Tetesi: Tetesi za usajili wa dirisha dogo ligi kuu Tanzania bara 2023/2024

Hichilema

JF-Expert Member
Sep 4, 2016
1,037
938
Huu ni uzi maalumu wa kupeana updates za usajili wa dirisha dogo unaotazamiwa kufunguliwa tarehe 15.12.2023. Karibu

1. Ladack Juma Chasambi ni mwekundu wa Msimbazi akitokea Mtibwa Sugar

2. Beki wa Yanga raia wa Uganda Gift Fred anahusishwa kuhitajika na Klabu ya Arab Contractors ya Misri kwa mkopo

3. Klabu ya Yanga wanaangalia uwezekano wa kumpata mshambuliaji wa Dynamo Doula , Leonel Ateba (24) .
4. Inaelezwa kuwa, Azam FC inaweza kufanya usajili wa Mlinda Lango kutoka nchini Kenya na klabu ya AFC Leopards Levis Opiyo ili kuimarisha eneo lao hilo ambalo kwa sasa Ali Ahmada, Zuber Foba na Abdulai lddrisu hakuna mwenye uhakika wa namba.

Opiyo msimu uliopita akiwa na AFC Leopards, alibeba Tuzo ya Kipa Bora katika michuano ya Mozzart Bet Cup, huku kwenye Ligi Kuu ya Kenya, akishika nafasi ya pili kwa waliokusanya clean sheet nyingi akiwa nazo 16, kinara alikuwa na 17.

4. Henock Inonga Baka anatakiwa na RS Berkane ya Morocco
5. Simba SC inawania saini ya kiungo Msenegali Sidy Sarr
5. Daniel Adrian mlinzi wa kulia kutoka Ghana ni mali ya Geita Gold

6. -Klabuya Simba sc wamefikia makubaliano ya kumsajili Eric Mbangossoum kutoka Union Touarga Sportiff,

-Vyanzo vya habari kutoka Moroco vinathibitisha kuwa wamekubali Simba sc kulipa zaidi ya $235,000 tu kama ada ya uhamisho.

7. Kiungo Mika Miche kutoka Lupopp anahusishwa na Simba SC

8. Bonaventure Bonito kiungo mshambuliaji kutoka Senegal anahisishwa na Yanga
9. Mlinzi Kelvin Kijili was Singida Fountain Gate anahusishwa na Simba SC
9. Simba SC inahusishwa na winga Kutoka Nigeria Jonathan Alukwu
10. Metacha Mnata anatakiwa na Geita Gold
11. Hernest Malonga -Diables Noirs to Simba Sports Club
12. Mohamed Mustapha -El Merriekh to Azam FC
13. Faris Ondongo kutoka AS Otoho anahitajika na Singida Fountain Gate
14. Striker Mcameroon Leon Ateba anatakiwa na Yanga
15. Simba SC inahusishwa na mchezaji raia wa Colombia Mauricio Cortes
16. Salehe Masoud kutoka JKU amesinya Simba SC

17. Augustine Okra ni mwananchi
18. Cesar Lobi Manzoki anahitajika msimbazi
19. Simba SC inahusishwa na kiungo wa Ittihad Tanger Madicke Kane

20. Striker Mzimbabwe, Michael Chalamba kutoka Chicken Inn ya Zimbabwe anakaribia kujiunga na Simba Sc
21. Simba SC inamfukuzia winga was Tanzania Prisons Edwin Barua
22..Yanga inafikiria kumtoa Jesus Morocco kwa mkopo Singida FG
23.. Winga wa As Maniema ya DRC anakaribia kujiunga na Young Africans
24. Gamba Idd kutoka JKU amejiunga na JKT
25. Babacar Sarr ni mnyama

26. Golikipa raia wa Burundi, Justine Ndikumana amejiunga na Mtibwa Sugar
27. Charles Ilanfya, Rashid Juma kutoka Ihefu pamoja na Nasoro Kapama kutoka Simba wamejiunga Mtibwa Sugar

28. Simba SC inawania saini ya kiungo mshambuliaji raia wa Gambia, Babou Cham
29. Winga kutoka Maniema, Basiala Agee anahitajika na Young Africans
30. Simba SC inafikiria kuachana na wachezaji wake. Shaban Chilunda, Steven Mwanuke, Ahmed Feruz, Mohammed Musana Nassoro Kapama
31. Yanga inamfukuzia striker raia wa DRC Kilangalanga
32. Saido, Phiri,Bocco,Kramo.Mhhh!
33. Tariq Simba kajiunga Tanzania Prisons
34. Peter Banda anakaribia kujiunga Singida Fountain Gate
35. Crispin Ngushi kajiunga Coastal Union
36. Simba SC inaangalia uwezekano wa kumsajili Hamza Regragui kutoka Wydad
 
Huu ni uzi maalumu wa kupeana updates za usajili wa dirisha dogo unaotazamiwa kufunguliwa tarehe 15.12.2023. Karibu

1. Ladack Juma Chasambi ni mwekundu wa Msimbazi akitokea Mtibwa Sugar
Asante Kwa updates muda wa mbwembwe huu
 
Hata Ulaya na Uarabuni kuna timu nyingi viongozi wanaingilia makocha e.g United, Belouzdad, Ahly eyao.
Unaizungumzia ulaya gani hii ya kina Teh Hag na Pochetino ambao mpaka sasa bado ni makocha au ulaya nyingine. Unaziona Liver na Arsenal leo zipo pale sababu,wamewapa uhuru makocha,Guardiola ndio kabisa hataki kuingiliwa.

Bongo hizi timu kubwa hamna hata mmoja ambayo ina project za muda mrefu kwa vijana ndani ya timu yao.

Simba ya Kibadeni na Julio walijaribu ila baada ya kuona mafanikio yanachelewa wakaachana na programs ya vijana.

Bongo kinacho tushindwa ni kimoja uvumilivu ,viongozi na mashabiki wote sio wavumilivu, ubaya zaidi kiongozi nae anakuwa na akili kama za shabiki maandazi za kumpa presha kocha.

Al Ahly hao unawaona,kuna wachezaji wengi wanapandishwa toka timu yao ya vijana,kwenye michuano yao ya vijana hawa okotezi vijana mitaani kama kwetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom