Bomoabomoa ya kufa mtu Dodoma inaendelea

Bomoabomoa ya kufa mtu Dodoma inaendelea

Hapana ni hivi like eneo ni la railway ata kuangalia kuna baadhi ya miundombinu ya shirika la reli ila imeachwa .

Ishu ni ivi like eneo ilikuwaga Mali ya railway manispaa ndo wakawa wameomba shirika la reli waanze kulitumia wakawaruhusu kulitumia lakini kwa shughuli temporary sasa manispaa wao wakajenga masoko hadi stand wakawa wanakusanya ushuru pia wakawauzia na wafanya biashara kama akina shabby wakajenga halimashauri wakajenga na ukuta wa stand kutoza ushuru vizuri ndo railway wakawawekea bomoa ndo ishu imeenda mahakamani railway wameshinda miundombinu ya manispaa yote inaondoka yakiwemo masoko na stand .Kama utakuwa unapafahamu utaona kabisa kama Ile stand ya kisasa ipo katika makazi ya wafanyakazi wa reli.

Kingine usisahau wale wanajenga reli za kisasa wanaandaa mazingira kwa ajiri ya bandari kavu.Nachokisema nakijua kwa asilimia zote mkuu
Kumbe
 
DODOMA: Kampuni Hodhi ya Usimamizi wa Reli (RAHCO) wameanza kubomoa nyumba zilizo karibu na hifadhi ya reli kupisha ujenzi wa reli ya kisasa

Wananchi walioathirika na zoezi hilo wamesema wamepewa muda mchache wa kuhama na mali zao zimeharibika na kuwasababishia hasara kubwa

Ofisa uhusiano wa RAHCO, Catherine Mushi amesema walitoa notisi ya kuwabomolea tangia mwezi Novemba mwaka jana

Bomoa bomoa hiyo linategemewa kuchukua siku 3 hadi 5 na watu walio katika hifadhi ya reli hawatalipwa




===============================

Hivi sasa hapa Dodoma ineandelea bomoabomoa ya kufa mtu.Vibanda vya biashara vingi vimenjwa ikiwa ni pamoja na ofisi za Shabiby na kituo cha mafuta cha ORYX kilichokuwa nyuma ya jengo la Shabiby.

Jengo la kampuni ya mabasi ya Shabiby lilikuwa bado jipya kabisa baada ya kulijenga upya hivi karibuni.

Kituo cha mafuta cha TOTAL kilichokaribu na stand ya Jamatani wao angalau wamefanikiwa kuokoa pump zao na wananyonya mafuta yaliyoko chini kwenye matenki.

Benki ya NMB nao ndio wanajaribu kuokoa mashine zao 3 za ATM zilizokuwakuwa zimefungwa katika kituo hiki cha mafuta cha TOTAL.

Kwa ujmla watu wengi sasa wanahangaika kuokoa mali zao.Zoezi limeanza saa 10 jioni hii na kuna taarifa wananchi walitangaziwa ingawa wengine wanasema hawakutarajia kuwa itakuwa ni leo.

Ukweli ni kuwa ajira nyingi sana zisizo rasimi zimeathirika maana vibanda vya biashara vilivyovunjwa ni vingi mno na eneo lililoathirika ni kubwa sana.

Eneo hili tunaambiwa ni mali ya Shirika la Reli nchini.

Ulinzi ni mkali.

Kwa hili zoezi hakika walitoa Notice na waliweka X kubwa ila cha ajabu watu walizifuta siku hiyo hiyo kwa hiyo Dhawabu za Kiburi ndiyo kama Ilivyo Hakuna Mtu aliyekuwa na Mwenye kiburi kama Shabiby Wamevunja kweli na hakuna hata Tanki lilooklewa kwa lile shell iliyokuwa karibu na Shabib
 
Poleni jamani, ha[a ni zaidi ya majanga
mategemeo ya familia yamepoyea kabisa kwani ajira zimepotea
na wengi walitaji kusomesha na kujiwekea vipato
 
Poleni jamani, ha[a ni zaidi ya majanga
mategemeo ya familia yamepoyea kabisa kwani ajira zimepotea
na wengi walitaji kusomesha na kujiwekea vipato
c3e7c5b5b46ca2338096715f7d00e323.jpg
e07fa819e67150d985fad99da4917555.jpg

Ofisi za mabasi ya ABC
7d6794c4728251937e8ae0c0afff9d67.jpg

(Kwa Mwansasu) ilipokuwa Railways Club kulikokuwa kukifanyika vikao vya sherehe kila mwishoni mwa juma pia ofidi za mabasi ya Safari Njema
00daf0f8569f666d40760d64b98a3f7f.jpg

Sun Set (Mpepo au kwa Kimei)
df3fe65e24a98ea40aab5a0db7aa1259.jpg

nyuma ya stand ya Daladala za Mjini (Artic open Bar) inapopakana na ukuta wa Kanisa la Kilutheri
b46743d7caf3d272483639cb4c7382a4.jpg
 
Inasikitisha! Hawa ni wakosaji na serikali ina haki ya kubomoa lakini, ukiwasikiliza uelewa wao uko chini kiasi cha kufahamu kosa lao. Serikali ikishafahamu ufahamu wa raia wake, inastahili ielewe mbinu ya kuwaelewesha. Tangu Dar, Moro, Dodoma, Tabora, Shinyanga, Mwanza kote huko ni mijini na uelewa uko chini. Bomoa ya aina hii ilihitaji uvumilivu wa masaa kadhaa ili waondoe mali zao za kuhamishika lakini naona mtindo umekuwa kama wa Mgambo wa jiji.

Hata hivyo baadhi ya watu ambao hawajitokezi ktk picha kama hizi, ufahamu wao uko juu na walifanya kwa makusudi. NIliwaona pale Dar kwenye godowns za wafanyabiashara zikiwa zimeinamia reli.
 
Sheria inafuata mkondo! Uzuri hakuna anayeonewa, wako watu walijua wana makosa ila wakawa wanademadema wakati wa awamu zile. Sasa awamu ya utekelezaji iko kazin
SAWA. JE JAMTIN NA LILE KANISA PALE KAMA UNAELEKEA SARAFINA BAR, VIPI NA ZENYEWE. JE ZIMEVUNJWA?
 
Back
Top Bottom