Bomu lategwa nyumbani kwa RC Mulongo

Bomu lategwa nyumbani kwa RC Mulongo

GanjaPlanter

Senior Member
Joined
May 27, 2014
Posts
117
Reaction score
119
Asubuhi hii askari Polisi na wa Jeshi wameizingira nyumba ya Serikali ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo iliyopo jirani na Mahakama Kuu Arusha wakijaribu kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kikiwa kimetegwa katika geti la kuingilia nyumba hiyo na watu wasiojilikana.

Hat kinjia kinachokatiza maeneo hayo kutokea Mt Meru Hotel nacho kimefungwa kwa muda.

Wakati huo huo kuna taarifa za usiku zikieleza watu kadhaa wamejeruhiwa katika Mgahawa mmoja maeneo ya Gymkhana Jijini hapa na wawili kati yao wako katika hali mbaya.

Hili litakuwa tukio la sita kutokea katika Jiji la Arusha ndani ya muda mfupi, kuanzia May 2013 mpaka sasa.

Tukio la kwanza lilikuwa Kanisani Olasiti watu watatu wakafa.

Baadee katika Mkutano Chadema Soweto watu watatu wakafa tena na mamia kulemaa

Ikafuata Usa River siku ya Mkesha wa mwaka mpya kwa wamama waliokuwa wanatoka kanisani

Halafu katoka Bar ya Arusha Night Park

Juzi hapa ikawa kwa nyumbani kwa Sheikh maeneo ya Majengo

Na sasa katika hiyo Vama Restaurant na chupuchupu kulipua nyumbani kwa RC!
 
Kwa Mlonngo hapa lingelipuka nadhani isingepita wiki walipuaji wangekamatwa
 
kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa mwenyekiti wake ni huyo Mulongo Magesa.
sasa tunategemea taarifa za kiusalama na wajibu wa kutunza usalama upo mikononi mwake.
Je! Mkuu huyu wa Mkoa anaweza kutupa taaarifa ya kuridhisgha juu ya milipuko Arusha tukianza na Olasiti mpaka huu wa kwa nyumbani kwa Sheikh?? Ni hatua gani muhimu amaechukua kiusalama kama mwenyekiti wa kamati ya usalama wa mkoa?
 
Tanzania Nchi Ya Amani Sana.Tulinde Amani Hii Isipotee Na MULONGO Asiwe Na SHAKA Hicho Ni Chuma Tu. Cc Mwigulu Nchemba
 
Last edited by a moderator:
Who is the target in Arusha?? Why Arusha wakati wengi (wanadini+wanasiasa) wako Dar? :laugh:
 
Kama Bomu limetegwa kwa Rc nani kagundua kabla ya kulipuka? Tunataka majibu ya kina? Swali lenye utata inakuwaje kwingine kote yanalipuka kwa Rc lisilipuke liteguliwe? Tunataka majibu
 
Who is the target in Arusha?? Why Arusha wakati wengi (wanadini+wanasiasa) wako Dar? :laugh:

Swali zuri sana, Arusha ndo centre of recruitment of potential terrorist, kuna viongozi wa dini wanapita wanawadanganya wazazi hasa familia maskini kwamba wanakwenda kuwasomesha watoto wao Kenya. Watoto wakifika Kenya wanashangaa kwamba mafunzo wanayopata ni karate, baadaye watoto hao hupelekwa Somalia kufanyiwa brainwashing na kufundishwa ugaidi.

Kwa taarifa za ndani ni kwamba wako wengi sana na wanaamini watu wote wasioamini wanachoamini ni makafiri na kwa hiyo wanastahili kifo.

It is time for the government to step up to confront recruiters otherwise there is more to come
 
kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa mwenyekiti wake ni huyo Mulongo Magesa.
sasa tunategemea taarifa za kiusalama na wajibu wa kutunza usalama upo mikononi mwake.
Je! Mkuu huyu wa Mkoa anaweza kutupa taaarifa ya kuridhisgha juu ya milipuko Arusha tukianza na Olasiti mpaka huu wa kwa nyumbani kwa Sheikh?? Ni hatua gani muhimu amaechukua kiusalama kama mwenyekiti wa kamati ya usalama wa mkoa?

Je kama wamejitegea? Maana dola hii ambayo sina imani nayo nitakua wa mwisho kuamini kuwa hawajajitegea.
 
chadema wameharibu mji wa Arusha. Huku Dodoma hatutaruhusu huu ujinga utokee.
 
Huu ni usanii tu. Nyumba ya mkuu wa mkoa inalindwa na FFU 24/7. Hao waliotega hilo bomu kwa nini hawakuonwa na hao askari na lilitegwa getini?

Nasema tena ni usanii.

Tiba

Ubalozi wa Marekani unalindwa na nani??? ........nilishakuambia nina wasiwasi na elimu yako.
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mwenyewe hayuko Salama. Ataweza vipi kulinda Usalama wa wengine?
 
Msifanye masihara katika masuara nyeti, sisi tuko Arusha ndo tunaface pinch

Mimi niko Chuga chalii yangu, hii mambo ni serikali inafanya. Siasa chafu za walioshindwa uongozi, huwezi niambia mabomu yoooote Arusha mpaka leo hakuna jibu la maana lililowahi kutolewa na polisi au kiongozi yeyote wa serikali.
Tuache ujinga.
 
Back
Top Bottom