BoT wajitafakari kabla ya kuwatuhumu Bloomberg

BoT wajitafakari kabla ya kuwatuhumu Bloomberg

Mkuu pamoja na hoja yako ndefu unajua wakati Rais Magufuli anachukua madaraka mwaka 2015 uchumi wa Tanzania ulikuwa una hali gani na alikuta akiba za fedha za kigeni kiasi gani Benki Kuu.
Kimsingi pamoja na kila hujuma zinazofanywa na baadhi ya Tanzania kwa kutumiwa na vibaraka wa kiuchumi Tanzania itajikwamuua kiuchumi chini ya serikali ya awamu ya tano.
Kwa imani za nchi marafiki kwa serikali ya awamu ya tano wafadhili wanazidisha kutoa missada mingi kwa serikali hiyo ni dalili tosha kuwa serikali ipo kwenye njia sahihi kurekebisha uchumi wa nchi hii.
Nyie kama viongozi wa vyama vya upinzani msifurahie kuona nchi inakwamwishwa katika kujenga uchumi imara. Wekeni uzalendo kwanza badala ya maslahi ya vyama.
Thamani ya fedha ya Tanzania ipo vilevile kama Benki kuu ilivyotangaza nenda maduka ya kuchenji fedha upate uhalisia.

Mbona unalia kama mfuasi wa ccyemu? Eti awamu ya tano, una akili sawasawa wewe?
 
Hata wewe ni mbumbumbu wa maswala ya kiuchumi...
Huyo unaemtetea nimeacha kusoma aliposema tanzania ilipitia inflation ya sukari????? Inflation inapimwa kutokana na bidhaa nyingi..mchumi kuongelea inflation ya bidhaa moja ni kuonyesha hujui unachosema....Consumer Price Index (CPI) ni 'kikapu' na hakipimwi kwa bidhaa mojamoja in isolation..thats Ecos 101..alafu unadanganya Tanzania inapitia Hyperinflation na kuelekea Galloping inflation...upuuzi mtupu!!!!! niko barabarani nitarudi
nahisi ulikua unasoma huku unatembea so hata ulikua huelew sukar ametumia kama mfano mbona bidhaa ziko nyingi tu au ulitaka azitaje zote unga bei unashndana na mchele

biggest cause ya inflation rising price of neccesity commodity ambazo ndo vyakula nahisi ecos 101 ulikua huielew ulimtesa sana mwalimu wako wa macroeconomics
 
Mkuu pamoja na hoja yako ndefu unajua wakati Rais Magufuli anachukua madaraka mwaka 2015 uchumi wa Tanzania ulikuwa una hali gani na alikuta akiba za fedha za kigeni kiasi gani Benki Kuu.
Kimsingi pamoja na kila hujuma zinazofanywa na baadhi ya Tanzania kwa kutumiwa na vibaraka wa kiuchumi Tanzania itajikwamuua kiuchumi chini ya serikali ya awamu ya tano.
Kwa imani za nchi marafiki kwa serikali ya awamu ya tano wafadhili wanazidisha kutoa missada mingi kwa serikali hiyo ni dalili tosha kuwa serikali ipo kwenye njia sahihi kurekebisha uchumi wa nchi hii.
Nyie kama viongozi wa vyama vya upinzani msifurahie kuona nchi inakwamwishwa katika kujenga uchumi imara. Wekeni uzalendo kwanza badala ya maslahi ya vyama.
Thamani ya fedha ya Tanzania ipo vilevile kama Benki kuu ilivyotangaza nenda maduka ya kuchenji fedha upate uhalisia.
unaongelea misaada gan??
tulimshuhudia mipango akilalamika kupata mikopo imekua shida

na kama misaada imezidi mbona deni la taifa linapaa kwa kasi ya ajabu?? bila kuona faida zake within two yrs mtu keshakopa zaidi ya trillion 20 hio misaada ilozidi inatumika wap??
 
Naongeza sababunyingine ya dola kushuka.
Kuondoka kwa Govana wa zamani ambaye alijua benki kuu ni nini na kumweka professa wa Law badala ya ntu wa fedha ama uchumi. Lol ! Nchi hii tunapenda kujiingiza kwenye matatizo wenyewe.
 
Kuna hoja za msingi kwenye mada. Ngoja nami nijaribu kwenda hoja kwa hoja.
1: Mfumoko wa bei. Kwanza mleta mada hakuna mahali ameonesha mtiriko wa mfumoko wa bei kwa kipindi cha hata mwaka mmoja. Je takwimu zinaonesha kuwa mfumoko wa bei umepanda ama umeshuka? Pili huwezi kutumia bidhaa moja tu (sukari) ukasema kuwa mfumuko wa bei unaelekea sijui hyperinflation. Je vip kuhusu bei ya unga wa mahindi, mchele, mafuta ya kupikia hivi navyo bei zake zilikuwaje na kwa sasa zikoje? Ni kweli kuwa bidhaa za vyakula zinabeba mchango mkubwa sana kwenye mfumuko wa bei lakini haimaniishi kuwa uchague bidhaa ile tu ambayo unataka na uache zingine. Hata hivyo mfumuko wa bei pia unahusisha bidhaa zisio za chakula kama mafuta ya petroli na dizeli, hivyo tusichague yale tunayotaka tu yasikike hata kama hayana ukweli.

2: BoP. Ni kweli ni muhimu kuuza nje lakini tukumbuke kuwa kuwa na 'deficit c/a' sio kuwa ni kosa. Kwanza kwa nchi zinazoendelea, kununua zaidi kuliko kuuza ni jambo la kawaida kwani nchi zinapaswa kuwa na mitambo, vipuli na zana mbalimbali. Marekani kwa mfano, imekuwa na BoT deficit toka mwaka 1975 hadi sasa na kwa mwaka jana iliuza bidhaa nje zenyethamani ya 2.2 trilion (USD) wakati ilinunua bidhaa kutoka nje zenyethamani ya 2.7(USD). Kununua zaidi kuliko kuuza pia hakumaanishi nchi haiwezi kutengeneza hizo bidhaa humu ndani bali wakati mwingine ni kwa sababu za "comperative advantage" waliyonayo wengine. Swala la msingi hapa linapaswa kuwa kwenye ishu tatu, mosi tunanua bidhaa gani, kwanini tunanua na tunanua kutoka wapi. Kama tunanua bidhaa kama matrekta kwa ajili ya kuongeza uzalishaji, na tunanunua kutoka kwa wala wanaouza kwa bei nzuri, basi hakuna shida. Marekani licha ya kuwa na trade deficit ya 500 bln (usd), ukweli kuwa sehemu kubwa ya manunuzi ya bidhaa hizo imekwenda kwenye kampuni za kimarekani zilizopo china. Hivyo kwenye GDP yake hizo value hazisomi lakini kwenye GNP yake zinasoma, kitu kinachowasaidia wananchi wake kuwa na pato kubwa.

3: Kuhusu kukopa nje. Kwanza nadhani hii hoja inaenda kinyume na kile alichotaka kusema. Thamani ya fedha ya nchi kama zilivyo bidhaa zingine, huamuliwa na mahitaji yake na upatikanaji wake. Katika muda mfupi. ukopaji wa fedha kwa fedha za kigeni, unaongeza mzunguko na upatakianaji wa fedha za kigeni. Kama nchi inapata mkopo wa dola milioni 500, maana yake ni kuwa kwa muda mfupi mzukungo wa dola utaongezeka. Hata hivyo, kwa kipindi kirefu haswa kama mkopo haukuwekwezwa kwenye uzalishaji, wakati wa mrejesho ndipo kutakuwa na kushuka kwa thamani ya fedha kwani itabidi kulipa dola amabazo kwa wakati huo hazipo. Kwa maelezo haya, hata kama serikali ingekuwa imekopa hizo fedha, bado isingesababisha kuporomoka kwa thamani ya fedha yetu. Hivyo hii hoja kwa sasa haina mashiko, isipokuwa tu kama tutaongelea ulipaji wa madeni ya nyuma.

4:Mazingira ya biashara. Hapa kuna hoja nzuri na ni jambo zito sana katika uwekezaji haswa kwa wageni. Lakini je, hayo mazingira yamebadilika kwa muda gani? Je wawekezaji wameshafunga biashara zao na kuondoka?

5: Matumizi holela ya fedha za kigeni. Hili jambo limeshazungumzwa sana lakini mamlaka husika hazitaki kulifanyia kazi. Ni ukweli kuwa ni lazima watu walazimishi kuitafuta fedha ya ndani. Hii bishara ya ku 'quote' dola kwa shilingi pia ni ya kupiga marufuku. Hata hivyo hizi ni jitahada kwa ajili ya muda mrefu zaidi na sio kwa ajili ya muda mfupi.

6:Hali ya kisiasa. Ni ukweli kuwa kumekuwa na changamoto kubwa sana kwenye ishu za kisiasa. Ili nchi zikue na kuchangia kuimarika kwa fedha ya ndani, 'inclusive economic institutions' ni lazima, na ambazo zinakuwa sapotedi na taasisi imara za kisiasa. Ni muhimu kuwa na sera zinalinda wawekezaji, kuruhusu nguvu ya soko kuamua pamoja na kuwa na mifumo ya wazi ya kushughulikia maswala mbalimbali.

Mwisho:
Ieleweke wazi kuwa thamani ya fedha ya nchi kuwa ndogo kuliko nchi nyingine sio jambo baya haswa kama itatumika vizuri. Kushuka kwa thamani ya fedha ya nchi yetu inapaswa kuwa chachu ya kuuza nje zaidi, kwa kwa dola chache walizo nazo wageni,wanaweza kuapata vitu vingi zaidi kutoka kwetu kuliko thamani yetu kama ingekuwa juu. China inafaidika zaidi na thamani ya fedha yake kuwa chini kuliko ile ya marekani kwa sababu wao wanauwezo wa kuzalisha zaidi. Hivyo kinachotakiwa hapa pamoja na mambo mengine, tuongeze uzalishaji wa bidhaa zainauzwa nje ili tutumie hali ya fedha yetu kuwa na thamani ndogo kama fursa.

Mleta mada ametufanya tufikiri kuhusu thamani ya fedha yetu. Hata hivyo sababu nyingi alizozitaja haziwezi kuwa visababishi vya karibu (immediate cause) bali kwa muda mrefu hna 'solution' zake pia ni za muda mrefu.
Nawasilisha.
 
unaongelea misaada gan??
tulimshuhudia mipango akilalamika kupata mikopo imekua shida

na kama misaada imezidi mbona deni la taifa linapaa kwa kasi ya ajabu?? bila kuona faida zake within two yrs mtu keshakopa zaidi ya trillion 20 hio misaada ilozidi inatumika wap??
Uchumi wa nchi yeyote uliokuwa umeharibiwa usitegemee utajengwa kwa miaka miwili. Soma article yangu vizuri Mheshimiwa Rais Magufuli alipochukua madaraka alikuta hali ya nchi vipi kiuchumi. Kumbuka mwaka 2005 Rais mstaafu Kikwete alipochukua madaraka alikuta hali ya uchumi wa nchi mzuri sana kwa kazi iliyofanywa na Rais mstaafu Mkapa.
 
Mbona unalia kama mfuasi wa ccyemu? Eti awamu ya tano, una akili sawasawa wewe?
Mkuu mie sina chama ila ni mtanzania ninaependa kuandika ukweli. Nina akili timamu ila wasio na akili ni wale ambao hawataki kwenda na wakati.
 
Tatizo wanataka kutudanganya kama ilivyo kawaida yao wameshaona kila mtu ni mtoto
 
nahisi ulikua unasoma huku unatembea so hata ulikua huelew sukar ametumia kama mfano mbona bidhaa ziko nyingi tu au ulitaka azitaje zote unga bei unashndana na mchele

biggest cause ya inflation rising price of neccesity commodity ambazo ndo vyakula nahisi ecos 101 ulikua huielew ulimtesa sana mwalimu wako wa macroeconomics
Una uhakika hata hiyo microeconomics anajua nn mkuu?Mungu anakuona,ths platform hadi la saba wamo so usishangae kwann hajaelewa

Ths is just the beginning,unanunua ndege 6 unalipa cash in USD,unajenga reli with 75% material unaagiza uturuki in USD,muhindi anunui mbazi zako tena,umezuia makinikia,you don't produce kuuza nje,Manufacturing imeshuka o the lowest,No foreign currency from agricultural pia and then put a blame at Bloomberg

Seriously I loved baba wataifa lakini ukweli wa Mungu hakufaulu kwny uchumi hata kidgo,and leo Gufu replicates the same policy tena unatangaz hadharani

It has never worked in Bolivia,Venezuela,Zimbabwe,etc
Socialism is cancer na mkijidanganya kuwa china ni socialist wenzenu basi we will end up naked ndio mrudi mezani
 
Back
Top Bottom