Bomu lategwa nyumbani kwa RC Mulongo

Bomu lategwa nyumbani kwa RC Mulongo

Wana - Arusha tujiulize, mbona Amani ilianza kutoweka baada 2010?
Maandamano, mapigano kati ya polisi na raia, mabomu kila mahali etc
Nafikiri unafanya 'siasa' kwenye suala lisilohitaji 'siasa'. Kama vyombo vyetu vya usalama vinafuata mawazo hayo basi tunalipalilia na kuliwekea mborea na maji tatizo!
 
Wana - Arusha tujiulize, mbona Amani ilianza kutoweka baada 2010?
Maandamano, mapigano kati ya polisi na raia, mabomu kila mahali etc
Kwa kujitoa fahamu hujambo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Who is the target in Arusha?? Why Arusha wakati wengi (wanadini+wanasiasa) wako Dar? :laugh:

Nahisi ni zaidi ya Siasa/Udini. Hii inaweza kuwa suala la kuhujumu uchumi. Especially kuumiza sector ya utalii. Nani atakayekuwa beneficiary kama utalii utaathirika? Nadhani kuna kikundi cha watu kinataka utalii uanguke. Serikali iliangalie suala hili zaidi ya Udini/Upinzani. Inawezekana hata majirani wakajaribu kuujeruhi utalii Tanzania.
 
Asubuhi hii askari Polisi na wa Jeshi wameizingira nyumba ya Serikali ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo iliyopo jirani na Mahakama Kuu Arusha wakijaribu kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kikiwa kimetegwa katika geti la kuingilia nyumba hiyo na watu wasiojilikana.

Hat kinjia kinachokatiza maeneo hayo kutokea Mt Meru Hotel nacho kimefungwa kwa muda.





Wakati huo huo kuna taarifa za usiku zikieleza watu kadhaa wamejeruhiwa katika Mgahawa mmoja maeneo ya Gymkhana Jijini hapa na wawili kati yao wako katika hali mbaya.

Hili litakuwa tukio la sita kutokea katika Jiji la Arusha ndani ya muda mfupi, kuanzia May 2013 mpaka sasa.

Tukio la kwanza lilikuwa Kanisani Olasiti watu watatu wakafa.

Baadee katika Mkutano Chadema Soweto watu watatu wakafa tena na mamia kulemaa

Ikafuata Usa River siku ya Mkesha wa mwaka mpya kwa wamama waliokuwa wanatoka kanisani

Halafu katoka Bar ya Arusha Night Park

Juzi hapa ikawa kwa nyumbani kwa Sheikh maeneo ya Majengo

Na sasa katika hiyo Vama Restaurant na chupuchupu kulipua nyumbani kwa RC!

Its purely vandalism of CMC ili kuonesha Arusha Mjini hakuna amani,,,,,,,but its all Stu,,d on the eyes of Internationa l community and the citizen of Tanzania at large
 
chadema wameharibu mji wa Arusha. Huku Dodoma hatutaruhusu huu ujinga utokee.

waliolipua Ubalozi wa Marekani pia ni CHADEMA? Au ndo sababu wakubwa wenu waliwahi kusema CHADEMA wamejilipua? Mlongo nae alitaka kujilipua? Au mnazuga ili mpate means za kumlipua mbunge wa Arusha? Hakuna ulemavu mbaya kama ulemavu wa fikra!
 
ccm wanatafuta pa kusema kwamba tokea jimbo limeshikwa na Lema ni vurugu na mauaji tu. huyo mulongo kajitegea mwenyewe hilo Bomu.
 
  • Thanks
Reactions: prs
hao polisi imekuaje wakajua kama kuna bomu hilo eneo? na ni kwanini wameweza kuwahi kwa huyo mheshiwa lakini wakashindwa kuwahi kuyagundua maeneo mengine? kuna kitu hapo hakijakaa sawa,polisi waje na maelezo mujarabu.
 
Sina hakika kwa jinsi serikali ilivyowekeza kwenye majeshi Kama ilivyooneshwa wakati wa sherehe za uhuru.Ikashindwa kulinda wananchi na Mali zao.Eeh MUNGU tuepushe hizi Mali asili ulizotujalia zisiwe laana.
 
Huu ni usanii tu. Nyumba ya mkuu wa mkoa inalindwa na FFU 24/7. Hao waliotega hilo bomu kwa nini hawakuonwa na hao askari na lilitegwa getini?

Nasema tena ni usanii.

Tiba

Uko sahihi kabisa usanii jazz band.
 
Haya matukio ni mengi hadi sasa! kimsingi tusiyausishe na SIASA.Lakini najua Rais ana hizi taarifa hvyo afanye maamuzi mapema lisijekuwa janga la kitaifa,au anasubiri waguse AICC na misifa yetu iishie hapo KIJESHI.
 
Bomu la kutegwa Ardhini utaligundua vipi?

Hii ni Sanaa unajitegea mwenyewe halafu unaita Jeshi..
 
serikali yetu ina mkono mrefu kwanini hii hali inaendelea mpaka sasa? na bado hamna taarifa rasmi? na kwanini arusha tu?
 
Nchi ya kusadikika hii kwake kunalindwa FFU masaa yote kwann wasione hilo tukio

Usanii wetu kutufanya maboya tu hawa
 
Back
Top Bottom