Bongo Star Search Season 16 Special Thread

Hiyo ni nzuri, kuongeza upambanaji na juhudi binafsi ya kila msanii. Ukiweka pesa nyingi kwa mshindi wa 2 - 5, wanabweteka wakijua pesa ipo ya kutosha.
Kwangu mimi sioni kama ni sawa

Maana mara nyingi mshindi wa 1 Hadi wa 3 huwa wanapishana kidogo sana
Na wengi wao hufeli Kwa sababu tu ya machaguo ya nyimbo, na si kwa sababu hawana uwezo.
 
Yule dada wa Mbeya alishinda bali siasa ndio zikampa ushindi binti wa Uganda
 
Naunga mkono hoja
Hili mimi nalisema tangu miaka mingi.
Mfano final ya 2015
Mshindi wa 2 Hadi 4 ,,hasa wa 4 alitakiwa ashinde
Mary Kato ,Fonabo, Frida Amani were far better than Kayumba

2018
Mshindi wa 1 na 2 walikuwa na uwezo sawa ila Phina akamzidi kete jamaa

2023 Asagwile aliyekuwa mshindi wa 2 2018akashiriki tena ndio akashibda
 
Hiyo ya Kayumba nakuunga mkono ni kwasababu Madam Rita alikuwa kipenzi chake ndio maana akashinda ila hakustahili. Waandaji wangejitahidi kutoweka gape kubwa kati ya mshindi wa Kwanza na wapili na hii ndio maana inafanya washindi wengi wasifanikiwe kwenye mziki wanakuja kutoboa wengine
 
Rita aache udikteta
Kama hawezi kuwasikiliza wenzie basi awe Jaji pekeyake
Ila siyo anaweka Majaji wengi halafu hataki wawe na maamuzi.
Nina hakika hata jana kulikuwa na malumbano pia Hadi Master akaona asuse.
 
Masterjay kakutana heka heka Kama hizo ndio maana kasusa Kwanza hakupenda Zack soul kupita kwenye ile performance alioimba nje ya key nafikiri hii ndio imechangia
 
Masterjay kakutana heka heka Kama hizo ndio maana kasusa Kwanza hakupenda Zack soul kupita kwenye ile performance alioimba nje ya key nafikiri hii ndio imechangia
Zacksoul alitakiwa kutoka ile siku ila Wakamsacrifice Jambia
Ni kweli jambia amebebwa sana Ila Ile siku hakutakuwa kutoka mbele ya Zacksoul
 
Rita aache udikteta
Kama hawezi kuwasikiliza wenzie basi awe Jaji pekeyake
Ila siyo anaweka Majaji wengi halafu hataki wawe na maamuzi.
Nina hakika hata jana kulikuwa na malumbano pia Hadi Master akaona asuse.
Baada ya kutolewa Sheridah, Rita akawa anashutumu wengine eti, alitaka hata Koy akengeushe alama zilizokuwa kwenye karatasi tayari.

Ikipendeza awe msimamizi tu, Judging awaachie wengine. Apewe KARATA 3 tu za kuingilia maamuzi ya judges, zikiisha basi.
 
Ya 3 ingemtosha. Haikuwa fair kwa Freya.
Bado hata ya 2 hakufsnya vibaya sana
Nimekaa nikaamgalia tena
Hakuharibu.

Ila Rita anatumia sana hisia kujaji
Kuliko akili.
 
Rita bwana
Halafu watuwekee majaji wenye msimamo kama master J na salama.

Eti Coy anajaji waimbaji
Sijui anajaji kitu gani

S2kizzy hajui waimbaji muendelezo wa waimbaji
Ghafla tu anaibukia kujaji
Ila Rita yaani sijui ndio anazeeka.
 
Coy anaulizwa 'umesema huyu kama Dodoma mbali aje jirani yako unamaanisha nini? Au atoke kwenye mashindano?'
Akajibu eti 'huyu atoke aende wapi, kwenye fainali yumo humu'😂
 
Coy anaulizwa 'umesema huyu kama Dodoma mbali aje jirani yako unamaanisha nini? Au atoke kwenye mashindano?'
Akajibu eti 'huyu atoke aende wapi, kwenye fainali yumo humu'😂
Mizaha yake ilivuka mipaka
Madam akamrudisha kwenye mstari
 
Mwakani watafanya juu chini Mkenya au mtanzania ashinde namba 1
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…