Hii story wanaweza kuambiwa wasio na akili ndiyo wakaamini. Kule kwenye mgahawa tunaambiwa bomu lilitupwa, hapa kwa RC lilitegwa getini. Mambo ya kujiuliza:
1. Mkuu wa Mkoa na makazi yake yanalindwa na polisi. Wakati bomu linawekwa polisi walikuwa wapi?
2. Kama nia ilikuwa kulipua makazi ya mkuu wa mkoa, kwa nini hilo bomu halikutupwa kama lilivyotupwa kule mgahawani?
3. Katika ulipuaji mabomu uliotangulia, kuna wananchi walilihisisha jeshi la polisi, serikali, TISS na CCM, na kuwa mauaji hayo yalikuwa na msukumo wa kisiasa. Wananchi walilitaka uchunguzi huru lakini serikali na polisi waligoma. Kama polisi hawahusiki, tume huru si ndiyo ingekuwa chombo cha kuwasafisha na kashfa ya kuwaua wananchi wanaotakiwa kuwalinda?
TAFSIRI - Kwa vile polisi, serikali, CCM na TISS walitajwa katika mabomu ya mwanzo, na wakakataa uchunguzi huru baada ya wao kuhusishwa, hata katika haya ya sasa itakuwa ni vigumu sana wao kutokuhisiwa na wananchi kuwa ni wahusika.
LENGO NI NINI?
1. Kuwatia hofu wananchi?
2. Akiuawawa aliyekusudiwa ionekane ni bahati mbaya maana mabomu yamekuwa yakiua au kulipuliwa maeneo mengi Arusha?
3. Ikifika wakati wa uchaguzi, upigaji kampeni uzuiwe kwa sababu ya usalama mdogo?
4. Kuna anayetafutwa akamatwe kwa kusingiziwa na ulipuaji huu?
PENDEKEZO
Kama hao wanaohisiwa na wananchi wana uhakika hawahusiki, basi serikali iridhie uchunguzi wa kamati huru ya uchunguzi kuhusiana na mambomu ya Arusha. La sivyo ni ngumu sana kuamini kuwa mabomu haya hayana mahusiano na harakati za kisiasa.