Heavy Weight
JF-Expert Member
- Mar 1, 2014
- 888
- 883
Wiki kadhaa nyuma kulikuwa na maandamano ya wasanii wa Bongo movie wakilalamika juu ya kudorora kwa bidhaa zao mbovu. Narudia tena kudorora kwa bidhaa zao mbovu.
Hawajui ni wapi walipoteleza lakini kiukweli hawakusoma alama za nyakati. Leo hii ukiangalia sehemu kubwa ya watu wanaosapoti upinzani hasa katika masuala ya kisiasa ni miji mikubwa na hata sehemu zenye miji midogo iliyochangamka. Watu wanaoishi katika hii miji ni wadau wakubwa waliokuwa wakisapoti bongo movie.
Tofauti na sehemu za vijijini ambako CCM ndo inaonesha kupokelewa zaidi. Sasa kitendo cha Bongo movie wengi kusapoti CCM kiliwavunja moyo wale watu wengi wa mijini kuisapoti bongo movie kwani waliona kuwa wao wamesalitiwa na Bongo movie sababu kipindi kama hiki tunalia nao shida ila ikifika wakati wa kampeni wanasapoti serikali iliyoshindwa kusikia kilio chao.
Hivyo basi salama ya Bongo movie ilikuwa kwa wao kutojikita katika siasa kama kweli walikuwa wanania ya maslahi ya kudumu, ila kwakua macho yao yalizibwa na kitambi cha JB wakaishia kuliona tumbo na kutoona mbele basi leo hii wasitulilie njaa. Kwakua hata sisi tunanjaa.