Bomu lategwa nyumbani kwa RC Mulongo

Bomu lategwa nyumbani kwa RC Mulongo

chadema wameharibu mji wa Arusha. Huku Dodoma hatutaruhusu huu ujinga utokee.

Kama ulivyomjibu Tiba,nasi tunawasiwasi na elimu yako,sijawahi ona chama chenye dola na usalama wa Taifa ,watu wanatega mabomu,wanaua watu harafu viongozi wa serikali ukiwemo na wewe unasema ni chadema ndio wamelipua bomu kwa lengo lipi?
 
Serikali ya kenya haiwezi kuhusika na kama ingehusika ingefanya kiufasaha zaidi au al shabab haiwezi kutengeneza vi bomu mshenzi. Eti kwenye mkutano wa hadhara unarusha bomu unaua watu 3. Au kwenye hotel unarusha bomu unaua mtu mmoja. Al shabab wanashusha hotel nzima. Hayo mabomu ni wahuni wa arusha na bodaboda wanajaribu kuuharibu mji. Na wala si dini.
 
Kenya hawana ujanja wa kupanga na kufanya haya bila kunaswa na machampioni wetu.....ni mambo ya ndani tu ndio maana hazijawahi kutolewa sababu za kiusalama ktk matukio yote.....
 
Swali zuri sana, Arusha ndo centre of recruitment of potential terrorist, kuna viongozi wa dini wanapita wanawadanganya wazazi hasa familia maskini kwamba wanakwenda kuwasomesha watoto wao Kenya. Watoto wakifika Kenya wanashangaa kwamba mafunzo wanayopata ni karate, baadaye watoto hao hupelekwa Somalia kufanyiwa brainwashing na kufundishwa ugaidi.

Kwa taarifa za ndani ni kwamba wako wengi sana na wanaamini watu wote wasioamini wanachoamini ni makafiri na kwa hiyo wanastahili kifo.

It is time for the government to step up to confront recruiters otherwise there is more to come
Wafiadini mmeishaanza kuchafua hali ya hewa !
 
Hilo bomu halijategwa kwa ajili ya discourage utali. Vama ni restaurant ndogo sana hivyo hao sio magaidi ni vibaka hata uharibifu co mkubwa .hivyo inanifanya niamini sio al shabab.
Pili mi nashawihika sana kwamba hao walio lipua hilo bomu ni visa tu vinavyohusishwa kati yao na mkuu wa mkoa baada ya kauli ya yake kwa hao wa islam hivyo kutaka kumfundisha adabu[huo mgahawa upo krb sana na kwa mkuu wa mkoa)

Yawezekana pia, kwani pia inaleta maswali jinsi Mgahawa wa wahindi ulivyohusishwa, na sababu yaweza kuwa ni kuwepo kwake jirani na Nyumba ya RC, so walitaka kufikisha ujumbe.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa ni kikundi hichohicho kinafanya haya masumbufu yote, na tukilala usingizi wakaweza kupata "vitendea kazi" vya kisasa, Arusha haitokalika.

Pia yaweza kuwa kutokana na kuwepo kwa haya matukio mara kwa mara, basi hata watakaogombana kwa ishu zao binafsi watatumia njia hizohizo kuadhibu wagomvi wao, kwa kuamini kuwa jamii sasa imeshachanganyikiwa, na mlipa kisasi atakaa pembeni akiangalia tunavyoulizana mswali lukuki, kama hivi.
 
Kama Bomu limetegwa kwa Rc nani kagundua kabla ya kulipuka? Tunataka majibu ya kina? Swali lenye utata inakuwaje kwingine kote yanalipuka kwa Rc lisilipuke liteguliwe? Tunataka majibu

Heko sana!
Umeuliza swali nyeti lenye tafakuli kali. Majibu tafadhali Usalama wa Taifa.
 
Maswali ya kawaida kujiuliza ni kwamba; kwa nini mabomu arusha na zanzibar? what is common between the two cities? TOURISM then jiulize who is our number one competitor kwenye tourism east africa? ishu za mabomu ya arusha na zanzibar hazina uhusiano na siasa .we are closing up a gap towards the real perpetrators

Yale yale badala ya kutafuta wahalifu miongoni mwetu tunaanza kutafuta wa kumsingizia na kumbembesha mzigo! Nimetoka kujadili jinsi gani Watanzania wenzetu walipoanza kukamatwa kwa madawa ya kulevya nje ya nchi sisi turelax na kusema ni Wanegeria na Wasomali wanaiba Passport zetu. Sasa usafirishaji wa dawa za kulevya ni aibu ya Taifa.

Nahifamu Arusha kwasababu nimeishi huko karibu muongo mzima. Mabomu yanayo lipuliwa Arusha kuna mkono wa Vikundi/kikundi haramu cha dini na baadhi ya watu Serikalini/CCM wenye malengo ya kisiasa. Kundi hilo la Kidini kwa mnaokumbuka Uchaguzi wa 2010 lilitumiwa sana na CCM kuwatishia Wananchi na Wapinzani.

Hawa vijana wamekua wanafanya mazoezi ya karate na kutumia silaha ndani ya nyumba za Ibada. Wameshiriki ktk mauaji ya Mchungaji kule Mto wa Mbu. Vurugu nyingi huko Mbauda,Majengo na Unga Ltd. Wanapeleka Wapiganaji wa kujitolea Somalia,nk. Siku zote nasema Tanzania haiko salama na Alshabab kwasababu Watanzania wenzetu wanao kwenda kupigana bega kwa bega na Alshbab mwisho wanarejea nyumbani. Natarajia makubwa zaidi ambayo yatalitikisa Taifa na Dunia!
 
Asubuhi hii askari Polisi na wa Jeshi wameizingira nyumba ya Serikali ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo iliyopo jirani na Mahakama Kuu Arusha wakijaribu kutegua kinachodhaniwa kuwa bomu kikiwa kimetegwa katika geti la kuingilia nyumba hiyo na watu wasiojilikana.

Hat kinjia kinachokatiza maeneo hayo kutokea Mt Meru Hotel nacho kimefungwa kwa muda.

Wakati huo huo kuna taarifa za usiku zikieleza watu kadhaa wamejeruhiwa katika Mgahawa mmoja maeneo ya Gymkhana Jijini hapa na wawili kati yao wako katika hali mbaya.

Hili litakuwa tukio la sita kutokea katika Jiji la Arusha ndani ya muda mfupi, kuanzia May 2013 mpaka sasa.

Tukio la kwanza lilikuwa Kanisani Olasiti watu watatu wakafa.

Baadee katika Mkutano Chadema Soweto watu watatu wakafa tena na mamia kulemaa

Ikafuata Usa River siku ya Mkesha wa mwaka mpya kwa wamama waliokuwa wanatoka kanisani

Halafu katoka Bar ya Arusha Night Park

Juzi hapa ikawa kwa nyumbani kwa Sheikh maeneo ya Majengo

Na sasa katika hiyo Vama Restaurant na chupuchupu kulipua nyumbani kwa RC!

Siku zote nasema watanzania sio wajinga kiasi hii mabomu mengine yote yalipuke alafu ili mtegue, serikali inabidi siasa kwenye maisha
 
Serikali ya kenya haiwezi kuhusika na kama ingehusika ingefanya kiufasaha zaidi au al shabab haiwezi kutengeneza vi bomu mshenzi. Eti kwenye mkutano wa hadhara unarusha bomu unaua watu 3. Au kwenye hotel unarusha bomu unaua mtu mmoja. Al shabab wanashusha hotel nzima. Hayo mabomu ni wahuni wa arusha na bodaboda wanajaribu kuuharibu mji. Na wala si dini.

Sawa lakini pia tusipuuze uwezekano wa kuhusiana na mambo ya kidini, kuna watu wana uwezo wa kukaa NDANI na kikundi cha watu (zaidi vijana), wakawapika wakaiva na wakitoka huko wakafanya lolote.

Na kwa vyovyote uwepo wa vikundi kama hivyo, pamoja na udhaifu wake kiutendaji (kama ulivyomention) ni rahisi kuvutia "wazoefu" waliopo nje kuja na kuwakuza ili watekeleze matakwa yao........MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA.
 
Polisi nendeni mkakague ofisi za chadema arusha, kuna chumba kimejaa mabomu
 
zile pikipiki za chadema ndio zimepelekwa arusha kusambaza mabomu
 
Tangu Mulongo aje Arusha amani imetoweka. JK mchukue mshikaji wako umpeleke BAGAMOYO.
 
Back
Top Bottom