= utaongea na nani? Ndugu unasubiri likukute lipi ktk pesa yako?
  • Mbona ile website ya ughaibuni na 2checkout waliweza kunihudumia kama mteja na kunipa mrejesho wa haraka wenye mwongozo ijapokuwa wao wapo mbali sana huko, lakini Vodacom ambao wapo hapahapa Tanzania wanaficha huduma za simu 100 kuongea nao; okey hata ukienda ktk mitandao ya kijamii online unaanza kuchat na Bot ambaye hakuelewi… daah. Okey Nikaenda VodaShop Njombe Mkoani na wakasema swala langu la Mpesa MasterCard wao hawawezi kulitatua mpaka makao makuu…Duu. Kwanini Nje waweze toa huduma nzuri, ila hapa hapa Tz washindwe? Inawezekana labda kampuni hili lina shida ya ‘MAHUSIANO YA KIJAMII NA HAWALIPI SWALA HILO UZITO KAMA THAMANI YA MTEJA’. Je, wafanyakazi wake wanafurahia kutoa huduma kwa wateja sisi au wanahasira na kazi hiyo?
  • Kama Bot wa facebook messenger wao wameshindwa kum-program vyema kuweza kunitatulia shida yangu au kuniongoza cha kufanya, Basi je inakuwaje mifumo mingine mbalimbali inayomuhusu mteja ambayo sisi hatuoni au kwa harakaharaka sisi hatuifuatilii? Just Bot programing iweze nijibu swala langu? Wadau hili mnalionaje kuhusu mifumo mingine ambayo sisi hatuioni? Yale mahesabu yetu ambayo sisi hatuyaoni? Umewahi fuatilia kwa undani? Unaweza nipa mchanganuo wa in and out zako kwa mwaka mzima ktk simu yako? Je, kuna urahisi gani wa kupata na ku-question hesabu za in and out zako ktk simu yako na ukapata msaada huo kutoka kwao inavyotakiwa? Nakosa imani kutokana na hili nililolipata la Bot.
  • Kama pesa ya mtu niliambiwa inachukua siku 3 na sasa ni karibia siku ya 30 (almost 10 times) bado sijapata, je, wewe mwenzangu una uhakika gani wa pesa ambayo utalipia kwa Mpesa MasterCard? Embu fikiri mfano nilikuwa namtumia labda rafiki yangu ambaye anaumwa na inabidi apate huduma ya kiafya na yupo nje ya nchi na akikosa ndani ya siku 7 huduma hiyo anafariki, hivyo basi angeweza kuwa amefariki tayari! Kwahiyo ni KIFO! Je, kama ulikuwa unauza nyanya zako na pesa ikakwamishwa kwa muda wa siku 21, je nyanya hizo mtanzania mwenzangu zitakuwa bado zipo nzima au zimeshaoza? Uhakika wa biashara yako kwa MPESA MASTER CARD upo wapi? Maana biashara ni MUDA; mfano umechelewa kuwasilisha tenda document ya ujenzi dakika chache tuu basi automatic unakuwa umeondolewa ktk mchakato wa kushindania tenda; je Uhakika wa biashara na kampuni yako upo wapi hapo?
  • Swala la kupewa ahadi zisizotekelezwa kuwa ndani ya siku tatu, ndani ya masaa 24… utakuwa umepata pesa yako… linaleta ukakasi. Je, ahadi nyingine zinazotolewa ktk huduma nyingine zina ukakasi wa hivi hivi? Tuna uhakika gani wa kuzipata?
Ndugu zangu kulingana na maelezo niliyoweka hapa ambayo yamenitokea, baada pia ya kuunganisha dots za mawazo na niliyoyapata ktk huduma za Mpesa MasterCard basi ninaona HAKUNA UHAKIKA WA HUDUMA kwa Mpesa MasterCard. Tshs. 471,016.73 sio ndogo wala kubwa sana ila kama sijapewa huduma inayotakiwa kwa pesa yangu hiyo, Je, wewe una uhakika gani wa kufanya biashara vyema? Okey kama tatizo likitokea je, wanakusaidia swala lako a kipesa kwa muda gani? Bishara yako itaweza kukaa bila pesa hiyo kwa muda gani? Unataka kutuma milioni ngapi kupitia Mpesa MasterCard, una uhakika gani?

Kama kuna watu wengine wamekutana na shida kama yangu au inayoendana na yangu kupitia huduma hii ya Mpesa MasterCard au Vodacom Tanzania, karibuni kuweka yenu hapa chini. Yamekuwa yakisikika malalamiko mengi ya bunde kuisha haraka… Je, hili lipo? Tuna uhakika gani na huduma kupitia watu hawa?

Makala hizi nitaendelea kuandika ktk mitandao kama Facebook, Twitter, Medium, Quora, YouTube, Instagram, Reddit, Trustpilot. Pia nitaomba media mbalimbali kuniruhusu kuandika kama: Businessinsiders, Techcrunch, IT forums, IT professional journals, Finance & Bankers professional journals, Investors professionals journals, blogs, magazeti ya ndani na nje ya nchi. Ninaandika ili kuwataarifu watu wengine wawe makini na huduma ya Mpesa Master Card maana wasije wakapitia matatizo ya fedha kubwa pengine zaidi ya mimi. Nitaacha kuandika makala hizi mpaka pale ambapo Tatizo na Kero niliyoipata itakapotatuliwa pamoja na wao kujirekebisha ktk hili!

Nina sisitiza watu tuandike zaidi yale ambayo tunatendewa na makampuni haya maana wewe mwenyewe ni shahidi wa kero unazozipata. Hivi, je kama bundle lako likiisha ghafla in unrealistic way na ukawapigia simu na wasitatue, huwa unaenda polisi kufungua kesi yako? — Tuandike makala hizi kuisaidia jamii yetu, watajirekebisha au biashara itawashinda kwa SAUTI YA UMMA…
 

crusader_jr

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
798
1,000
Samahani kwa kuqoute uzi mrefu kwa machache ntakayoyaandika.
Vodacom ni wezi sana na wana customer care mbovu.
Haiwezekani unaweka salio(mfano 2k)ujiunge kifurushi na bado unaambiwa salio halitoshi 😪😪hua wanamaanisha nini by the way.
Juzi nimeweka salio wamekata pesa bila sababu alafu ukiwatafuta unaambiwa mambo tofauti kabisa aisee🤨🤨🤨🤨
All in all vodacom Qmanina zao waache ungese
 

brobiz

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
320
250
Tunashukuru sana mdau kwa kutupazia sauti maana kinachofanywa na mitandao Sasa ni ujambazi wa waziwazi kabisaa pamoja na majibu ya ovyoovyo,nilisha acha kutumia huduma zao za master card baada ya kuona ni ubabaishaji tu,nadhan malalamiko ni mengi sana tunashukuru kwa kutufungulia njia
 

nshaaa

Member
May 19, 2013
35
125
Mwanzo niliufurahia sana uanzishwaji wa hii huduma kwakua watu wa IT inaturahishia sana kulipa vitu kupitia mtandao, lakini usalama wa huduma hii ni changamoto, unaweza weka kiasi kwa lengo la kulipia, pindi unapolipa hakikisha hubaki na salio maana punde si punde utasikia mtu ametumia kadi yako kulipia huduma nyingine pasipo ridhaa yako, sasa unajiuliza wameijua vipi Master Card yako? Kiukweli huduma inahitaji maboresho hasa usalama wa huduma yenyewe la sivyo tutarejea kwenye mfumo wa benki...
 

keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
1,261
2,000
Makato makubwa sana kwa mpesa ukitoa pesa pia wanawalipa sana mawakala Hela ndogo aka kamisheni na huku wadada wanakaa juani kuhangaika.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,110
2,000
Mleta mada umeibiwa na website za wanigeria .Nunua vitu toka maduka ya kimataifa ya kueleweka Kama Amazon, eBay nk

Kununua website za makampuni binafsi uwe na uhakika asilimia Mia moja kuwa Ni genuine na kuwa wao wamejiunga na Master card Kuna wengine payment zao za online hawajaji connect na Master card wengine. Wameji connect ila wezi

Waweza kutangazia bidhaa nzuri mno wakati hawana ukilipa pesa inaondoka .Mimi ilishawahi Nikita elfu kumi na tano yangu ikaondoka Baada ya kuona kitabu nilichonunua kinakataa ki download.Wakati ukilipa tu inatakiwa product uipate Happ hapo kuwauliza wakasema haojafika tuma Tena nikarusha elfu mbili kucheki Kama itakubali kupokea pesa nikakuta pesa imrondoka!!! Kitabu kinauzwa elfu 15 Mimi natuma elfu mbili zikaenda kikawaida ilitakiwa ikatae system kuwa hela. Haitoshi!!! Lakini ikameza tu

Nikawauliza imefika wakasema bado tuma tena nikajua nimeliwa wakasema kuwa kutakuwa na matatizo kwenu nikawaambia acheni uongo wezi nyie wakakata mawasiliano
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
49,878
2,000
Mleta mada umeibiwa na website za wanigeria .Nunua vitu toka maduka ya kimataifa ya kueleweka Kama Amazon, eBay nk

Kununua website za makampuni binafsi uwe na uhakika asilimia Mia moja kuwa Ni genuine na kuwa wao wamejiunga na Master card Kuna wengine payment zao za online hawajaji connect na Master card wengine. Wameji connect ila wezi

Waweza kutangazia bidhaa nzuri mno wakati hawana ukilipa pesa inaondoka .Mimi ilishawahi Nikita elfu kumi na tano yangu ikaondoka Baada ya kuona kitabu nilichonunua kinakataa ki download.Wakati ukilipa tu inatakiwa product uipate Happ hapo kuwauliza wakasema haojafika tuma Tena nikarusha elfu mbili kucheki Kama itakubali kupokea pesa nikakuta pesa imrondoka!!! Kitabu kinauzwa elfu 15 Mimi natuma elfu mbili zikaenda kikawaida ilitakiwa ikatae system kuwa hela. Haitoshi!!! Lakini ikameza tu

Nikawauliza imefika wakasema bado tuma tena nikajua nimeliwa wakasema kuwa kutakuwa na matatizo kwenu nikawaambia acheni uongo wezi nyie wakakata mawasiliano
Voda wamecheki kwenye system wameona pesa ipo pending ndiyomaana wanaprocess reversal.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,110
2,000
Mwanzo niliufurahia sana uanzishwaji wa hii huduma kwakua watu wa IT inaturahishia sana kulipa vitu kupitia mtandao, lakini usalama wa huduma hii ni changamoto, unaweza weka kiasi kwa lengo la kulipia, pindi unapolipa hakikisha hubaki na salio maana punde si punde utasikia mtu ametumia kadi yako kulipia huduma nyingine pasipo ridhaa yako, sasa unajiuliza wameijua vipi Master Card yako? Kiukweli huduma inahitaji maboresho hasa usalama wa huduma yenyewe la sivyo tutarejea kwenye mfumo wa benki...
Sio kweli CVV na password za kujua balance ya master card anazitoa wapi?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
26,110
2,000
Voda wamecheki kwenye system wameona pesa ipo pending ndiyomaana wanaprocess reversal.
Sio kweli hao uzoefu hawana .Pesa ikiondoka haiwezi elea angani.Ukiona salio limepungua hiyo ilishatoka na kutua ardhini inatakiwa uidai toka ilikotua Sio Vodacom

Halafu Vodacom haiwahusu wenye mtandao wa Master card Ndio waweza just what happened

Mleta mada wasiliana na Master card wenyewe

Usiwe na maneno mengi andika tarehe hii hapa nilifanya malipo kwa kampuni hi hapa kwa kutumia master card yenu namba hii.Hela wanasema hazikufika wakati kwenye card yangu namba hii hii hell kwangu ziliondoka .Watakusaidia chap chap.Nenda website ya master card.Ila andika kifupi Sio Hadith ndefu go direct to the point.Sababu hizo customer care zao huwa busy kuliko kawaida be short and clear usiandike hotuba

Kuhusu kuandika kwa hicho Cha kuchafua Vodacom kila eneo kwa kitu usichpjua kwa uhakika waweza ishia jela na kudaiwa mabilioni kwa kuchafua kampuni
Dai Hali yako kwa adabu na heshima na usijifanye una uhakika Sana kuwa tatizo liko Vodacom!! Pesa uruhusu wewe ziondoke Halafu. Uwakomalie Vodacom

Sema wao Wana huruma ningekuwa Mimi ndio MD saa hii ungekuwa unakiona Cha mtema kuni mahakamani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom