Boss Saalah wa Silent Ocean, wana Simba SC tunajua mchanganuo wa ahadi yako ya milioni 30 kama Tanzania Prisons ikiifunga Simba SC Ijumaa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,128
Boss Saalah Said Mohammed Mmiliki wa Kampuni ya Silent Ocean na Mdogo wake wa Damu Tajiri wa Yanga SC Gharib Said Mohammed tunajua kila Kitu juu ya ahadi yako ya Tsh Milioni 30 kama wakiifunga Simba SC ijumaa kwa Mkapa.

Ufuatao ndiyo Mchanganuo mzima wa hiyo ahadi ya Tsh Milioni 30 kwa Klabu ya Tanzania Prisons kutoka kwa Tajiri Mdogo Saalah Said Mohammed (SSM)

Milioni 10 wamezitoa Yanga SC kwa Tanzania Prisons FC kupitia Ndumilakuwili Saalah ya Kuwaumiza Wachezaji wa Simba SC.

Milioni 10 umezitoa Mwenyewe kwa Tanzania Prisons ili isikubali Kufungwa na Simba SC Ijumaa.

Milioni 10 amezitoa Kaka yako mkubwa Gharib Said Mohammed kwa Tanzania Prisons FC kupitia Kwako kama itafunga Simba SC.

Na ulivyo Mnafiki Tanzania Prisons FC ilivyocheza na Yanga SC yako ulitoa ahadi ya Tsh Milioni 20 wakishida na wala hukutoa ya kama ikitoka Sare /Suluhu ila kwakuwa inacheza na Simba SC usiyoipenda umeweka ahadi ya Tsh Milioni 30 ambapo wakimfunga Simba SC ila Safari hii umeweka /umetoa ahadi ya Tsh Milioni 10 kama wakikomaa na kutoka Sare.

Wape hata Tsh Milioni 100, ila hiyo Ijumaa Klabu yako unayoidhamini ya Tanzania Prisons itafungwa tu na Simba SC kwa Mkapa na wala hutoamini kabisa.
 
Na ulivyo Mnafiki Tanzania Prisons FC ilivyocheza na Yanga SC yako ulitoa ahadi ya Tsh Milioni 20 wakishida na wala hukutoa ya kama ikitoka Sare /Suluhu

Ile mechi kulikuwa na milioni kumi kama wakitoka sare na ndio maana walipaki bus la maana. Walipofungwa wote wakanywea
IMG_20221228_231052.jpg
 
Msemaji wa Simba sc,baada ya Azam kufungwa amesema wanahitaji kuongeza juhudi na pia wanataka timu zinazokutana na Yanga zishinde.wanafanyaje ili zishinde?

Yanga wapo wazi Kama wanavyoweka mikataba ya udhamini.Simba SC wanazipa hela kwa kujificha.kuipa timu motivation kwa kuahidi fedha SI kuvunja kanuni kuweni wazi Kama huyu.
 
Huu mchezo wa hawa Silent Ocean ulitengenezwa na GSM ili kubalance story, walizoea kuweka mizigo kwa timu nyingine zikicheza na Simba ili kuzihamasisha Simba ifungwe, wakadhani na Simba ingefanya hiyo michezo kwao, lakini Simba SC hawakuwa na habari nao, sasa ni aibu.

Sasa ndio ameibuka huyo Silent Ocean, ambaye tangu mwanzo nilimtilia shaka nilijua amekuja kutuliza hali ya mambo, kama vile kubalance, lakini kimsingi hao jamaa nao ni GSM tu, wote wanaifanyia kazi Yanga.

Simba acheze game zake uwanjani, huu ujinga wa GSM wawaachie wenyewe.
 
Mechi hii mwamuzi achunguzwe sana.

Upo uwezekano wa mwamuzi kuwa naye ameahidiwa,na wanaweza kuhusika kwenye kuua move za wachezaji wa Simba kama tulivyozoea kuwaona.

Wachezaji wa Prison wakianza kujaribu kuwavunja miguu,mi nawaambia tu akuanzae mmalize

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Acha kuwapangia watu na pesa zao!!, Kama vipi olewa nao. Mwanaume kutwa kusema Mambo ya kipuuzi unapakatwa wewe.
Pole sana kwa ile Popular ID yako kuwa BANNED na sasa umeamua kuja na hi ili kuendelea Kunitukana, Kunikashifu na hata Kunidhalilisha pia.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!
 
Upo mbali sama ma ukweli huyaki kuamini kwamba simba mbovu. Makonda alipowapa pesa kms wewe ulikuwa wapi?
 
Napenda namna anavyoitangaza kampuni yake ya SILENT OCEAN,na sasa ameanza kuwa gumzo,biashara inaendelea
 
Pole sana kwa ile Popular ID yako kuwa BANNED na sasa umeamua kuja na hi ili kuendelea Kunitukana, Kunikashifu na hata Kunidhalilisha pia.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!
Mama isihaka unajiitaje king wakati wewe ni mwanamke?wasalimie sana kongowe
 
Huu mchezo wa hawa Silent Ocean ulitengenezwa na GSM ili kubalance story, walizoea kuweka mizigo kwa timu nyingine zikicheza na Simba ili kuzihamasisha Simba ifungwe, wakadhani na Simba ingefanya hiyo michezo kwao, lakini Simba SC hawakuwa na habari nao, sasa ni aibu.

Sasa ndio ameibuka huyo Silent Ocean, ambaye tangu mwanzo nilimtilia shaka nilijua amekuja kutuliza hali ya mambo, kama vile kubalance, lakini kimsingi hao jamaa nao ni GSM tu, wote wanaifanyia kazi Yanga.

Simba acheze game zake uwanjani, huu ujinga wa GSM wawaachie wenyewe.
Kwahiyo unataka kusema ile mechi amabazo Prisons waliahidiwa mil 10 endapo ingetoka sare na Yanga, wangetoa sare wasingepewa hizo milioni 10?
 
Back
Top Bottom